Askofu Gwajima: Madikteta wote walishinda uchaguzi wa kidemokrasia lakini hawakuwa na maono

Askofu Gwajima: Madikteta wote walishinda uchaguzi wa kidemokrasia lakini hawakuwa na maono

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Kauli za Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima, Bungeni leo Juni 21, 2022

"Inapotokea utawala mmoja unamaliza na kuingia utawala mwingine, na kwa sababu mtazamo wa utawala uliopita ni tofauti na unaokuja, inabidi viongozi wengi sana wabadilike kwa sababu inaonekana kwamba maono mapya yanaingia.

“Tungekuwa na maoni yaleyake uongozi ungekuwa unabadili staili tu ya uongozi lakini maono ni yakeyake

"Madikteta wote walishinda uchaguzi wa kidemokrasia kuanzia Bokassa hadi Hitler, isipokuwa walikuwa hawana maono ya wananchi ambayo wamejipangia, wakatoka nje na nchi zao zikaharibiwa.

“Zawadi kubwa tunayotakiwa kuipa Nchi hii ni maono ya muda mrefu, tunatakiwa kuiona Dunia ijayo kwa mbali sana ili kama nchi tujipange katika mitaala yetu ya elimu ili watoto wetu waweze kuendana na mahitaji ya dunia ijayo.

"Kujenga Taifa ni sawa na kujenga nyumba, hauwezi kujenga nyumba bila ramani, unaweza ukajenga nyumba bila ramani lakini mwishoni utakuja kupata changamoto kwamba pale palipofaa kukaa dirisha, hakuna tena dirisha hukuweka.

“Ilani za uchaguzi ziwe zinaongelea maono ya nchi, mitaala ya elimu vilevile, mipango ya muda mfupi tuliyonayo ni mizuri lakini haiwezi kujenga nchi imara.

“Mfano ni Mtwara ilipoibuka miradi ya gesi zikajengwa hoteli, lakini leo hoteli hizo hazina watu kwa kuwa maono yamebadilika.

"Tunapojenga Taifa tunapaswa kuwa na maono ya muda mrefu, mwanzoni nilipochangia kuhusu maono nilionekana kama sioni maono, lakini nazungumzia maono ya muda mrefu ya miaka 50, 60 au 100 ya Tanzania ijayo.

"Kiongozi anapaswa kuona mbali zaidi ya wengine, kuona sana zaidi ya wengine na anapaswa kuona kabla ya wengine, na katika maono anapaswa kuwa na maono ya mbali ili nchi yetu iweze kujengwa kutokea mbali.

"Nitoe mfano wa maono ya muda mrefu, ndani ya miaka 50 ijayo kila barabara ziwe za lami, kila nyumba iwe na huduma ya maji safi na salama, kila Wilaya iwe na Hospitali ya Wilaya na chuo kikuu cha serikali, hiki ndio kinachoitwa maono ya muda mrefu ya nchi.”
 
Lazima tuwe na maono, i share view zake, na mimi ni mmoja wa wafuasi wakubwa wa kuwa na sera za nchi badala ya party manifestos. Sera za nchi zitumike kupima vyama ni kwa namna gani watazitekeleza.

Hii italeta continuity na kuondoa mambo ya kishamba kama ya kujenga kiwanja cha ndege Chato ambacho hakina tija na kazi yoyote zaidi ya kuanikia mpunga au kuacha kutekeleza miradi ya maendeleo kwa sababu za wivu kama kile chuo kikuu cha Aga Khan kilichotaka kujengwa Arusha.
 
Kauli za Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima, Bungeni leo Juni 21, 2022

"Inapotokea utawala mmoja unamaliza na kuingia utawala mwingine, na kwa sababu mtazamo wa utawala uliopita ni tofauti na unaokuja, inabidi viongozi wengi sana wabadilike kwa sababu inaonekana kwamba maono mapya yanaingia...
Anachoongea gwaji boy ni very important kwa nchi kama yetu ila kwa sababu tumezoea kufanya mambo kwa mazoea na mapuuza hatutatilia maanani hoja yake ..ingawa wenye akili na upeo tunamuelewa Nini hasa Anamaanisha .
 
Nilimkubali sana JPM kwa kuwa alikuwa na maono hayo aliyoyataja Gwajima. Na alikiuwa na sifa moja kuu ya kuona mbali kabla ya wengine. Miradi yote mikubwa aliyoinzisha ni kwa sababu ya Tanzania ya kesho, huyu mwamba kwa kweli hapo nilimkubali sana.
 
Nilimkubali sana JPM kwa kuwa alikuwa na maono hayo aliyoyataja Gwajima. Na alikiuwa na sifa moja kuu ya kuona mbali kabla ya wengine. Miradi yote mikubwa aliyoinzisha ni kwa sababu ya Tanzania ya kesho, huyu mwamba kwa kweli hapo nilimkubali sana.
Kujenga uwanja Chato ni maono ya kesho au uharibifu wa pesa za nchi?
 
Back
Top Bottom