Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima atangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Kawe

Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima atangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Kawe

Kama heading inavyoeleza wengi wanaopinga hapa JamiiForums wanasukumwa na udini na chuki binafsi 'iliyopitiliza'. (1) Hakuna mwanadamu aliyemkamilifu, awe ni CCM, CHADEMA, CUF, NCCR, Mwarabu, Mhindi, na nk., (2) hata sasa kuna wabunge ni ma-alhaj, mashehe, wachungaji na wapendwa. Ova!
 
Kama heading inavyoeleza wengi wanaopinga hapa JamiiForums wanasukumwa na udini na chuki binafsi 'iliyopitiliza'. (1) Hakuna mwanadamu aliyemkamilifu, awe ni CCM, CHADEMA, CUF, NCCR, Mwarabu, Mhindi, na nk., (2) hata sasa kuna wabunge ni ma-alhaj, mashehe, wachungaji na wapendwa. Ova!
Ishu ya huyo ni maadili, anacheza picha za ngono na kubanjuka na waumini wake tena wake za watu
 
Upo sahihi kusema Halima hatatoboa,ni haki yako.

Na mimi nipo hapa kusema Gwajima ni mavi na hatatoboa,ni haki yangu..

Uzuri baada ya uchaguzi tuje hapa tu-verify.

Haina shida Mkuu!
Sawa mkuu tunza maneno yako na mm nitunze yangu October sio mbali tuombe uzima
 
Nasikia Hata makonda kashachukua kisiri siri jimbo la ubungo
 

Askofu Josephat Gwajima ametangaza nia ya kugombea ubunge Jimbo la Kawe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na leo amefika kwenye ofisi za chama hicho kupewa utaratibu.

Kuhusu kuunga mkono UKAWA mwaka 2015, amesema hajawahi kuwa Mwanachama wa CHADEMA, ila hutetea haki wakati wote.

===
Aliingia Ofisi ya CCM Wilaya ya Kinondoni

Amesema alikwenda pale baada ya kumsikia Rais na Katibu mkuu wa CCM aliyetangaza kuwa wale wenye nia ya kumsaidi Rais achukue fomu, na yeye ameona aweze kwenda ofisini kujua utaratibu wa kugombea

Amesema inaweza kuwa mtu mchungaji haimzuii kuwa mbunge kwa kuwa wako viongozi wa dini ambao pia ni viongozi kisiasa, amesema hajawahi kuwa mwananchama wa chadema

Amesema amekuwa mwanachama wa CCM tangu mwaka 1994, aliipata katika mkoa wa Mwanza, Wilaya ya Misungwi, kata ya Buhingo kijiji cha Kabale na alipewa kadi na mzee Kasmiriki Futumo, alikuwa ni mwenyekiti wa ccm ambaye katibu wake alikuwa Leoneidas Masungwa

Kadi yake amesha-upgrade kuingia mfumo mpya, amesisitiza hajawahi kuwa mwanachama wa CHADEMA, ila anapenda kutetea haki na tatatetea haki siku zote. Amesema anatetea haki sehemu yoyote, iwe CCM au kokote pale atatetea haki

Hajasema kitu ambacho anaweza kwenda kuwafanyia watu wa Kawe. Aidha ilionekana kuwa angeweza kugombea Misungwi, lakini amesema Misungwi ni sehemu aliyozaliwa lakini maisha yake yamekuwa Kawe kwa hiyo atagombea Kawe

View attachment 1495050
Nchi ina vituko hii
Huyu naye anawaza kudhalilishwa au katumwa!
 
Gwajima 2017

"Mimi siwezi kuwa Mbunge ni kujishusha mimi ni mtumishi wa bwana ambaye ni zaidi ya Mbunge,Waziri na Rais"

Gwajima 2020
"Naishi kawe naona kuna naweza kuifanyia kitu kawe kupitia CCM,hivyo nina gombea Ubunge"

Gwajima 2010

"Mnashinda facebook,kwa taarifa yenu facebook ni mtandao wa kishetani,Shetani anakusanya mafairi yake"

Gwajima 2020

"Ukiwa mbali na kanisa unaweza ingia facebook kwenye live stream kuendelea na mahubiri na kutuma sadaka yako kupitia M-Pesa"

Wana kawe kueni makini na huyu mtu.
 
Back
Top Bottom