Askofu Dkt. Bagonza amshukia Lugola kwa kumfananisha Magufuli na Yesu. Asema hii laana lazima itafune mtu na Taifa

Askofu Dkt. Bagonza amshukia Lugola kwa kumfananisha Magufuli na Yesu. Asema hii laana lazima itafune mtu na Taifa

Lugola hana kosa lolote.

Yesu alikua binadamu kuna ubaya gani kumlinganisha na Magufuli?

Yesu alifanya makubwa kama binadamu na ndio hayo Magufuli anafanya. Kuna ubaya gani?
 
Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
___________
Kufuru haina kinga. Kwa Wakristo, dhambi isiyosameheka katika Agano Jipya ni kumkufuru Roho Mtakatifu. Na katika Agano la Kale ni ibada ya sanamu (idolatry). Amri ya kwanza aliyopewa Musa inasema, "Mimi ni Bwana Mungu wako, usiwe na miungu mingine" (Kutoka 20:3-6).
_
Kufuru haina kinga duniani wala mbinguni. Ghadhabu ya Mungu iko wazi katika vitabu vyake vyote.

Tuzitendee haki kumbukumbu zetu;

1. Mwaka 2005 mjinga mmoja alitumia uhuru wake vibaya huko Denmark. Akachora katuni yenye kumdhihaki Mtume Muhammad (S.A.W). Dunia nzima iliwaka moto.

2. Mwaka 2010 mpuuzi mwingine huko Marekani akachoma moto Quran tukufu. Hakuna jiwe lililosalia juu ya jiwe.

3. Mwaka 2012 huko Mbagala utoto ukavuka mipaka. Msahafu ukakojolewa. Amani yetu ilitoweka kwa muda. Majivu yakawa majivu.

4. Huko Sumbawanga, msimu wa uchaguzi kama huu, ulimi wa mmoja uliteleza. Akaufananisha UTATU mtakatifu na mafiga matatu ya chama chake. Hapakutosha. Mzee Pinda (mtu wa amani), ana cha kusimulia mpaka leo.

Mungu wetu hafananishwi. Mungu wetu halinganishwi. Mungu wetu hashindanishwi. Ni ibada ya sanamu kupenda kitu kingine kuliko unavyompenda Mungu wako. Ni ibada ya sanamu kuchukia kitu kingine kuliko unavyomchukia shetani. Ni ibada ya sanamu kumlinganisha Muumbaji na uumbaji wake.

Hatumtendei haki Mungu kumlinganisha na aliowaumba. Hatuwatendei haki wale tuwapendao kwa kuonesha kuwa tunawapenda kuliko tunavyompenda aliyewaumba.

Walinzi na waangalizi wa imani (viongozi wa dini), kama hatuwezi kukemea hili (la Lugola) basi angalau tuchukie na tuonekane kweli tumechukizwa.!
Tatizo sio wakuu wa makanisa; bali ni huyo aliyefananishwa na mola kukaa kimya!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lugola hana kosa lolote.

Yesu alikua binadamu kuna ubaya gani kumlinganisha na Magufuli?

Yesu alifanya makubwa kama binadamu na ndio hayo Magufuli anafanya. Kuna ubaya gani?

Absurd and Non-sense!
 
Lugola hana kosa lolote.

Yesu alikua binadamu kuna ubaya gani kumlinganisha na Magufuli?

Yesu alifanya makubwa kama binadamu na ndio hayo Magufuli anafanya. Kuna ubaya gani?
Mbona wabunge/wawakilishi wa Zanzibar walimcharukia mbunge mwenzao (Mwezi uliopita) kwa kile kinachodaiwa kumkashifu ...Mt... ambaye alikuwa binadamu kwa 100%? Sembuse Yesu ambaye ni Mungu? Acha kudhihaki imani za watu kama Lugola alivyofanya.
 
Yesu Ni binadamu kwa 100% sio mungu,MUNGU hawezi kufa.wala kuteswa
 
Nimesikiliza mchango wa Mhe. Kangi Lugola kwenye Bajeti Kuu ya Serikali 2020/21 inasikitisha na imekosa focus.
Mhe. Kangi Lugola hakupashwa awe Bungeni huyu Fisadi mkubwa na mlarushwa aliyebobea. Neno la Mungu linasema: AMRLAANIWA AMTUMAINIYE MWANADAMU! Sifa zote alizoimba na mapambio yote kwa Rais Magufuli kiasi cha kumfananisha na Bwana Yesu Kristo hakika ni kufuru kwa Mwenyezi Mungu na Kangi Lugola atavuna hichi alichopanda maana Mungu hadhihakiwi!
Msamaha wa Rais Magufuli kwa MAFISADI WA CCM ndani ya Jeshi la Magereza chini ya Adengenye na Kangi Lugola ndiko kumepelekea Lugola kumwona Magufuli Kama Mungu wake.....!

Mfungwa wa kisaisa huyo
 
Back
Top Bottom