Wakuu,
Napata mkanganyiko hapa, naomba msaada nipate taarifa ya kweli kama Gwajima amesema haya maneno.
Napata mkanganyiko hapa, naomba msaada nipate taarifa ya kweli kama Gwajima amesema haya maneno.
- Tunachokijua
- Madai
Baada ya Askofu Josephat Gwajima kuzungumza na waandishi wa habari Julai 16, 2025 kumeibuka taarifa inayodai kuwa katika mazungumzo yake amaeomba msamaha na kutaka makanisa yake yafunguliwe.
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia taarifa hiyo na kugundua inapotosha.
Ufuatiliaji umebaini kuwa taarifa hiyo inapotosha kwani maneno hayo hayajatolewa na Askofu Gwajima. Katika taarifa yake aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari Askofu Gwajima alijielekeza zaidi katika kuzungumzia namna navyopinga utekaji.
Askofu Gwajima alihoji pia kwamba mambo aliyoyazungumza yalikuwa na uhusiano gani wa kufungia makanisa yake.
Askofu huyo pia alisisitiza kuwa hatokalia kimya suala la utekaji hataka kama makanisa yatafungwa kwa miaka mia, Gwajima alisema;
"Lakini mimi nataka kusema na mtu yeyote, kuhusu utekaji mimi simuogopi mtu. Siogopi asubuhi, siogopi jioni siogopi mchana. Kuhusu utekaji siogopi mtu hata kama ungefunga makanisa kwa miaka miamoja." - Askofu Josephat Gwajima
Aisha grafiki zilizotumika kubeba ujumbe huo zenye utambulisho wa vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo Jambo TV, Mwananchi na The Chanzo ni za kughushi kwani hazijatolewa na vyanzo hivyo.