Leo nimemsikia Gwajima akisema hataruhusu vyombo vya ulinzi, madaktari, manesi na viongozi wa dini wachanjwe! Nimepatwa na mshangao mkubwa na mshituko nikajiuliza mtu huyu katoa wapi ujasiri wa kuamuru au kutoa ushsuri kwa vyombo vyetu vya ulinzi nini wafanye na nini wasifanye! Hajui kama jeshini kuna chain of command? Au siku hizi kapewa cheo cha msemaji wa jeshi letu na madaktari wetu?
Gwajima kasahau kwamba nchi hii ina Amiri jeshi mkuu ambaye pia ni Rais wa nchi ambaye aliunda jopo la wataalam wakaja na mapendekezo ya kitaalam..Yaani Gwajima anataka vyombo vyetu vya ulinzi wapinge amri halali ya Amiri jeshi mkuu!? Kwa lugha nyepesi Gwajima anafundisha uasi jeshini?
Hajui kama anachokifanya ni uhaini tena mchana kweupe? Huyu Gwajima hajui adhabu ya uhaini? Kama ana mawazo yake na mapendekezo yake hajui namna ya kuwasilisha mpaka kuanza kuwahimiza wanajeshi wetu wagome !
Huyu Gwajima amejisahau kiasi hiki au ni laana ya kumtukana Pengo? Nitashangaa huyu Gwajima asiposhughulikiwa kwa kuhimiza uasi kwa vyombo vyetu vya ulinzi na madaktari wetu!