SI KWELI Askofu Gwajima aomba radhi kwa viongozi wa Mamlaka zote husika na kuomba makanisa yafunguliwe

SI KWELI Askofu Gwajima aomba radhi kwa viongozi wa Mamlaka zote husika na kuomba makanisa yafunguliwe

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Wakuu,

Napata mkanganyiko hapa, naomba msaada nipate taarifa ya kweli kama Gwajima amesema haya maneno.

Gwajima Chanzo July 16, 025.jpg
Gwajima Jambo Tv July 16, 025.jpg
Gwajima Mwananchi July 16, 2025.jpg
 
Tunachokijua
Madai

Baada ya Askofu Josephat Gwajima kuzungumza na waandishi wa habari Julai 16, 2025 kumeibuka taarifa inayodai kuwa katika mazungumzo yake amaeomba msamaha na kutaka makanisa yake yafunguliwe.

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia taarifa hiyo na kugundua inapotosha.

Ufuatiliaji umebaini kuwa taarifa hiyo inapotosha kwani maneno hayo hayajatolewa na Askofu Gwajima. Katika taarifa yake aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari Askofu Gwajima alijielekeza zaidi katika kuzungumzia namna navyopinga utekaji.

Askofu Gwajima alihoji pia kwamba mambo aliyoyazungumza yalikuwa na uhusiano gani wa kufungia makanisa yake.

Askofu huyo pia alisisitiza kuwa hatokalia kimya suala la utekaji hataka kama makanisa yatafungwa kwa miaka mia, Gwajima alisema;

"Lakini mimi nataka kusema na mtu yeyote, kuhusu utekaji mimi simuogopi mtu. Siogopi asubuhi, siogopi jioni siogopi mchana. Kuhusu utekaji siogopi mtu hata kama ungefunga makanisa kwa miaka miamoja." - Askofu Josephat Gwajima

Aisha grafiki zilizotumika kubeba ujumbe huo zenye utambulisho wa vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo Jambo TV, Mwananchi na The Chanzo ni za kughushi kwani hazijatolewa na vyanzo hivyo.​
SS hatupo hivyooo wasukuma kwan wakat hilokanisa linaanzishwa miaka yotehiyooo hawakuona linavibali selikal achen kuonea watuuuu
 
Wanaukumbi:

GWAJIMA: NAWAOMBA RADHI VIONGOZI NA MAMLAKA ZOTE HUSIKA, KWA KUWA TAYARI NIMEJULISHWA NA NIMEPOKE TARIFA RASMI KUTOKA KWAO.
GWAJIMA ATUBU HADHARANI, AOMBA SERIKALI IREJEE UAMUZI WA KUFUNGA MAKANISA
taarifa hiyo inapotosha kwani maneno hayo hayajatolewa na Askofu Gwajima. Katika taarifa yake aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari Askofu Gwajima alijielekeza zaidi katika kuzungumzia namna navyopinga utekaji.

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom