Mwandishi: Kusaidia kwenye hii janga, sijui ungependa kutuambiaje?
Gwajima: Kwanza hii hali ni hali ya kusikitisha sana, ni hali ya hatari, mbaya na hali ya kuhuzunisha kwelikweli na mimi hata siamini mtu anaweza kuruhusu wananchi, binadamu wakawa na hali ya maisha hii.
Kwa miaka kumi na mitano mtu ni mbunge wa jimbo hili, maeneo haya Basihaya, Chasimba, Chachui mafuriko wananchi wanaelea, kila mwaka wananchi wananunua vitu vinakwenda na maji, ni hali hatarishi kwa kwa maisha ya wanadamu.
Je yeye anaishi hapa? Je yeye anafanya kazi hapa? Wananchi wanakula wapi sasa hivi? Kwa mfano sasa hivi magodoro yameloana, vitanda vimeshaondoka.
Sasa kwa miaka 15 mbunge alafu anasema nataka tena, unataka watu wafe? Kwa hio ni jambo la kuhuzunisha, niwape pole wananchi na niombe tushirikiane tumalize tatizo hili na litamalizika.
huyu bwana kama angekuwa ni mwanafunzi wa Yesu lazima angeitwa YuDa Iskariote sio kwa utopolo huu
eti mbunge kashindwa kutengeneza miundombinu
hii hali ya kutokuelewa mambo madodo kama haya naona itakuwa imechangiwa na hali yake ya kusoma form 4 kwa miaka minane
Kweli uyu Malaya mzoefu Sasa mbona anawachungulia madada wawatu dirishani;Binafsi sizan Kama hii inaweza kumnyanyua kisiasa maana Serikal inayokusanya Kodi niyachama chake,Je kunabalozi,mwenyekiti au mtendaji Alie wahi kwenda kushtaki kuwa mbunge wetu hatengenezi miundo mbinu wakati Kodi tunampa yeye?
Gwajima bhana!!! Hizo lawama peleka TARURA na kwa Mkurugenzi,Mbunge siyo mkusanya mapato.Kazi Yale nikuwa semea bungeni na mahalii popote ila kabla hujasema vyema Ukajua unachokisema
Haya ni maeneo yapo ama below sea level au mapito ya maji kutoka milimani, hawa wote wanapigika kwa uasilia wa maeneo yenyewe, hali ya kawe beach ni mbaya sana, kwa bahati tuu ni maeneo ya mchanga. Wabunge au Rais kwa nchi zetu hizi ambazo zina scarce resources lazima wakubali kubeba lawama.