Askofu Gwajima na Jerry Silaa waitwa kwenye Kamati ya Bunge kujieleza kwa kusema uongo na kushusha hadhi ya Bunge

Hao wabunge wote wanaonewa tu.

Chanjo ni hiyari na hii chanjo ni usanii tu haina maana yoyote.

Wabunge hawalipi kodi. Kiasi wanacholipia Kodi ni kidogo sana ila kikubwa zaidi ya 80% hakikatwi kodi.

Hii nchi haiwezi kupata maendeleo chini ya ccm.
 
Mwambieni tu awafukuze Ubunge ndo ndo atajua kilichokunja mkia wa mbwa.
Yeye mwenyewe Kongwa alibebwa na JPM,leo kaanza mdomo ili tu kulinda kibarua chake.
unakipi cha kumfanya ndugai wewe
 
Kwahiyo wewe umejigeuza mtetezi wa wapinga chanjo, na wasumbua wenye hiari ya chanjo sio, wao kukataa chanjo nu hiari yao ila sii kuwazuia wenye hiari au kuwapotosha wengine.
 
Inapotokea wameitwa km hv huwa wanapewa nauli na pesa ya kujikimu km wanavyofanyiwaga ktk vikao vya kawaida???
 
Kwahiyo wewe umejigeuza mtetezi wa wapinga chanjo, na wasumbua wenye hiari ya chanjo sio, wao kukataa chanjo nu hiari yao ila sii kuwazuia wenye hiari au kuwapotosha wengine.
Kama nyie mnapigia kampen watu wachome...acha uf...a
 
Hii kamati ndio ndugu Pasco Mayalla aliwahi kuitwa nadhani, akabadilika sana toka aende huko
Alitishiwa kupotezwa, akawa mdogo kama piriton! Tangu siku alivyorudi akaenda Lumumba kukabidhi akili kwa Polepole yeye akabaki anatembea na kopo tu!
 
Yawezekana walisema uongo walipokuwa ndani ya Bunge.
 
Kosa alilolifanya Gwajima ni kuamua kutumikia Mabwana wawili , Mbaya zaidi anaenda Kwa bwana huyu na masharti na taratibu za Bwana mwingine kitu ambacho hakipo. Akubali amekengeuka ama sivyo ataaibishwa mchana kweupe
Mungu hadhihakiwi
Yeye alishasema hawezi kuwa Mbunge wala Rais Hivyo ni kujishusha hadhi.
 
Jerry kusema wabunge watoe tozo kwenye mishahara yao imekuwa nongwa, khaaa! Na kila baada ya miaka 5 wanafunga mikataba ya ajira zao za ubunge wanapewa marupuru yao yote haijalishi mbunge ataendelea kwa vipindi vingapi? Tena hiyo hiyo serikali inayafanya mambo tofauti kabisa kwa wafanyakazi wake wengine fikiria walimu, makarani, askari kama yule aliye kuwa analalamika hadharani akisema mke wake ni mwalimu ana ahueni kuliko yeye. Ulinganishe watumishi wote hawa na wabunge ambao spika wao anamwita Jerry kwenye kamati kwa kosa la nafsi yake kumsuta na kuwaambia wenzake walipe tozo kutoka kwenye mishahara yao.

Kweli wabunge wetu wasingeona fahari mh Mwigulu akitutangazia kwamba tumekusanya bilioni kadhaa kutoka kwenye tozo ya miashara ya miezi 3 ya wabunge na fedha hizi tayari zimepelekwa kuchimba visima vya maji kadhaa kwenye vituo vya afya/ shule zilizo na changamoto ya huduma hiyo ya maji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…