Askofu Gwajima alikuwa Mwanamkakati wa Lowassa na Magufuli

Never...
Unawaona wananchi tofauti na ninavyowaona.

Naheshimu maoni yako.
 
Never...
Unawaona wananchi tofauti na ninavyowaona.

Naheshimu maoni yako.
Ninayoyaongea ni uhalisia wa binadamu. Hata wanyama kama Simba, Fisi, Tembo, Mbwa mwitu, hata nyuki wanaangalia nani anaweza kulinda maslahi yao katika mazingira yao halisi.

Ni figisu, rushwa, kutumia vyombo vya habari kumpamba mmoja na kumzuia mwingine asionekane ndiyo inaondoa level playing field. Kutumia vyombbo vya dola, kodi za wananchi kuhonga.
 
Fanya research kidogo mtaani kwako.

Angalia ni asilimia ngapi ya wananchi wanaosoma ilani za vyama, ni wangapi wanaenda kwenye mikutano ya kampeni kusikiliza Ilani za wagombea.

Wengi wanaenda kufuata mashati, kitenge, speakers tu zimesikika kijijini anaamua aende, chakula, mkumbo au pesa wamegawiwa.

Unataka ujue uhalisia wa hili tafuta watu 100 waliopiga kura mwaka 2015 au 2020 kisha uliza orodhesha Imani 10 za Chadema na za CCM.
Hao watu wakiweza kuorodhesha njoo niambie.

Tabia ya upigaji kura ya wapiga kura is dynamic [nakosa neno la kiswahili]...hasa Africa na vijijini ambako wasomi na watu wenye exposure wachache....

Mwaka 2015 tulikuwa tunapokea wapiga kura wa umri kati ya 45+ wanafanya decision ndani ya chumba cha kura.....wanakuuliza huyu naye ni nani? Unawatajia majina.

Wanakuuliza ooouh ndiyo yule aliyefanyia mkutano wake mahala fulani...... ilani ni kigezo ila sio kikuu kwa aina ya wapiga kura wetu.
 
Sababu kubwa ni figisu. Waambie wananchi ukweli huu uchaguzi ni kuhusu kuleta bomba ya maji nyumbani kwako, umeme nyumbani kwako, vituo vya afya ukiumwa, mtoto wako azaliwe salama.

Waambiwe ukweli uchaguzi ni kuhusu miundombinu, kujenga barabara kufikisha mazao yako sokoni,kupata kipato, kulinda haki yako ya msingi ya kuishi, kulinda mali zako, afya yako.

Wananchi sio wajinga unavyofikiri. They are very logical. Wanajua yupi atalinda maslahi yao. Sababu ya umaskini wao mkubwa sana uliowekwa na CCM wanarubuniwa na hivyo vitu vidogo kama vitenge, elfu kumi, t-shirt.

Kiumbe hai yoyote, Simba, binadamu, nyuki, inzi anapigania haki yake ya msingi kwanza kuishi akiwa huru, kupata chakula,haki zake, kuangalia jamii yake inalindwa hata akipigana hadi kufa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…