Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tatizo wakienda CCM ni rahisi sana kuchafuka maana walioko huko wengi ni wachafu na mambo yao ni machafu tu!!!Ni jambo jema sana kuongozwa na watumishi wa Mungu wakiwa ndani ya chama kubwa CCM,
Kila la kheli baba askofu
Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
Hizo point zake unafikiri zinatakiwa kwenye siasa! Pale alipo kama mchungaji yeye ndiye kiongozi na hakuna wa kumpinga, akisema wote wanaitikia Amen. Kwenye siasa kwanza atakuwa chini ya chama cha siasa ambacho kina uongozi; ni lazima sasa yeye ndiye aseme Amen vinginevyo.Katika watu niliokuwa natamani siku moja aingie bungeni ni Gwajima.
Anakuaga na point sana za maswala mbalimbali yahusuyo nchi coz ana exposure kubwa ya nje.
Harmo, Liquid, MwnFA.Sasa 'comedy squad' inaenda kukamilika bungeni, yaani, 'just imagine', Musukuma, Kibajaji ...... na sasa GWAJIMA! 😅
NI SHIDAAA! 😅
👊 ✌✌✌💥
Alima mdee hawez kusimama na gwajima huu ndio ukwel gwajima anaongea Sana
Amemrahisishia Halima Mdee kazi asante sana.View attachment 1494766
Askofu Josephat Gwajima ametangaza nia ya kugombea ubunge Jimbo la Kawe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na leo amefika kwenye ofisi za chama hicho kupewa utaratibu.
Kuhusu kuunga mkono UKAWA mwaka 2015, amesema hajawahi kuwa mwanachama wa CHADEMA, ila hutetea haki wakati wote.
===
Aliingia Ofisi ya CCM Wilaya ya Kinondoni
Amesema alikwenda pale baada ya kumsikia Rais na Katibu mkuu wa CCM aliyetangaza kuwa wale wenye nia ya kumsaidi rais achukue fomu, na yeye ameona awezekwenda ofisini kujua utaratibu wa kugombea
Amesema inaweza kuwa mtu mchungaji haimzuii kuwa mbunge kwa kuwa wako viongozi wa dini ambao pia ni viongozi kisiasa, amesema hajawahi kuwa mwananchama wa chadema
Amesema amekuwa mwanachama wa CCM tangu mwaka 1994, aliipata katika mkoa wa Mwanza, Wilaya ya Misungwi, kata ya Buhingo kijiji cha Kabale na alipewa kadi na mzee Kasmiriki Futumo, alikuwa ni mwenyekiti wa ccm ambaye katibu wake alikuwa Leoneidas Masungwa
Kadi yake amesha-upgrade kuingia mfumo mpya, amesisitiza hajawahi kuwa mwanachama wa CHADEMA, ila anapenda kutetea haki na tatatetea haki siku zote. Amesema anatetea haki sehemu yoyote, iwe ccm au kokote pale atatetea haki
Hajasema kitu ambacho anaweza kwenda kuwafanyia watu wa Kawe. Aidha ilionekana kuwa angeweza kugombea Misungwi, lakini amesema Misungwi ni sehemu aliyozaliwa lakini maisha yake yamekuwa Kawe kwa hiyo atagombea Kawe
View attachment 1495050