#COVID19 Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

#COVID19 Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

Ni wazo baya sana kuwachanja chanjo ya Corona askari wa majeshi yetu kwa sababu hatujui usalama wa hizo chanjo.

Baba Gwajima amesema anapinga kwa 100% vyombo vya dola kuchanjwa kwa sababu tunaweza kupoteza taifa. Askofu Gwajima amesema haya Kanisani kwake leo.

Askofu Gwajima amewataka wafuasi wake na wapiga kura wa jimbo la Kawe wakatae kabisa kuchanja kwa sababu watapata hasara kubwa sana maishani.

" Naikataa kabisa chanjo ya Corona " amesisitiza baba askofu.

Chanzo: Mtandao wa You tube!
Kwa hiyo Wapewe Wananchi kama inauma iwaue Wananchi? Kweli Wewe Matope kabisa

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Kwenye Hili la chanjo naungana na hayati JPM,

Kwenye Hili naungana na Jpm, kweny uongozi wa JPM asinge ruhusu wa Tz kua sehemu ya majaribio....

Hata wengi huku benchi tulio wai kua na ndoto za kua Rais hata zisipo be accomplished atleast kuna chuma kili ishi maono yetu.....
Yes, kuna mambo tulipishana nae ila kweny Hili alitukoshaa....

Kuna tabia za JPM ambazo tipically ni zangu....

Jpm angali hai wasinge thubutu kuleta hizo chanjo.

Namuunga mkono Gwajima kweny chanjo...Tumekataa kua sehemu ya majaribio...

Napenda nisikie maoni ya Kiranga kuhusu huu mjadala.
 
Watu sio kwamba hatutaki chanjo. Hoja ni kuhakikishiwa usalama wake. Sio na hiyo WHO bali na vyombo vya serikali yetu.

Kama vyombo vya serikali haviwezi tujitafakari kama Taifa.
 
Unaongea na mtu anayeishi ulimwengu mwingine, ni kama kumpigia mbuzi gitaa acheze au kumlazimisha punda anywe maji mtoni 🤣
 
Atake asitake......! Tutamuongezeaaaa mudaaa!!!! Hii ilikua lazima iwe tuuu 🤣🤣🤣🤣
Askofu Gwajima amemtaka mwenyekiti wa CHADEMA mh Mbowe kufuta kauli yake ya kutaka chanjo ya Corona iwe ni lazima.

Gwajima amesema Chadema ni chama cha demokrasia hivyo ni lazima Mbowe aishi kama mwanademokrasia na siyo dikteta.
Kama Freeman Mbowe analazimisha chanjo angali yupo Ufipa je akifika Ikulu itakuwaje?!

Mungu awabariki!

Pia soma > #COVID19 - CHADEMA: Chanjo ya COVID-19 iwe ya lazima
 
Ni wazo baya sana kuwachanja chanjo ya Corona askari wa majeshi yetu kwa sababu hatujui usalama wa hizo chanjo.

Baba Gwajima amesema anapinga kwa 100% vyombo vya dola kuchanjwa kwa sababu tunaweza kupoteza taifa. Askofu Gwajima amesema haya Kanisani kwake leo.

Askofu Gwajima amewataka wafuasi wake na wapiga kura wa jimbo la Kawe wakatae kabisa kuchanja kwa sababu watapata hasara kubwa sana maishani.

" Naikataa kabisa chanjo ya Corona " amesisitiza baba askofu.

Chanzo: Mtandao wa You tube!
Kama anazo fact aweke wazi kwa nini chanjo siyo salama. Otherwise itabaki maelezo yasiyokuwa na msingi wowote ule na ni taarifa potofu kwa jamii. Mzigo umeshafika na imetolewa taarifa kuwa chanjo itakuwa hiyari, anayetaka aende akapige chanjo asiyetaka akae nyumbani. Sasa hivi ng'eng'eee zinatoka wapi?
 
