kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Ziko dawa, chanjo, na njia za matibabu ambazo zimeachwa kutumia wakati hapo mwanzo zilipitishwa na kuruhusiwa kutumiwa. Mfano, watu wameacha kutumia dawa kali kutibu minyoo, indocid, chloroquine na SP kutibu malaria, kuacha kutumia spirit kusafisha eneo la kuchoma sindano, kunyoa nywele za kinena wakati wa kwenda kwenye upasuaji, nk. Dawa, chanjo na njia za tiba zinabadilishwa na kuacha kutumiwa mara TU sayansi itakapogundua kuwa Ina madhara, haina faida au Kuna njia, dawa, chanjo mbadala nzuri zaidi ambayo inaleta matokeo bora kwenye jambo lile.
Sioni kosa la Waziri yuleyule, WHO ileile, TFDA ileile, TBS ileile, kukubali kuachana au kuongeza njia, dawa, au chanjo kwenye zile za awali. Huwezi kusema kwakuwa kuna penicillin kwa kutibu kaswende tusikubali aina nyingine za antibiotics kama erythromycin, azithromycin, ciproflaxin, etc.
Waziri Gwajima anakosa gani kutangaza dawa mpya na nzuri ya kutibu gonorhea, pumu, kisukari na covid-19 badala ya zile za zamani ? Kama kuna mtu anaemshangaa Waziri kwa hili basi mtu huyo ni ama mwehu au ana ajenda nyingine pana zaidi kuliko covid-19.
Tunapomtizama Askofu Gwajima msimtazame peke yake, watazameni pamoja na timu ya awamu ya tano iliyonyang'anywa usukani. Askofu na Polepole inawezekana wanatumika kama loud speaker TU kwenye mission fulani.