Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima atangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Kawe

Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima atangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Kawe

Askofu Josephat Gwajima ametangaza nia ya kugombea ubunge Jimbo la Kawe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na leo amefika kwenye ofisi za chama hicho kupewa utaratibu.

Kuhusu kuunga mkono UKAWA mwaka 2015, amesema hajawahi kuwa Mwanachama wa CHADEMA, ila hutetea haki wakati wote.

===
Aliingia Ofisi ya CCM Wilaya ya Kinondoni

Amesema alikwenda pale baada ya kumsikia Rais na Katibu mkuu wa CCM aliyetangaza kuwa wale wenye nia ya kumsaidi Rais achukue fomu, na yeye ameona aweze kwenda ofisini kujua utaratibu wa kugombea

Amesema inaweza kuwa mtu mchungaji haimzuii kuwa mbunge kwa kuwa wako viongozi wa dini ambao pia ni viongozi kisiasa, amesema hajawahi kuwa mwananchama wa chadema

Amesema amekuwa mwanachama wa CCM tangu mwaka 1994, aliipata katika mkoa wa Mwanza, Wilaya ya Misungwi, kata ya Buhingo kijiji cha Kabale na alipewa kadi na mzee Kasmiriki Futumo, alikuwa ni mwenyekiti wa ccm ambaye katibu wake alikuwa Leoneidas Masungwa

Kadi yake amesha-upgrade kuingia mfumo mpya, amesisitiza hajawahi kuwa mwanachama wa CHADEMA, ila anapenda kutetea haki na tatatetea haki siku zote. Amesema anatetea haki sehemu yoyote, iwe CCM au kokote pale atatetea haki

Hajasema kitu ambacho anaweza kwenda kuwafanyia watu wa Kawe. Aidha ilionekana kuwa angeweza kugombea Misungwi, lakini amesema Misungwi ni sehemu aliyozaliwa lakini maisha yake yamekuwa Kawe kwa hiyo atagombea Kawe

View attachment 1495050

Yaani anapicha mpaka chafu mitandaoni eti Askofu!!!
 
Hafai ubunge, uaskofu ndio kabisa kabisa, hafai kitu mwacheni aende zake.
 
Gwajima ndo atapeleka hoja ya Rais aongezewe muda. Huko Russia wananchi wamepiga kura kumuongezea Putin muda mpaka 2036.

Wananchi wa China na Russia wameishamaliza kazi yao wamewaongezea muda viongozi makini wa nchi hizo.

Dunia kwa sasa haihitaji maraisi mafisadi na wanaochekacheka.

Yajayo yanafikrisha sana.
 
Gwajima 2017

"Mimi siwezi kuwa Mbunge ni kujishusha mimi ni mtumishi wa bwana ambaye ni zaidi ya Mbunge,Waziri na Rais"

Gwajima 2020
"Naishi kawe naona kuna naweza kuifanyia kitu kawe kupitia CCM,hivyo nina gombea Ubunge"

Gwajima 2010

"Mnashinda facebook,kwa taarifa yenu facebook ni mtandao wa kishetani,Shetani anakusanya mafairi yake"

Gwajima 2020

"Ukiwa mbali na kanisa unaweza ingia facebook kwenye live stream kuendelea na mahubiri na kutuma sadaka yako kupitia M-Pesa"

Wana kawe kueni makini na huyu mtu.
Sasa hapo sijaona point jamaa angu
 
Joseph Gwajima leo amefika ofisi za ccm ili kupewa utaratibu wa jinsi ya kugombea ubunge.

Amedai kuwa anataka kugombea ubunge jimbo la kawe kupitia chama cha mapinduzi na amekana kuwa hajawahi kuwa mwanachama wa cdm.

Tujiandae kumuongezea cheo kwenye jina lake na sasa tutamuita MHESHIMIWA MCHUNGAJI GWAJIMA. View attachment 1494735
sura yake tu ya wizi
 
Ha ha ha ha mshenga.

Wale aliowakutanisha waoane wanasemaje?
 
Gwajima 2017

"Mimi siwezi kuwa Mbunge ni kujishusha mimi ni mtumishi wa bwana ambaye ni zaidi ya Mbunge,Waziri na Rais"

Gwajima 2020
"Naishi kawe naona kuna naweza kuifanyia kitu kawe kupitia CCM,hivyo nina gombea Ubunge"

Gwajima 2010

"Mnashinda facebook,kwa taarifa yenu facebook ni mtandao wa kishetani,Shetani anakusanya mafairi yake"

Gwajima 2020

"Ukiwa mbali na kanisa unaweza ingia facebook kwenye live stream kuendelea na mahubiri na kutuma sadaka yako kupitia M-Pesa"

Wana kawe kueni makini na huyu mtu.
Huyu jamaa ni hopeless pastaor

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Gwajima 2017

"Mimi siwezi kuwa Mbunge ni kujishusha mimi ni mtumishi wa bwana ambaye ni zaidi ya Mbunge,Waziri na Rais"

Gwajima 2020
"Naishi kawe naona kuna naweza kuifanyia kitu kawe kupitia CCM,hivyo nina gombea Ubunge"

Gwajima 2010

"Mnashinda facebook,kwa taarifa yenu facebook ni mtandao wa kishetani,Shetani anakusanya mafairi yake"

Gwajima 2020

"Ukiwa mbali na kanisa unaweza ingia facebook kwenye live stream kuendelea na mahubiri na kutuma sadaka yako kupitia M-Pesa"

Wana kawe kueni makini na huyu mtu.
Best reference. Ngoja kampeni zianze tumsambaratishe.
 
Unawajua waumini wa Gwajima lakini.... ni zile typ za ulipo tupo!

Hukuona walivyokua wanamtetea kipindi cha ile video?

Yaani Gwajima Akiwaambia vaa kijani wote watavaa!
Akiwaambia vaaa kaki wote watavaa!

Yani sijui kawalisha nini Aisee!

Ni kweli wahumini wake ni watiifu kwake, lakini kwa idadi yao hata wakimpigia kura wote, hizo kura haziwezi kumpitisha.
Jambo lingine kuwa mbuge kunategemeana na kukubalika kwa watu wa dini tofauti, sasa yeye kama atategemea waumini wake, basi hatafanikiwa kwani watu wa imani nyingine watampinga.
 
.
FB_IMG_1593757859428.jpg
 
Back
Top Bottom