Akina kibwetere hawatakuja kuisha hapa Duniani!!! Gwajima pia anaweza kujaribiwa na Shetani,... kama Mtume wote kina Daudi, Petro, Paulo alijaribiwa na Ba yesu mchawi tena wazi wazi kwani yeye gwajima ni nani asijaribiwe??...

hata km Gwajima ni mtumishi wa Mungu kweli hawezi kuzidi utumishi wa mtume Paulo ... Jamani wa TZ kwa nini hamuelewi? mmeruhusiwa kuwajaribu hawa wachungaji wenu wano jiita watumishi!!

km haitoshi Yesu Mwana wa Mungu hasaa!! alijaribiwa na shetani tena mara kibao tu! eti '' ageuze mikate ale''!! Gwajima yeye nani asijaribiwe kwa hili ili kupoteza umati wa TZ?? eti awe sahihi tuuu! wkt woote?? mweee!! akome tena

ningekuwa Rais ningeanza nae ili aka ombewe vizuri hukohuko kizuizini akili imkae sawa!! KM kweli unamuabudu Mungu wa kweli Basi atakuwa wa wote tulioumbwa nae!! siyo yeye tu!! hata kipindi cha Yesu kulikuwa na Manabii wa uongo weeengi!!

Na ilitabiliwa zamani sana kuwa siku za Mwisho kutakuwa na Manabii wa uongo!! watafanya maajabu ''wajaribuni!!! yamkini watashusha Moto kutoka Mbinguni. hayo ya miujiza kuokoa misukule!! kweli utaokoa sana lkn sisi kamwe Gwajima haya tutishi!!! elewa hivo...

Mungu ni wa wote Gwajima anapaswa kujua hili si wa Gwajima peke yake!! kiasi kwamba tumsikilize yeye tuuu!! Tujisaidie kwa kumuweka Mungu wetu mbele! wkt tukichukua tahadhari !! sisi km taifa hatuta kaa kusubili mungu wa Gwajima atende!!

Mungu wa Sabato, Islam, Rc, Budha nk ndiyo Mungu wa Gwajima au... hata hao waumini wake ni kuwachapa viboko tu mpaka watie akili, huyo mungu wako anaruhusu Bendera ya sinagogi la shetani tena kwenye Mimbali ya kanisani kwako!! wengine wanaona si kweli!

Km kweli Wazungu wanataka tufe!! ,... mbona wao wanakufa sasa?? km haitoshi wana wa israel waliuawa huko Misri lkn bado wakawa wengi tu? Ukimwi tumeletewa Mbona tunakula bata sambamba kwa mtiti wa watu kuliko hata hao waletaji??

hata wakileta hiyo covid acha ije hatuogopi tutachukua tahadhari km kawaida lkn Mungu ana jambo na sisi!!! huwezi zuia kauli ya Mungu kwa kuweka tahadhari ambazo Mungu hakusema, Imani yako ndo itakuokoa siyo imani ya gwajima!!

alisema siku za mwisho yatakuja Magonjwa hatari yasiyo kuwa na Dawa!! sasa si ndo safi unabii unatimia? omba kwa bidii ukijua mwisho sas unatimia!!! kuyakwepa hayo ni kupinga unabii wa Mungu usitimie yawache yaje!! unabii utimie!!

Kuto chukua tahadhari Maksudi eti gwajima mtumishi amesema ni kumjaribu Mungu!! utakufa wewe gwajima kwanza! kmkibwetere alivo potea usicheze wewe...Unisikie!! najua unapita pita humu na walee wachungaji wako! watakwambia!

Atatuvusha salama tu km alivo vusha wana wa Israel! lkn siyo wewe gwajima utuvushe !! mtu km wewe pia unae weza rubuniwa na shetani huyo huyo! ili kupoteza umati!! haya yalimpata mtume paul pia!!! ebu tupe nafasi tuabudu kwa uhuru bana......
 
Huwa wanajeshi wanatumika wachache tu Kwa ajili ya majaribio na sio wote.

Sasa mamlaka waangalie namna wanafanya ,

Isiwe wote ila Wachache tu Kwa ajili ya kuangalia uelekeo wakee.
Serikali ndio ilikuwa ya kwanza kupotosha wananchi wake, ndio maana sasa inakuwa ngumu kueleweka!!na wale wapotoshaji ndio hao hao leo wanaipigia debe!!hayo ni mawazo potofu tu kuwa eti wanajeshi wachanjwe kwa majaribio!!ina maana hizo nchi nyingine walizochanja wanajeshi, hawana akili kama tayari mmshekubali chanjo?!!hao manesi , madaktari polisi hawana umuhimu kwa taifa?!!
 
Askofu yuko sahihi kabisa! acha wachanjwe wengine kwanza, Kwani wanausalama ndio nchi yenyewe, ndiyo amani pia, huko kwa papa wanaandamana kuishurutisha serikali ije na majibu ya maswali yao,

serikali iseme wazi na itoe takwimu juu ya wanaokufa, je ni wote hadi waliochanjwa?
 
Huwa wanajeshi wanatumika wachache tu Kwa ajili ya majaribio na sio wote.

Sasa mamlaka waangalie namna wanafanya ,

Isiwe wote ila Wachache tu Kwa ajili ya kuangalia uelekeo wakee.
Uangalie uelekeo kupitia roho za watu..?...
Muogope Mungu.
 
Mzee porno huyu anatafuta kiki ya kutokea. Hana issue

Aliahidi kuwapeleka Marekani wanakawe wote. Mbona kimya??
 
Je ukichanjwa huvai tena Barakoa?
Je ukichanja
Hutaambukizwa Covid?
Je ukiambukizwa kuna uezkano wa uliyechanjwa kuambukiza wengine?
Je upo uezekano wa aliyechanjwa kufariki kwa covid ?

Kama majibu yote utajibu sawasawa basi hakuna haja ya chanjo kwa sasa.
Ingekua vipi toka enzi zile tumechanjwa chanjo ya TB alafu tukaendelea kuvaa barakoa mpk leo.
I stand with Gwajima.

Alafu ww hushangai kwanini chanjo hii tu,mbona za huko nyuma hazilalamikiwi tangu kipindi hicho hata sasa?
 
Gwajima ni CCM mwenzangu....

Ila....

Ni mtu mjinga sana.....ndio maana NCHI ZETU tukatenganisha DINI NA UTAWALA.....

Hawa watu wa IMANI KALI za DINI ukiwapa waendeshe IKULU basi ujue TUTAUISHI UJINGA NA UPUMBAVU.....

#TwendeniTukachanjwe
#KaziIendelee
#NchiKwanza
Kuwa CCM na kupinga chanjo ya corona vinauhusiano gani? Kwani chanjo nayo ni Sera ya CCM?
 
..watu wameenda kusikiliza neno la MUNGU halafu Gwajima anaanza kumzungumzia Mbowe.

..Nadhani Gwajima angetafuta jukwaa sahihi la kumshambulia Mbowe na sio kutokea Kanisani.

..Ningemshauri apumzike Uchungaji ajikite kwenye UBUNGE.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Huu unafiki ni wa kiwango cha lami!

Kipindi kile mnawahi kukaa siti za mbela kanisani kwake ili kusikiliza ubuyu wa Bashite lilikuwa neno la Mungu lile?
 
Haiwezi kuwa uchochezi. Hizi chanjo hazijafanyiwa utafiti wa kutosha. You take them at your own risk.

..lakini msimamo wa SERIKALI ni kwamba chanjo za covid-19 ni salama.

..sasa Gwajima anaposema polisi na wanajeshi wasichanjwe ana maana gani?

..hudhani kuwa amevuka mipaka kuizungumzia serikali na vyombo vya ulinzi na usalama namna hiyo?
 
...na wao wameonyesha mfano kuanza kuchanjwa wao.
Hapo usinidanganye kuwema wamechanjwa take care ndg.

Umeshasema hatuwezi kuwafikia na sisi as afrikan hatujawai toa mchango wowote, (labda) BUT...

Iyo chanjo kama ina madhara unadhani vile vichupa is serious vina kile kimiminika chenyewe cha k8nga ya covid?.

Wale jamaa ni great thinker na wanatumia akili sana, so usione wanadungana masindano ukadhani ni kinga ya corona NO!.
 
Huyo Gwajima nina uhakika 100% amechanjwa tayari. Waumini wake wamuulize ana safiri vipi nje bila kuchanjwa?
 
Gwajima ni Mbunge, Sasa kwa wadhifa wake Kwanini asingetumia Bunge kusemea jambo hili??. Kwaajili ya faida ya Wanawanchi wote.Sasa hapo sijui anapinga km Askofu au km Mbunge??.
 
Back
Top Bottom