Askofu Gwajima: Kuna mtu ameleta barua Kanisani jioni hii, sikuiona amesema atarudi kesho

Sasa kama hakuwa amepokea barua yoyote kwa nini akanushe kuwa hiyo iliyopo mtandaoni si ya kweli?

Huyu naye ana mapungufu makubwa kwenye public speaking.

Gazeti la The Citizen bado linaripoti kuwa kanisa lake limefungiwa, kwa mujibu wa hiyo barua.
Kama hajapelekewa barua bado taarifa hiyo itabaki kuwa si ya kweli
 
Eti yuko na maAskofu,maaskofu wa wapi hao wakati walikuwa wabeba mkaa hapo soko la Tandale. Biblia hawaijuii, ujanja ujanja tu wa kuiba hela za waumini
Kuna tapeli kama Mwamposa??
 
Enzi hizo za Matukio ya kibiti hatukuwahi kuona misikiti ikigungiwa. Kufungia kanisa ni tusi kwa Ukristo na ni kufuru kwa Mungu. Hakuna binadamu mwenye mamlaka ya kufungia kanisa.
 
Tumetokea kwenye mkondo mkali, kwa sasa unakwenda kupoa polepole!
 
Sasa kama hakuwa amepokea barua yoyote kwa nini akanushe kuwa hiyo iliyopo mtandaoni si ya kweli?

Huyu naye ana mapungufu makubwa kwenye public speaking.

Gazeti la The Citizen bado linaripoti kuwa kanisa lake limefungiwa, kwa mujibu wa hiyo barua.
Swali muhimu ni kwamba, hiyo barua inafikaje mitandaoni kabla ya kumfikia mlengwa?
 
Mkuu hiyo barua ina muhuri ina saini ya mtoa barua?
 
Kwani Askofu unataka atoke wapi? Awe meneja wa TRA au Bandari? Kwamba wabeba mkaa hawawezi kuwa Maaskofu!? Akili finyu mno
Wakati Askofu wa kwanza ambaye ni mtume Petro alikuwa ni mvuvi tu
 
Dunian hamn vita Kali kama ya dini, kwa hili watawal wataumbuka mchana kweupe Tupo hapa
 
Sasa kama hakuwa amepokea barua yoyote kwa nini akanushe kuwa hiyo iliyopo mtandaoni si ya kweli?

Huyu naye ana mapungufu makubwa kwenye public speaking.

Gazeti la The Citizen bado linaripoti kuwa kanisa lake limefungiwa, kwa mujibu wa hiyo barua.
Hiyo barua ina muhuri na saini?
 
Kwani Askofu Gwajima kaanza leo kuhubiri mahubiri yenye mlengo wa kisiasa? Kwanibutekaji ni siasa?
 
Vipi kama haijamfikia tu lakini ipo njiani?

Kusema hiyo barua ni ya uongo maana yake ni kwamba haijaandikwa na huyo ambaye jina lake lipo kama mwandishi.

Gwajima angeweza tu kusema kuwa yeye hajapokea taarifa zozote kuhusu kufungiwa.
Ikiwa ipo njiani maana yake haijakufikia.

Ili uwe reasonable katika kutoa majibu yasiyo pinga uvumi unaosambaa mitandaoni ni lazma uwe walau na taarifa ya ujio wa barua kutoka kwenye hiyo mamlaka ili uwe katika nafasi nzuri ya kusema huwenda kuwa ipo njiani.

Sasa wewe huna taarifa, unasikia tu watu wanaongea, utaachaje kupinga?

Halafu

Saini zinagushiwa tu wala sio kitu cha kufanya mtu akubali uvumi wa mtandaoni.

Katika ule waraka wa G55 kuna baadhi ya wajumbe walioinga kuitambua nyaraka ile hali ya kuwa saini zao zipo kwenye documents.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…