Pre GE2025 Askofu Dkt. Benson Bagonza aimiminia sifa na pongezi Serikali ya Rais Samia kwa kutekeleza Miradi ya Maendeleo

Pre GE2025 Askofu Dkt. Benson Bagonza aimiminia sifa na pongezi Serikali ya Rais Samia kwa kutekeleza Miradi ya Maendeleo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu watanzania,

Haya ni maneno ya Mtumishi wa Mungu Askofu Dkt Benson Bagonza

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

====

1727180798530.png

Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Karagwe, Dk Benson Bagonza ameipongeza serikali kwa kuhakikisha inarudisha kodi za wananchi kwa kutekeleza miradi ya kisasa ya barabara.

Dk. Bagoza ametoa pongezi hizo leo katika uzinduzi wa barabara ya lami yenye mita 700 Kishao Lukajange ambapo amesema serikali imeendelea kuwa na uaminifu wa kukusanya fedha za wananchi na kuzirudisha katika jamii kwa kutekeleza miradi imara ikiwemo barabara nzuri.

Pia soma: Askofu Mkuu Kanisa la AICT atoa tamko Mpina kufukuzwa bungeni

Amesema barabara hiyo ambayo inaelekea katika makao makuu ya Dayosisi ya Karagwe imekuwa kiunganishi kikubwa kati ya wananchi na waumini na kuondoa vikwazo kwa wanachi ambao zamani walishindwa kuhudhuria ibada kwa kisingizio cha matope.

Habari Leo
 
Usivyo na akili kumwelewa Bangoza itakuchukua miaka 50 ijayo
barabara imejengwa na serikali sikivu ya CCM chini ya kiongozi wetu makini sana na kipenz cha waTanzani Dr.Samia Suluhu Hassan, na Askofu Dr. Bagonza ameiona kazi ya barabara hiyo na ameipongeza serikali kwa kazi hiyo nzuri sana kwa manufaa ya wanainchi...

unahitaji kupigwa virungu na polisi ndio mtu aelewe jambo wazi kama hilo kweli?🐒
 
..Ni barabara ya mita 700?
 
Back
Top Bottom