Askofu Dkt. Bagonza amshukia Lugola kwa kumfananisha Magufuli na Yesu. Asema hii laana lazima itafune mtu na Taifa

Askofu Dkt. Bagonza amshukia Lugola kwa kumfananisha Magufuli na Yesu. Asema hii laana lazima itafune mtu na Taifa

Bagonza anafikili anaweza kuchukua nafasi ya mungu? Hawezi ku finally hukumu ya mungu kwa binadamu hata siku moja, pia akumbuke kuna watu wanaitwa yesu hapa duniani kwa maana hiyo hao hawatasamehewa kwa vile wamejiita jina la yesu?

Pia lazima ajue mfano sio lazima iwe kitu halisi,
Ujuaji anaotaka kujifanya anao Bagonza unamuondolea hadhi ya kuwa Askofu.

Kuna wanasiasa wanasema uongo na anajuwa wanasema uongo na wengine ni waumini wake mbona hatujaona andiko kuwakemea ili waache uongo kwa kuwa vitabu vya dini vinasema usimsemee mtu uongo, pia uongo ni zaidi ya mchawi, sasa hilo halijui?

Mapenzi yake kisiasa hayamzuii kuacha uaskofu ili aje apambane kama mwanasiasa kwa kuwa yeye hatakuwa wa kwanza, kuna Dr slaa, kuna marehem rwakatale kuna msigwa na wengine wengi.
Yeye anashambulia upande wa CCM tu je huko Upinzani ni watakatifu?

Maaskofu wa hivi laana zao watazibeba wenyewe maana mungu anaiona mioyo yao inavyohangaika na maovu wanayowaza kika siku.
Bagonza ajitathimini.
Mpumbavu mmoja anaandika "CCM",lakini anaandika "mungu" na "yesu". Upumbavu ni kipaji kumbe.
 
Siku moja askofu Munga alijaribu tu kuwaonya mkambagaza na maneno ya hovyo wakati mnajuwa huyo ni member wenu itakuwa CCM kumshukia askofu mwanachama wa chadema?
Tulieni munga anajijua madhaifu aliyonayo, na kama hajui basi mungu anayajua
Akafanye toba mungu atamfunulia tu.
Mpumbavu mmoja anaandika "CCM",na pia anaandika "mungu". Kweli wapumbavu mmejazana huko.
 
Lazima amuite Yesu sababu amemuokoa kukaa gerezani kwa wizi mkubwa aliufanya mpaka sasa yupo uraiani na wakati kuna watu wapo mahabusu kwa milioni 17 za uonevu
 
Ila wakristo kidogo tunakuwaga na huruma sana, angetolea huo mfano wake kwa kumlinganisha na yule wa upande mwingine, asingeamini huo moto wake.. Angeshatoka kwenye vyombo vya habari kuomba radhi..!
 
Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
___________
Kufuru haina kinga. Kwa Wakristo, dhambi isiyosameheka katika Agano Jipya ni kumkufuru Roho Mtakatifu. Na katika Agano la Kale ni ibada ya sanamu (idolatry). Amri ya kwanza aliyopewa Musa inasema, "Mimi ni Bwana Mungu wako, usiwe na miungu mingine" (Kutoka 20:3-6).
_
Kufuru haina kinga duniani wala mbinguni. Ghadhabu ya Mungu iko wazi katika vitabu vyake vyote.

Tuzitendee haki kumbukumbu zetu;

1. Mwaka 2005 mjinga mmoja alitumia uhuru wake vibaya huko Denmark. Akachora katuni yenye kumdhihaki Mtume Muhammad (S.A.W). Dunia nzima iliwaka moto.

2. Mwaka 2010 mpuuzi mwingine huko Marekani akachoma moto Quran tukufu. Hakuna jiwe lililosalia juu ya jiwe.

3. Mwaka 2012 huko Mbagala utoto ukavuka mipaka. Msahafu ukakojolewa. Amani yetu ilitoweka kwa muda. Majivu yakawa majivu.

4. Huko Sumbawanga, msimu wa uchaguzi kama huu, ulimi wa mmoja uliteleza. Akaufananisha UTATU mtakatifu na mafiga matatu ya chama chake. Hapakutosha. Mzee Pinda (mtu wa amani), ana cha kusimulia mpaka leo.

Mungu wetu hafananishwi. Mungu wetu halinganishwi. Mungu wetu hashindanishwi. Ni ibada ya sanamu kupenda kitu kingine kuliko unavyompenda Mungu wako. Ni ibada ya sanamu kuchukia kitu kingine kuliko unavyomchukia shetani. Ni ibada ya sanamu kumlinganisha Muumbaji na uumbaji wake.

Hatumtendei haki Mungu kumlinganisha na aliowaumba. Hatuwatendei haki wale tuwapendao kwa kuonesha kuwa tunawapenda kuliko tunavyompenda aliyewaumba.

