Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima: Naweza kufanya kazi yoyote ambayo haijakatazwa kibiblia, Mungu alijitambulisha kwa majina tofauti!

Ndo breaking news ya leo ? Uko mlipo kuwa kanisani kwake
 
Aaache unafiki, anajifanya kusafisha kauli aloisema mwanzoni kua yy ni zaidi ya mbunge.....ila anyway Kwani mbona alikata mauno juu ya kondoo wakati Biblia imekataza Uzinzi?? Gwaji miunoo akae kando, Siasa awaachie magabachori
Na yule mkewe pamoja umati wote ule...akasema zile picha si mchungaji gwajima' Aibuuu
 
JK aliweza pambana na masheikh ambao walikuwa devisive, Magufuli huyu mtu alitakiwa ashughulike nae lakini ndio kwanza anamwalika Ikulu kwenda kunywa chai.

Huyu mtu ni hatari kwa mshikamano wa Tanzania katika watu ni nao wachukia Tanzania Gwajima is on the list he is full of hatred and endorses tribalism halafu ana bahati ya kuchekewa kweli na mamlaka.
 
Anakosea sana huyu baba Askofu
 

Kwa kweli hata mimi namshangaa sana Bishop wangu....

Sijui kama ni Roho Mtakatifu kamuongoza ama vipi....

Kama ni Roho wa Bwana kamuimongoza, basi mimi sina comment maana who am I ku - challenge maamuzi ya Kristo?

Lakini nina mashaka kama ndivyo. Kwa sababu uamuzi wake unapingana na maandiko....

Kwangu Mimi Bishop Gwajima ni mmoja wa wahubiri ambao mahubiri yao hunigusa sana kiroho...

Mara zote aliposhambuliwa kiroho kwa kashfa mbalmbali nilisimama pamoja naye kwa maombi....

Kwa hili, ni kweli kabisa hakuna dhambi yoyote kwa kutaka kuwa mwanasiasa. Lakini akumbuke kuwa ndiyo anatengeneza mazingira ya kukabiliana na dhambi LIVE.....

Hata kunywa pombe wala siyo kosa kibiblia. Shida iko kwenye matokeo ya unywaji wa pombe....

Math. 6:24 inaonya na kutahadharisha kuwa hatuwezi kutumikia mabwana wawili kwani unaweza kumpenda huyu na kumchukia yule. Inaendelea kusema, hatuwezi kumtukia MUNGU na wakati huo huo MALI...

Mtu aweza kuanza kujitetea kuwa hapo imetajwa "MALI" na siyo "madaraka ya Ubunge ama Urais" na Bishop Gwajima kama ni mali tayari anazo na kwa hiyo huko bungeni hafuati "MALI"...

Kwa mtu kujitetea hivi ni kutoyajua maandiko....

Yesu alipojaribiwa na shetani kwa kupandishwa juu kinarani na shetani na kisha kuoneshwa TAWALA na FALME za ulimwengu huu, moja ya vitu alivyooneshwa kwa sharti la kumsujudia shetani ni " utawala wa dunia hii" kama ubunge, Urais nk

Yesu alikataa kwa sababu alitambua hili kwamba hataweza kutumikia kusudi la BABA YAKE lililomleta hapa duniani huku akiwa na majukumu mengine ya utawala wa kidunia....

Mimi sina hakika kama Bishop Gwajima ameambiwa na Mungu kuchukua maamuzi haya. Mimi nadhani huu ni msukumo toka nje na siyo wa Roho Mtakatifu....

I am afraid kuwa amenasa katika mtego wa Ibilisi na sasa anakwenda kuiua huduma yake kwa kutumia mikono yake mwenyewe...

Muda anao wa kutafakari upya maamuzi yake. It's not too late....
 
Naomba na mimi nichangie kwenye mada hii! Askofu huyu ni mpumbavu, hakuna tafasiriya hivyo kwenye Biblia. Tena Biblia imekataza kabisa huwezi kuwatumikia mabwana wawili! Yeye kama ameamua kumtumikia Mungu abaki huko huko!! Ila ukweli ubaki pale pale bila mbereko ya polisi hawezi kushindana na Halima!
 
Huyo Baunsa Mandingo asituzengue alishasema hawezi kugombea ubunge maana mtumishi ni zaidi ya ubunge hivyo ni kujishusha.
 
Hakika Ni sawa kabisaa # Dunia Imepufushaa Akili za watumishi wa Mungu kuwa hurusiwi Kuchukua nafasi za kiserikali # Gwajima keep Going
 
Kwa
Hapa lazima uwe Mtu mzima KWENYE Mambo ya Mungu ndo Utamuelewa Gwajima # lakini wachanga wote Hawatamuelewaaa #
 
Hapa
Hakika GWAJIMA Yuko Vizuriii na Mungu
#Kama Unamkubari Gwajima nawe pia uko Vizuriii hata ki Akili
 
Usijifananishe na Mungu mkuu Mungu atakuadhibu
 
YAANI HUYU JAMAA KAMA AMEWALOGA VILE WAUMINI WAKE.. .

ANAWAPELEKA VYOVYOTE ANAVYOTAKA.. . .

ANAGEUZA GEUZA KAMA CHAPATI.. .
Wajinga siku zote ndio waliwao kuna wapumbavu wengi sana wanadanganywa miaka yote
 
huyu akipitishwa anapigwa saaa 4 hasubui na akitoka huko ana kuta kanisani kwake hata mumin mmoja hayupo,anafikili bado mahalufu? umaalufu wake ulisha isha kitambo
 
Kila mtu ale kulingana na urefu wa kamba yake, kwani msigwa ni mchungaji wa nini?
Aya Rais mpya wa Malawi anatokea wapi?
Aache utapeli, naona sasa anapeleka siasa kanisani na waumini wake watakuwa wanamshangilia kama kawaida yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…