Waumini tumpuze Askofu Gwajima kuhusu Chanjo ya Corona maana ata Biblia imetamka wazi kujikinga na magonjwa ya mlipuko
Kuna Mahusiano makubwa Sana Kati ya sayansi na Biblia. Ndani ya biblia mambo mengi yameelezwa namna ya kujilinda na afya zetu.
Serikali kupitia wizara ya Afya inavyosema watu tuchukue tahadhari dhidi ya ugonjwa wa CORONA wamesimama kisayansi zaidi lakini nikukumbushe Askofu Gwajima kuwa hata katika Biblia katika wakati wa Sheria za Musa waliwatenga wagonjwa wenye magonjwa ya mlipuko Kama ilivyo kwa Coronau ili kuwalinda watu wengine dhidi ya magonjwa hayo. Rejea mambo ya Walawi sura ya 13 na 14 utapata somo zuri sana Askofu Gwajima.
Pia Biblia imesisitiza Sana maswala ya usafi katika kujikinga na magonjwa ya mlipuko. Mfano kasome kitabu cha Hesabu sura ya 19:11, 19 utaona jinsi Musa alivyokuwa mkali katika swala la usafi wa kunawa mikono kujilinda na magonjwa.
Askofu Gwajima kasome kumbukumbu la torati pia utapata somo kubwa sana juu ya umuhimu wa kujikinga na Afya sura 23:13.
Sijajua Askofu Gwajima kuhofia Chanjo ya Corona hofu inatoka wapi wakati kitabu cha Mungu (Biblia) anachokitumia kimempa mamlaka kisayansi kujilinda na afya zetu.
Askofu Gwajima ulichanjwa ndui vipi kabla ya kuchanjwa ulipata wasaa wa kwenda kiwandani kuangalia hiyo Chanjo jinsi ilivyotengenezwa? Tusitoe matamko katika madhabahu bila kupima uzito wa tamko hilo.
Askofu Gwajima anahofu ya Chanjo wakati amewaruhusu wanae kuchanjwa ili kwenda masomoni Uingereza ila hapa anatufanya Watanzania Mazwazwa.
Askofu Gwajima kaa utafakari namna Bora ya kuwalinda na kuwashauri Waumini sio kila kitu unajua
View attachment 1869698