Walinzi na waangalizi wa imani (viongozi wa dini), kama hatuwezi kukemea hili (la Lugola) basi angalau tuchukie na tuonekane kweli tumechukizwa.!
Ujinga mwingine ni tatizo. Haiingii akilini kusikia MTU anatolea mfano ghafla Askofu unageuza huo mfano kuwa laana ya taifa.
Shule ya maisha ni bora kuliko shule hii Bagonza.
 
Ila wakristo kidogo tunakuwaga na huruma sana, angetolea huo mfano wake kwa kumlinganisha na yule wa upande mwingine, asingeamini huo moto wake.. Angeshatoka kwenye vyombo vya habari kuomba radhi..!
Aah wapi sio tz
 
Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
___________
Kufuru haina kinga. Kwa Wakristo, dhambi isiyosameheka katika Agano Jipya ni kumkufuru Roho Mtakatifu. Na katika Agano la Kale ni ibada ya sanamu (idolatry). Amri ya kwanza aliyopewa Musa inasema, "Mimi ni Bwana Mungu wako, usiwe na miungu mingine" (Kutoka 20:3-6).
_
Kufuru haina kinga duniani wala mbinguni. Ghadhabu ya Mungu iko wazi katika vitabu vyake vyote.

Tuzitendee haki kumbukumbu zetu;

1. Mwaka 2005 mjinga mmoja alitumia uhuru wake vibaya huko Denmark. Akachora katuni yenye kumdhihaki Mtume Muhammad (S.A.W). Dunia nzima iliwaka moto.

2. Mwaka 2010 mpuuzi mwingine huko Marekani akachoma moto Quran tukufu. Hakuna jiwe lililosalia juu ya jiwe.

3. Mwaka 2012 huko Mbagala utoto ukavuka mipaka. Msahafu ukakojolewa. Amani yetu ilitoweka kwa muda. Majivu yakawa majivu.

4. Huko Sumbawanga, msimu wa uchaguzi kama huu, ulimi wa mmoja uliteleza. Akaufananisha UTATU mtakatifu na mafiga matatu ya chama chake. Hapakutosha. Mzee Pinda (mtu wa amani), ana cha kusimulia mpaka leo.

Mungu wetu hafananishwi. Mungu wetu halinganishwi. Mungu wetu hashindanishwi. Ni ibada ya sanamu kupenda kitu kingine kuliko unavyompenda Mungu wako. Ni ibada ya sanamu kuchukia kitu kingine kuliko unavyomchukia shetani. Ni ibada ya sanamu kumlinganisha Muumbaji na uumbaji wake.

Hatumtendei haki Mungu kumlinganisha na aliowaumba. Hatuwatendei haki wale tuwapendao kwa kuonesha kuwa tunawapenda kuliko tunavyompenda aliyewaumba.

Walinzi na waangalizi wa imani (viongozi wa dini), kama hatuwezi kukemea hili (la Lugola) basi angalau tuchukie na tuonekane kweli tumechukizwa.!
Alafu ww Kangi Lugola acha kumshambulia baba Askofu
 
Lazima amuite Yesu sababu amemuokoa kukaa gerezani kwa wizi mkubwa aliufanya mpaka sasa yupo uraiani na wakati kuna watu wapo mahabusu kwa milioni 17 za uonevu
Hizo nyingi mbona,elf 20 tu kakosa kazi plus fine milioni moja na nusu plus za kuhonga ili kesi iishe haraka.Aliona heri kununua Uhuru wake ili aisozee jela,kwa kupima kipi muhimu Kati ya familia au kukaa ndani miaka ili kusubiria hizi kesi za uonevu hazina dhamana hata Kama sh 500 ukituhumiwa nazo ujui mwaka gani utatoka.
Wengi wako ndani wa 5 Sasa wanasubiria ushahidi toka mbinguni labda
 
Hatuwezi kunyamazia upuuzi wa wabunge kumfananisha mtu na Mungu kamwe hatuwez, hii ni kufuru ngoja tumwombe Mungu atajibu tu

Huyu Ndugai na CCM pamoja na Wabunge wao wamelewa MADARAKA kiasi cha kumfananisha Magufuli na Bwana Yesu Kristo, Mungu Mkuu muumba wa Mbingu na nji. Hakika Mungu atalipa kisasi kwa kufuru hii!
 
Askofu Bagonza ni kweli kabisa umefika wakati kwake kuvua majoho ya uaskofu na kupanda jukwaani.

Acheni propaganda za kijinga enyi nzi wa KIJANI. Mbona wakti wa Corona mliwaagiza Maaskofu kupitia Magufuli ili waombe kwa ajili ya Tanzania? Leo Askofu kumkemea Lugola kwa DHAMBI ya KUKUFURU mnamgeuza kuwa MWANASIASA....!!! Non-sense!
 
Shida ya Mzee wangu Bagonza amejaa chuki, Chuki Imemjaa hata kwenye vitu vidogovidogo tu.
Tatizo lako wewe ni Mapenzi kwa Lugola mpaka unawachukia wengine kisa tu kumkosoa Lugola wako!!!!
 
Back
Top Bottom