#COVID19 Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

Waumini tumpuze Askofu Gwajima kuhusu Chanjo ya Corona maana ata Biblia imetamka wazi kujikinga na magonjwa ya mlipuko

Kuna Mahusiano makubwa Sana Kati ya sayansi na Biblia. Ndani ya biblia mambo mengi yameelezwa namna ya kujilinda na afya zetu.

Serikali kupitia wizara ya Afya inavyosema watu tuchukue tahadhari dhidi ya ugonjwa wa CORONA wamesimama kisayansi zaidi lakini nikukumbushe Askofu Gwajima kuwa hata katika Biblia katika wakati wa Sheria za Musa waliwatenga wagonjwa wenye magonjwa ya mlipuko Kama ilivyo kwa Coronau ili kuwalinda watu wengine dhidi ya magonjwa hayo. Rejea mambo ya Walawi sura ya 13 na 14 utapata somo zuri sana Askofu Gwajima.

Pia Biblia imesisitiza Sana maswala ya usafi katika kujikinga na magonjwa ya mlipuko. Mfano kasome kitabu cha Hesabu sura ya 19:11, 19 utaona jinsi Musa alivyokuwa mkali katika swala la usafi wa kunawa mikono kujilinda na magonjwa.

Askofu Gwajima kasome kumbukumbu la torati pia utapata somo kubwa sana juu ya umuhimu wa kujikinga na Afya sura 23:13.

Sijajua Askofu Gwajima kuhofia Chanjo ya Corona hofu inatoka wapi wakati kitabu cha Mungu (Biblia) anachokitumia kimempa mamlaka kisayansi kujilinda na afya zetu.

Askofu Gwajima ulichanjwa ndui vipi kabla ya kuchanjwa ulipata wasaa wa kwenda kiwandani kuangalia hiyo Chanjo jinsi ilivyotengenezwa? Tusitoe matamko katika madhabahu bila kupima uzito wa tamko hilo.

Askofu Gwajima anahofu ya Chanjo wakati amewaruhusu wanae kuchanjwa ili kwenda masomoni Uingereza ila hapa anatufanya Watanzania Mazwazwa.

Askofu Gwajima kaa utafakari namna Bora ya kuwalinda na kuwashauri Waumini sio kila kitu unajua

 
Bado nasubiri trip ya USA hayo mengine pambaneni tu.
 
Mara ya kwanza nilimwona kama ni mpayukaji tu na hajielewi. Lakini kwa hiki alichokiongea hapa kina mashiko. Nmeweka Chuki pembeni natumia akili kutafakari. Na naomba wataalamu waje wamjibu kitaalamu.

Pili nampongeza kwa kutoyumba kimsimamo. Taifa linahitaji watu wenye msimamo. Hata nikitokea kuchanjwa leo but ntampongeza ambaye ameshikilia msimamo alio nao toka mwanzo. Ndo UANAUME HUO.

Your browser is not able to display this video.
 
Mjinga huyo, hapo kanisani watajadili?

Yeye ni mbunge ana nafasi kubwa kuwawakilisha bungeni.

Hivi ilikuwaje Kawe nzima akapewa ubunge huyu mtu
Alishawasikisha bungeni ushauri wake kuhusu chanjo za COVID19.
 
Huyo Gwaji yupo CCM ipi? tuanzie hapo kwanza maana haeleweki aliwahi sema uchungaji ni zaidi ya ubunge leo yupo bungeni na anaropoka tu mradi maneno yanaunganika.
 
Sukuma gangs.... Mtakufa woooooote.
 
Ukimsikiliza vizuri utamwelewa.
Chanjo hii bado haina usalama kwa kuthibitika.
Anachotaka ni kujihakikishia.
Mimi binafsi siwezi chanjwa Mimi siwezi nikawa sehemu YA majaribio.
Ujue ukweli hata nje huko haya mambo yanatafrani.
Anachosemea kuhusu usalama wa watu NA vizazi vyao muhimu achana NA siasa
DNA NA vinasaba vingine jamani havichezewi [emoji41][emoji41][emoji41][emoji41]
 
Hadi hapa sijaona aliyempinga Gwajima Kwa hoja zenye mshiko zaidi ya mihemko na chuki binafsi.
Hili ni tatizo!
Kweli kabisa watanzania wengi wafuata mikumbo NA wepesi kusahau.
Kama walituletea barakoa feki vipimo feki watashindwaje chanjo feki.
NA vipi Kenya korona haipo?
Marekani haipo?
Ana fact sana sema watu wamejazwa upepo.
Huwezi jaribu nchi nzima kama inafahaa kwanini inaonyo kuhusu madhara wao kutohusika?
Kwanini hata ukiwa NA chanjo bado uvae barakoa nk
Mimi sichanji labda daktari atakayekuja kunichanja aje akiwa tayari kuishi au kufa Mimi au yeye
 
Hoja ya Gwajima lazima ipewe majibu ya kina na yente utaalamu na siyo kutumia mipasho kumjibu.wataalam wetu watueleze side effects ya chanjo hiyo Mara baada ya kuchanjwa.kumtukana na kumdhihaki Gwajimu hakutasaidia chochote, Mie ingawa si muumini na mfuasi wa Gwajima Ila kwa Hili nipo pamoja naye mpaka pale majibu ya kina yatakapo tolewa.Gwajibu katoa hoja hivyo asitishwe kwani taifa Hili Ni la kwetu sote hakuna mwenye hatimiliki nalo.wanasiasa wasitumike kuwashawishi watu kuchanjwa bali wachanjwe wao na familiya zao asiyetaka asilazimishwe.
 
hajakataa kujilinda amesema chanjo haaziaminimi
 
Gwajima ni kichaa
 
Point. Kuna hoja muhimu zinazohitaji majibu na ufafanuzi

1. Chemical content zilizomo ni zipi?

2. Effects zake ni nini? (Long term na short term).

3. Chanjo tunayochanjwa watu weusi ni sawa na wanayochanjwa watu wa dunia ya kwanza? Kama siyo, kwanini?

4. Chanjo watakayochanja wakubwa zetu ndo tutayochanjwa akina kajamba nani?

5. Kwanini serikali inayotuaminisha kuwa chanjo ni salama wanajitoa kudhamini chanjo hii? Kuwa madhara utayopata wao hawahusiku?

6. Any scientific proofs kuwa tz wamefanya utafiti wa kimaabara na kuonyesha kuwa chanjo hii ni safe?

7. Kwanini movement ya corona inakuwa kubwa sana kipindi hiki? Yaani hatupumui, tukilala corona, tukiamka corona. Kuna nini nyuma ya pazia? Serikali nzima sasa wimbo ni corona corona corona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…