Askofu Gwajima asema yeye na Abbas Tarimba ni mapacha, amkaribisha kanisani kwake na kumpigia kampeni

Askofu Gwajima asema yeye na Abbas Tarimba ni mapacha, amkaribisha kanisani kwake na kumpigia kampeni

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mchungaji wa Kanisa la ufufuo na uzima Dkt. Gwajima amesema yeye na mgombea ubunge wa jimbo la Kinondoni ni mapacha.

Gwajima amesema hayo leo alipomkaribisha Abbas Tarimba Kanisani kwake na kumtambulisha kwa waumini wake ambao walimshangilia kwa nderemo na vigelegele.

Mchungaji Gwajima amesema yeye na Abbas Tarimba wameletwa na Mungu kuwatumikia wananchi wa Tanzania.

Chanzo: Eatv

My take: Mnaosema Gwajima ana chuki na waislamu soma hiyo!

Maendeleo hayana vyama.
 
Anajikosha baada ya kututukana waislam.pole zake amechelewa. Angefanya kipindi kile tungemuelewa hivi sasa anawapigia mbuzi gita
 
Upinzani wanatetemeka!! Jimbo la kawe linabaki historia kwa mdee..alijua angekua mbunge wa kudumu kawe.

Ukizingatia kwamba Jimbo la Kawe linajumuisha maeneo Kama vile Msasani, Mikocheni, Ostebay, Makongo, Kunduchi, Wazo, Madale, Bunju, Tegeta, Boko, Mbweni, Mbezi Beach, Ununio na Mabwepande.

Ni sehemu za kishua sana kwa Dar na kuwashawishi hawa wapiga kura unahitaji kuwa smart sana.

Ukiangalia Mdee na Gwajima wapo smart kichwani haswa ukirejea hotuba zao na namna ya kujenga hoja.

Kashfa za Gwajima na uropokaji wake ndiyo kikwazo kwake.

Sasa inategemea na uwezo wake wa kuzifukia hizi kashfa na kusonga mbele kitu ambacho Ni kazi ngumu ikizingatiwa na muda Ni mchache.

Ila kimsingi mechi ya Kawe Ni ngumu
 
Utapeli kwa mgongo wa dini!

Kutumia nyumba za badala kufanya kampeni,ni kujimaliza kisiasa.

Huyu kura za Waislaumu hapati kabisa na hata za wakristo wa madhehubu mengine pia hatozipata kwani hawamuamini.
Tehe tehe,Kura Ni Siri ...uzuri wetu ccm huwa tunakwenda moja kwa moja kwenye jembe na nyundo kwanza.Tupo 6 million Kati ya wapiga 12 million
 
Watu wanaangalia utendaji..kama kashfa ingekuwa kigezo cha kutokubalika basi kanisa la gwajima leo hii lingekuwa na waumini wasiopungua hamsini.

Hiyo habari ya kashfa zinaenda zaidi mitandaoni na si kila mtu yupo bize na mitandao..kama ni kashfa hata halima ana kashfa za muda mrefu tu za kusagana. Na hata bungeni alishawahi kutuhumiwa na wabunge wenzie na bawacha wanajua hiyo skendo..
 
Back
Top Bottom