Mkuu, hebu nisikilize vizuri, binafsi sina dini na siipendi, humu jukwaani nimeliweka wazi kabisa,
Tanzania kuna udini mkubwa sana, tena wa kutisha kuliko hata ukabila. Uzuri ni kwamba wazee wa TANU na CCM chini ya Raisi Nyerere walijitahidi kutengenisha dini na uongozi. Huu ndiyo ulikuwa utaratibu wetu, kwamba mbali na watu kuwa na dini zetu, hicho siyo kigezo cha kuwa kiongozi.
Watu waliliamini hili sana, japo mara chache kumekuwepo na matukio madogo madogo (Sporadic Events) za vurugu za kidini. Ila wakati wote serikali ilisimama imara kwasababu ya imani kwamba nchi ni yetu sote. Kuna wakati Mzee Nyerere aliitisha uchunguzi kwenye baraza la mawaziri baada ya malalamiko kwamba wamejaa wakatoliki, na mwishowe ikaoneka yalikuwa ni majungu.
Tatizo linakuja pale ambapo tumepata kiongozi ambaye hajachanga karata zake vizuri. Hili sakata lilipoanza, watu walianza kusema Uzanzibar na Uarabu. Ila watetezi wa mama wakaja na hoja kubwa kwamba, mama anachukiwa kwasababu ni Muislamu. Shida ilianzia hapa. Aheri wasingelisema kabisa hili, maana ukweli ni kwamba watangulizi wake kama Jakaya na Magufuli walishambuliwa mno, ila hoja za udini hazikuwa kama ilivyo sasa.
Yote haya chanzo ni rushwa na mkataba mbovu wa DP World. Wanakwepa ukweli kwamba hili ndiyo tatizo, na wanaenda kwenye hoja za dini. Unadhani hii michezo ya kuzunguka makanisani ndiyo itaenda kutatua matatizo. AU unadhani sisi hatufahamu nini kinachozungumzwa huko kwenye vikao vya ndani vya maaskofu na mashekhe, ???
Raisi aliyaona haya mapema kabisa, kwanini hakutoka hadharani kuwakemea wafuasi wake wanaotumia dini kumtetea. Mzee Nyerere alishawahi kuwaandikia barua kali mno maaskofu baada ya Mzee Rugambwa na wenzake kutaka kuingilia baadhi ya mambo. Hata Kikwete alipoona Masheikh wa dini yake wanatumia dini kwenye siasa aliwaweka ndani. Raisi Samia zaidi ya kusema Tanzania ni moja tu, akiongelea Uzanzibar na Utanganyika, wapi alikemea hizi propaganda za kidini zinazopigwa mtandaoni na waumini wenzake, ???
Kiukweli, mdharau mwiba mguu huota tende. Sasa huo mkataba unaendelea kuligawa taifa, anaukumbatia wa nini, ??? Kama ni uwekezaji bandarini kwanini asitangaze tenda kwa makampuni mengine ya kimataifa, ???