Askofu Dkt. Fredrick Shoo: Tusiwagawe watu kwa misingi ya dini

Askofu Dkt. Fredrick Shoo: Tusiwagawe watu kwa misingi ya dini

Wanaukumbi.

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dkt. Fredrick Shoo ameiomba Serikali kukataa na kukemea kwa nguvu yote wale wote wanaoonesha dalili za kuwagawa watu kwa utofauti wa Dini na kusema hata pale Mtu anaposema jambo la kuipendeza Serikali iwapo amejenga hoja yake katika msingi wa kuwagawa Watu kidini au kwasababu nyingine yoyote akemewe kwakuwa hana nia njema.

Dkt. Shoo amesema hayo mbele ya Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa Maadhimisho ya
Miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) katika

Chuo cha Tumaini Makumira, Arusha leo August 21,2023.

Dkt. Shoo amenukuliwa akisema
"Umoja wa Taifa letu la Tanzania, mshikamano ni muhimu kuliko Mtu au kundi lolote, niwaombe Viongozi wenzangu wa Dini zote, niwaombe Wanasiasa, kuacha kabisa kujaribu kuwagawa Watu kwa misingi ya Dini au kwa misingi ya itikadi iwayo yoyote ya kisiasa na kwa misingi ya maslahi binafsi"

"Niombe Serikali yako kukataa na kukemea kwa nguvu yote wale wote wanaoonesha dalili za kutugawa kwa utofauti wa Dini zetu, hata pale Mtu anaposema jambo la kuipendeza

Serikali iwapo amejenga hoja yake katika msingi wa kutugawa kidini au kwasababu nyingine yoyote huyo akemewe, tumkatae hana nia njema"

Chanzo: Millard Ayo.

Kwa maneno mengine alichokisema askofu shoo ni kuwa, kama dhehebu ama taasisi za kidini zipo zliyopongeza uwekezaji wa dp world na hakuna aliyesema jambo kukemea, basi ikitokea taasisi ama dhehebu lingine la dini lilakosoa basi lisitishiwe kwa mlango wa kuingiza dini kwny siasa, na kwamba mtamkaji ndie wa kukemewa kwa kuleta udini.

Ukianza kupongezwa basi jitayarishe kukosolewa. BTW, dini ni Siasa iliyosoma
 
Naamini anawaambia wanasiasa ambao Nina HAKIKA hawajaenda hapo kusali, Wana agenda zao.

Mkataba na DP world ni fake batili ufutwe haraka.
Wanasiasa pamoja na maaskofu na mawaraka yao.
 
Huyo mswahili ana matatizo, anaonekana wazi leo ndio alikuwa anategemea yeye na mamake watapata angalau pointi ya kujitetea lakini wapi, hali yao bado mbaya sana hawa viumbe.
nadhani unemsikia Bana Askofu Shoo, anampongeza Rais kwa utulivu wake wakati huu wa mawimbi ya asubuhi, tuna imani sana na Rais

Mwisho wa Mtanange huu kuna Taasisi zitapata lesson mpya kuwa mipaka yao ya kutoa maelekezo na maagizo hayavuki nje ya majengo yao na kwa wafuasi wao
 
Na kweli mimi binafsi siwachukii Waislam kabisaa wala sina tatizo nao. Pia nina ndugu wa damu Waislam wengi kabisa. Ndugu na baadhi ya rafiki zangu Waislam ni wakweli na hawana dhuluma. Ni watu wema. Mwenyezi Mungu anayejua kila mtu anachowaza na kutenda Awaangamize wote wanaoeneza chuki za udini hapa Tanganyika! Ni wapumbavu kwa sababu si wasomi wa lo lote lile na nahisi wana akili ndogo sana.
Hata mimi nina ndgu, jamaa na marafiki wengi tu ambao ni dini changanyikeni lakina hakuna mikwaruzano ya kidini achilia mbali mada za kuongea dini ipi ni blra.

Mtaani hizo story hamna kabisa ni huku mitandaoni tu.
 
Usione vyaelea, ujue vimeundwa.

Hii Tanzania ya amani na utulivu ambayo wewe unaiishi imetengenezwa na watu waliojitoa (Waislamu na Wakristo) hadi leo hii unahisi udini na ukabila haupo. Matatizo na kelele za kidini, hapa Tanzania zimekuwepo sana, sema busara imetumika kulifikisha taifa hapa lilipo leo. Hii nchi bila kuwepo na BALANCE OF POWER baina ya Muslims & Christians kwenye mgawanyo wa madaraka, hatutakuwa na utofauti na nchi kama Central African Republic.


Wewe unamchukia mtu asiye wa dini yako??
 
Waraka uko clear!!

Bandari zetu ni URITHI wetu hazitauzwa, kubinafsishwa Wala kugawiwa Bure Kwa wageni.
Haya uwe umeyasema pasipo kufikiria, au uwe umeyasema ukiwa hujui lolote kuhusu uchumi wa dunia ya leo hii.

TICTS amekaa pale bandarini kwa miaka 22, tunamuweka kwenye kundi lipi?.
 
Utulivu wa Rais Samia natamani uwekwe kwny Katiba Mpya kama sifa ya msingi ya Mtu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Samia ana bahati mbaya anaongoza nchi wakati huu ikiwa na vyuo vikuu vingi ikiwa na simu za mikononi zenye mawasiliano ya kisasa. Ana haki ya kuwa mpole na naamini Mzee Mwinyi licha ya kuwa umri ni mkubwa sana bado ana hekima nyingi na kila kinachosemwa anakielewa vyema.

Pia yupo mzee JK, huyu hana uzee kama wa Mwinyi hivyo anamfariji sana SSH kila wanapoongea kwenye simu.
 
IBARA ya 4(2) ya mkataba huu wa Kimangungo inasema, iwapo Tanzania inapotaka kuweka mwekezaji mwingine maeneo mengine ya bandari, inatakiwa iende Dubai kuomba ridhaa, Dubai wakikataa kutoa idhini, ndio basi. Yaani nchi huru ikaombe ridhaa Dubai? Tena kwa Mali zake? Huu ujinga ubaki CCM na Dubai.
Upuuzi mtupu umeandika mkuu elias, Mwezi wa kumi anakuja mwekezaji mwingine hapo hapo bandarini atapewa magati namba tisa mpaka kumi na mbili, pia Bagamoyo anakuja mwekezaji mwingine hivyo hakuna kitu kama hicho ulichokisema.
 
Back
Top Bottom