PreGE2025 Askofu Gwajima: Ikatokea Abdul mtoto wa Mama Samia amechukuliwa kesho kaokotwa hana macho utajisikiaje?

PreGE2025 Askofu Gwajima: Ikatokea Abdul mtoto wa Mama Samia amechukuliwa kesho kaokotwa hana macho utajisikiaje?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Inawezekana kweli huyu ni mtumishi wa Mungu. Ukiwa mtumishi wa Mungu kwa haya yanayoendelea Tanzania, huwezi kukaa kimya.

Huwa najiuliza sana, wenye mamlaka wanajisikiaje wanajiita viongozi halafu watu wao wanatekwa na kupotea na hamna lolote wanalofanya?

Kwa maswali haya ya Askofu, naona mashetani lazima wamuundie kamati ya kumfurusha ndani ya chama.

Kama uongozi umewashinda sio vibaya kupisha wengine. Huwezi kuwa baba halafu ndani kuna chatu anameza watoto na wewe baba upo tu umetulia.
​
Mtu aliyeapa kuilinda na kuitetea katiba anasema ni kijitabu tu maana yake hakina maana, tutegemee nini hapo?
 
Anahoji Askofu Gwajima.!

Je, Abdul anaweza kupotezwa na kuokotwa hana macho? Je mtoto wa Majaliwa au wa IGP Wambura, au wa Askofu Gwajima wanaweza kupotezwa na kuokotwa hawana macho na Taifa likakaa kimya? Kama haiwezekani kwa hao, kwanini watoto wa wengine wanapotezwa halafu tunakaa kimya kana kwamba wamepotea mbuzi au kondoo?

Wakipotea ICC watakosa uhondo
 
Chura kiziwi anapigwa spana kushoto kulia juu chini mashariki magaharibi 😆😆😆😂 ni bora amuachie Lissu halafu Reforms kwenye mfumo wa uchaguzi ili atawale raha mustarehe.
Problem isthat she isn't the one to decide.
Watu wa mfumo na maccm yanataka ushindi kwa ghatama yoyote to keep their extravagant lifestyles going.
She is in a gigantic dilemma.
 
Problem isthat she isn't the one to decide.
Watu wa mfumo na maccm yanataka ushindi kwa ghatama yoyote to keep their extravagant lifestyles going.
She is in a gigantic dilemma.
Na yeye mwenyewe tu mbona Jiwe hakupelekeshwa bali yeye ndiye alupelekesha mhimili wa uraisi.
 
Japo humo humo na kujipakulia minyama, asisahau aliahidi wananchi wa kawe atawapeleka mbele huko.....,
We unaonaje,tuzungumzie suala ka watu kutekwa na kupotezwa tena wengine wakiuawa ba kutobolewa macho au tuongelee hilo la kwenda HUKO na wakipelekwa huko,wakirudi waje watekwe,sindiyo?
Nakuonea huruma hiyo hoja ungeiwasilisha mbele ya ndugu wa mzee Kibao,Tundu Lissu,Soka na wengine.Pole sana.
 
Mwamba ameamua kuuliza maswali lakini na majibu anayo mwenyewe.

Ametumia akili nyingi sanaa
 
Huyu tapeli kama tapeli soon mtasikia ameomba radhi
 
Anahoji Askofu Gwajima.!

Je, Abdul anaweza kupotezwa na kuokotwa hana macho? Je mtoto wa Majaliwa au wa IGP Wambura, au wa Askofu Gwajima wanaweza kupotezwa na kuokotwa hawana macho na Taifa likakaa kimya? Kama haiwezekani kwa hao, kwanini watoto wa wengine wanapotezwa halafu tunakaa kimya kana kwamba wamepotea mbuzi au kondoo?

Hizi hoja ingependeza Gwajima angeziongelea Bungeni ingekuwa vizuri sana
 
Taifa likakaa kimya? Kama haiwezekani kwa hao, kwanini watoto wa wengine wanapotezwa halafu tunakaa kimya kana kwamba wamepotea mbuzi au kondoo?
A very profound statement.

Mchengerwa yeye anasema "Yupo tayari kutoa maisha yake kuilinda AMANI iliyopo Tanzania sasa hivi".

Maana yake ni kwamba, kwa kuwa yeye binafsi hajaguswa, AMANI ndani ya nchi hii imetamalaki.

Hao wanaopotezwa na kutobolewa macho kwake yeye haimhusu kabisa.
 
Hizi hoja ingependeza Gwajima angeziongelea Bungeni ingekuwa vizuri sana
Ataziongeleaje Bungeni, wewe hujui vibano vya huko Bungeni, au hujawahi kufuatilia maswala ya Bunge ndani ya nchi hii?
 
Hapo Prof Gwajima anamuuliiza Mama sio mimi maana mwenye mtoto ni mama sema wasizwa wameshindwa kuelewa alivyoongea...
 
Kipimo cha kwamba una akili timamu ni huruma.
Inasikitisha sana ndugu zetu kuuawa na kutekwa kwa wingi namna hii.
Ee Mungu fanya kitu sasa.
CCM na vyama vingine ni takataka tu mbele ya maslahi ya taifa.
Taifa letu nakupenda sana.
Ungependa nchi yako usinge jipachika jina la hovyo namna hiyo!
 
Back
Top Bottom