Askofu Gamanywa: Makonda yuko sahihi Ushoga umekatazwa kwenye Biblia, wananchi acheni kushabikia dhambi

Askofu Gamanywa: Makonda yuko sahihi Ushoga umekatazwa kwenye Biblia, wananchi acheni kushabikia dhambi

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Askofu Gamanywa ambaye ni mjumbe wa kamati ya amani na juzikati aliliombea taifa pale Ikulu katika utiaji saini mkataba wa Barrick na Serikali amesema Marekani inamuonea Makonda.

Askofu Gamanywa amesisitiza kuwa ushoga ni katazo mbele za Mungu na ni dhambi isiyosameheka.

Gamanywa amedai kuwa Makonda ni kiongozi hodari, shujaa na mwenye uthubutu na kwamba hapa Tanzania hakuna mtu mwenye ubavu wa kuikemea Marekani kama alivyofanya Makonda.

Askofu Gamanywa ameitaka Marekani ijitafakari juu ya uamuzi wake usio wa haki.

Source: Ibadani BCIC - Mbezi jogoo
 
Ki ukweli Ushoga haupendezi na zaidi ya 99% hawaukubali ushoga.Ila kwa ujumbe ule wa US hakuna mahali nimeona ushoga. Alafu nikivuta picha jinsi Raisi wa Uganda alivyoweka vikwazo juu ya ushoga basi yeye ndo angekuwa wakwanza kuguswa na hii adha.
Kushika kaa la moto huku wajitetea sio la moto anae dhuriaka ni mshikaji.
Ingependeza tujadili waliyo yataja alafu tupinge kwa hoja kuwa wamemuonea sio kuleta dhahania
 
Mpe 'twita' ya Pompeo halafu arudie hotuba, halafu atwambie na Sweeden wamesemaje ili tubaki njia kuu.
Askofu Gamanywa ni mwanahabari anayemiliki gazeti na Radio......hivyo uelewa wake siutilii shaka!
 
johnthebaptist,
Marekani siyo mbinguni! Wasijidanganye kuwa tuna hamu sana ya kwenda Marekani! Kusema ukweli hatuhitaji kwenda kwao nchi ya mashoga!!!
 
Askofu Gamanywa ambaye ni mjumbe wa kamati ya amani na juzikati aliliombea taifa pale Ikulu katika utiaji saini mkataba wa Barrick na Serikali amesema Marekani inamuonea Makonda.

Askofu Gamanywa amesisitiza kuwa ushoga ni katazo mbele za Mungu na ni dhambi isiyosameheka.

Gamanywa amedai kuwa Makonda ni kiongozi hodari, shujaa na mwenye uthubutu na kwamba hapa Tanzania hakuna mtu mwenye ubavu wa kuikemea Marekani kama alivyofanya Makonda.

Askofu Gamanywa ameitaka Marekani ijitafakari juu ya uamuzi wake usio wa haki.

Source: Ibadani BCIC - Mbezi jogoo
Mzee ungepanda ndege ukawaambie Wakubwa huko Marekani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom