#COVID19 Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

Mmeuita sana na kuutukuza,lazima uwashinde tu
 
Baada ya jana mbunge wa Kawe mh Gwajima kuwataka watanzania waikatae chanjo ya Corona leo wameibuka wabunge machachari wa CCM January Makamba na Dr Kigwangalla na kumjibu

Kigwangalla amemtaka Askofu Gwajima ajisomee majalada ya sayansi na kama hawezi basi aende ofisini kwake akampe twisheni kwa sababu yeye ni daktari wa binadamu kitaaluma.

Naye January Makamba amemtaka askofu Gwajima kuacha kutumia nafasi yake ya uongozi wa kiroho kuupotosha Umma

Mungu ni mwema wakati wote!
 
Huu ndiyo unaitwa utapeli kwa kutumia neno la Mungu. Unaootosha wajinga wa neno la Mungu kwa kutumia maandiko.

Hata katika magumu gani sitamwacha Mungu. Nitawasikiliza wale ambao Mungu amewaleta kwetu ili kulihuisha neno lake.

Kamwe sitapumbazwa wala kupotoshwa na matapeli na walio wakala wa shetani, kama Gwajima, anayelitumia neno la Mungu kutimiza uovu na ukahaba wake.
 

Ufunuo wa Yohana 13:16-18
Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;

tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake

Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.
 
Hatutaki wote mchanjwe, kwanza hazitoshi.
Tunachotaka ni muache upotoshaji mkiongozwa na askofu wenu uchwara gwajifix
 
Habari!

Hili jambo nililisikia 2020 toka kwa waumini 2 wa Gwajima.

Mimi niko karibu na waumini kadhaa wa Askofu Gwajima ambapo kati yao 2 ninafanya nao kazi ofisi moja, idara moja. Na hao wote ni wachungaji wa kikundi (Ministry pastors) wa kanisa la Ufufuo na Uzima.

Aliamini huenda angerithi mikoba ya Magufuli 2025 lakini Magufuli ametangulia mbele za haki.

Je, atasubiri mpaka 2030 pindi atakapomaliza Rais Samia Suluhu?
Hapana.

Hataweza kusubiri 2030 bali atajaribu karata yake ya bahati 2025.

Msitegemee 100% kuwa Gwajima atamuunga mkono Rais Samia Suluhu kwa sasa.

Gwajima mtu mwenye akili nyingi anaweza kuipiga ngome ya mama na ikapigika. Ngoja tusubiri.

Hii ni tetesi hivyo naomba msiufute huu uzi, hauna dhamira ya uchochezi.
 
Pesa pesa pesaaaaaa... Bill Gates kakuona😀
 
Wote wana kesi za kujibu. Ushahidi na uhalisia wa kesi ndiyo utakaotambua haki ya kila moja. Ni kosa kuingilia uhuru wa mahakama
 
Maagizo leo ni full frontal assault kwenda kwA Gwajima,,,,😂....Kwani si tumekubaliana tujenge uchumi kwanza?
 
Mropokaji huyo na urais wapi na wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…