Askofu Dkt. Bagonza amshukia Lugola kwa kumfananisha Magufuli na Yesu. Asema hii laana lazima itafune mtu na Taifa

Askofu Dkt. Bagonza amshukia Lugola kwa kumfananisha Magufuli na Yesu. Asema hii laana lazima itafune mtu na Taifa

KOMA kumfananisha YESU na midude mingine
Na ukitaka kupata impact ya huo ulinganisho ambao wengine wanautolea utetezi hebu hili la Yesu tuliweke pembeni halafu badala yake tumweke Mtume Mohamad afananishwe na Magufuli tuone waislamu watakavyo react.Haya mataga akili hayana Lugola Jibaba zima hovyo kabisa.
 
Hakuna mahali Kangi amemfananisha Yesu Kristo mwana wa Adamu na Rais Magufuli, bali ametumia neno kama, neno ambalo halina mfanano wa moja kwa moja na kitu husika, Sasa wewe kwa akili yako unadhani YESU KRISTO MWANA WA ADAMU Anaweza kufananishwa na Mwandamu hapa duniani ingawa na Yeye YESU KRISTO alikuwa ni mwanadamu???? 😫👂

Ile tafsiri ya neno kama niliyo iweka katika hoja yako ina eleweka vizuri ,na mwanzo uliunga mkono hoja ya Lugola.
 
Kuna mtu aliwahi kusema kuwa huyu mzee alikuwa anaishi marekani, baada ya kurudi kwenye hilo kanisa akatoa rushwa kwa viongozi wa kanisa na kumfitinisha askofu aliyekuwapo kisha akapewa yeye hiyo nafasi, tena akawa na tuhuma ya kutembea na wake za watu kama si waumini wake
Kwa hiyo ana mapungufu makubwa,
Na mtu aliyeseam hayo ni mtu wa huko kwake anakoongoza hilo kanisa.
Kama alitubu akasamehewa basi asijifanye kuwa mtakatifu yeye na kuona kibanzi machoni mwa wengine wakati yeye analo liboriti mwilini mwake.
Mkuu..ile tuhuma ya kudeti na binti ya kaka yako iliisha vipi, ama mlimaliza ilo SAGA kifamilia zaidi?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ile tafsiri ya neno kama niliyo iweka katika hoja yako ina eleweka vizuri ,na mwanzo uliunga mkono hoja ya Lugola.
Mkuu wacha nilale, tutaonana asubuhi nikiamka, asante kwa uelewako tofauti na wengine wenye matusi kwenye hoja zao.
 
Mkuu wacha nilale, tutaonana asubuhi nikiamka, asante kwa uelewako tofauti na wengine wenye matusi kwenye hoja zao.

Wewe Lala tu Mkuu wangu ila wakati mwingine jifunze kujibu kwa Hoja ili kuonesha mapungufu katika Hoja ya mwingine.Sija mtukana Mtu zaidi ya kutaja Sifa za Watu kutokana na kauli zao.
 
Mkuu ebu jibu ulichoulizwa na mkuu kikulachako.

Nimesha mjibu ,huu sio mjadala wa Dini ila ni mjadala wa Siasa kuchanganywa na Dini ili kuwalaghai Watu wengine wasio fikiri zaidi ya wanavyo fikiri.
 
Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
___________
Kufuru haina kinga. Kwa Wakristo, dhambi isiyosameheka katika Agano Jipya ni kumkufuru Roho Mtakatifu. Na katika Agano la Kale ni ibada ya sanamu (idolatry). Amri ya kwanza aliyopewa Musa inasema, "Mimi ni Bwana Mungu wako, usiwe na miungu mingine" (Kutoka 20:3-6).
_
Kufuru haina kinga duniani wala mbinguni. Ghadhabu ya Mungu iko wazi katika vitabu vyake vyote.

Tuzitendee haki kumbukumbu zetu;

1. Mwaka 2005 mjinga mmoja alitumia uhuru wake vibaya huko Denmark. Akachora katuni yenye kumdhihaki Mtume Muhammad (S.A.W). Dunia nzima iliwaka moto.

2. Mwaka 2010 mpuuzi mwingine huko Marekani akachoma moto Quran tukufu. Hakuna jiwe lililosalia juu ya jiwe.

3. Mwaka 2012 huko Mbagala utoto ukavuka mipaka. Msahafu ukakojolewa. Amani yetu ilitoweka kwa muda. Majivu yakawa majivu.

4. Huko Sumbawanga, msimu wa uchaguzi kama huu, ulimi wa mmoja uliteleza. Akaufananisha UTATU mtakatifu na mafiga matatu ya chama chake. Hapakutosha. Mzee Pinda (mtu wa amani), ana cha kusimulia mpaka leo.

Mungu wetu hafananishwi. Mungu wetu halinganishwi. Mungu wetu hashindanishwi. Ni ibada ya sanamu kupenda kitu kingine kuliko unavyompenda Mungu wako. Ni ibada ya sanamu kuchukia kitu kingine kuliko unavyomchukia shetani. Ni ibada ya sanamu kumlinganisha Muumbaji na uumbaji wake.

Hatumtendei haki Mungu kumlinganisha na aliowaumba. Hatuwatendei haki wale tuwapendao kwa kuonesha kuwa tunawapenda kuliko tunavyompenda aliyewaumba.

Walinzi na waangalizi wa imani (viongozi wa dini), kama hatuwezi kukemea hili (la Lugola) basi angalau tuchukie na tuonekane kweli tumechukizwa.!
Asante sana Baba Askofu kwa Maonyo yako Mungu hadhihakiwi
 
“Ye men of Galilee, why stand ye gazing up into heaven? this same Jesus, which is taken up from you into heaven, shall so come in like manner as ye have seen him go” (Acts 1:11).
Hatimaye ujio wa pili umetimia, 'yesu' ametua bongo.
 
Back
Top Bottom