PreGE2025 Askofu Gwajima: Ikatokea Abdul mtoto wa Mama Samia amechukuliwa kesho kaokotwa hana macho utajisikiaje?

PreGE2025 Askofu Gwajima: Ikatokea Abdul mtoto wa Mama Samia amechukuliwa kesho kaokotwa hana macho utajisikiaje?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Anahoji Askofu Gwajima.!

Je, Abdul anaweza kupotezwa na kuokotwa hana macho? Je mtoto wa Majaliwa au wa IGP Wambura, au wa Askofu Gwajima wanaweza kupotezwa na kuokotwa hawana macho na Taifa likakaa kimya? Kama haiwezekani kwa hao, kwanini watoto wa wengine wanapotezwa halafu tunakaa kimya kana kwamba wamepotea mbuzi au kondoo?

Kitendo Cha kukaa kimya siyo hekima wakati mwingine unafiki unasaidia!!keep quiet may mean Yes!! Hii ni hatari
 
Anahoji Askofu Gwajima.!

Je, Abdul anaweza kupotezwa na kuokotwa hana macho? Je mtoto wa Majaliwa au wa IGP Wambura, au wa Askofu Gwajima wanaweza kupotezwa na kuokotwa hawana macho na Taifa likakaa kimya? Kama haiwezekani kwa hao, kwanini watoto wa wengine wanapotezwa halafu tunakaa kimya kana kwamba wamepotea mbuzi au kondoo?

Gwaji ni Tai, kachoka na yanayoendelea nchini kaona liwalo na liwe.
 
Anahoji Askofu Gwajima.!

Je, Abdul anaweza kupotezwa na kuokotwa hana macho? Je mtoto wa Majaliwa au wa IGP Wambura, au wa Askofu Gwajima wanaweza kupotezwa na kuokotwa hawana macho na Taifa likakaa kimya? Kama haiwezekani kwa hao, kwanini watoto wa wengine wanapotezwa halafu tunakaa kimya kana kwamba wamepotea mbuzi au kondoo?

Gwajima ni msema kweli.
Mungu ambariki

Ni hatari sana kufumbia macho uovu.. Mungu mbinguni atatudai.
Lazima kanisa lisimame katika zamu yake kwa kukemea uovu na kuhubiri haki maana haki huinua taifa.
 
Anahoji Askofu Gwajima.!

Je, Abdul anaweza kupotezwa na kuokotwa hana macho? Je mtoto wa Majaliwa au wa IGP Wambura, au wa Askofu Gwajima wanaweza kupotezwa na kuokotwa hawana macho na Taifa likakaa kimya? Kama haiwezekani kwa hao, kwanini watoto wa wengine wanapotezwa halafu tunakaa kimya kana kwamba wamepotea mbuzi au kondoo?

Kuna mambo ameongea kwa mifano ila ndivyo yalivyo,hususani kutenguliwa kisa kupinga uuzwaji wa port.
 
Better late than never
Ni VIZURI ameongea,but why imemchukua muda kutoka na kusema muda huu?inakosa nguvu it sounds like he's calculating on how to play his last cards towards October election,utekaji upo since mwenda zake kinachofanyika ni muendelezo tuh wa wale wasiojulikana...asijiafanye kurusha jiwe gizani,kwa sisi wafia dini tunachokiona hapo ni Islamophobia tuh
 
Inawezekana kweli huyu ni mtumishi wa Mungu. Ukiwa mtumishi wa Mungu kwa haya yanayoendelea Tanzania, huwezi kukaa kimya.

Huwa najiuliza sana, wenye mamlaka wanajisikiaje wanajiita viongozi halafu watu wao wanatekwa na kupotea na hamna lolote wanalofanya?

Kwa maswali haya ya Askofu, naona mashetani lazima wamuundie kamati ya kumfurusha ndani ya chama.

Kama uongozi umewashinda sio vibaya kupisha wengine. Huwezi kuwa baba halafu ndani kuna chatu anameza watoto na wewe baba upo tu umetulia.
​
 
Kinachotisha n siku upande wa pili wakianza kulipa kisasi kwa wanaowadhani wanawatenda leo..nchi Itaangamia
 
Anahoji Askofu Gwajima.!

Je, Abdul anaweza kupotezwa na kuokotwa hana macho? Je mtoto wa Majaliwa au wa IGP Wambura, au wa Askofu Gwajima wanaweza kupotezwa na kuokotwa hawana macho na Taifa likakaa kimya? Kama haiwezekani kwa hao, kwanini watoto wa wengine wanapotezwa halafu tunakaa kimya kana kwamba wamepotea mbuzi au kondoo?

Kwa Tanzania ili uaminike hii script angetakiwa isemwe na mtu mwingine lakini si aliye katika system. Mpaka a nafika hapo kwenye press hiyo script is hapatikani na kuhakikiwa. Facial expression haioneshi msisitizo kwa anachokiongea, gestures haziendani na uzito wa jambo.
Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini anachokiongea kuwa ni kuumizwa na kukerwa na haya yanayotokea. Angekuwa kinyume na mfumo asinge fanya press hiyo peupe hivyo.

Another political strategic plan. Tunasukuma kete, tunasubiri kete za wananchi.
 
Gwaji boy, kumuelewa uwe na D 2. Kaongea kiutu uzima sana, kachengesha ili mtoa mipasho, asione kamshutumu direct. Kwenye mifano mule ndiko kwenye ukweli wenyewe.

Majibu ya tengua, teua za Mkuu wa Idara x, huenda walikataa haya. Kuna watu wana hofu ya Mungu na wanajua damu, huwa zinarudi kudai haki. Wakawa labda wanashauri vingine, wanajikuta out.

Kuhusu mifano ya watoto, amewatolea wahusika wakuu, ili waone je ingekuwa wao? Uchungu wake ungekuaje? Wajiweke nafasi ya Mama/ Baba yake Mdude n.k, je wangeona ni sawa na kawaida?

Kingine, nilichopenda amesema hawa wanaotekwa na kuuwawa, ni binadamu siyo mbuzi. Hapa nampongeza sana. Watu tunaona ni wao na si sisi. Ila hujui nani anayefata baada ya hao. Hakuna aliye salama.
 
Back
Top Bottom