The Khoisan
JF-Expert Member
- Jun 5, 2007
- 16,434
- 14,547
Wanajeshi wa Tanzania hawatakuwa wa kwanza kudungwa chanjo. Nchi nyingi tu tu tayari wanajeshi wameshadungwa ...!!Kuna kile kijikamati kiliundwa hivi majuzi, kikaja na mapendekezo kwamba wanajeshi wote wadungwe chanjo kwa sababu ati wako kwenye mstari wa mbele wa maambukizi.
Kutokana na ufinyu wa maarifa wa hao wanaoitwa madaktari na wanasayansi wa Tanzania; mpaka sasa hawajaweza kutoa taarifa kamili ya kisayansi kuhusu madhara marefu na mafupi ya chanjo hizo.
Madaktari wetu wanategemea maarifa kutoka ulaya na nchi zingine za magharibi. HAWAJIWEZI.
Ndio maana kabla ya kudungwa chanjo, unapewa fomu ujaze ambayo inasema kwamba SERIKALI HAITAWAJIBIKA KWA MADHARA YOYOTE YATAKAYOKUPATA BAADA YA WEWE KUDUNGWA CHANJO.
Kwa vyovyote vile, chanjo hii haina ithibati ya usalama.
Ni gunia lililotoka ulaya wakalibwaga nchini halafu tunaambiwa tulifakamie.
Kuwadunga chanjo wanajeshi na vyombo vingine vya usalama bila kujiridhisha usalama wake ni jambo ambalo hata fyatu hawezi kulielewa.
Ni vyema serikali iachane na haya machanjo ya ajabu ajabu ya mwendokasi hayafai yataliangamiza taifa.
Anyway, wanajeshi wao kama walinzi wetu ndiyo lazima wawe wa kwanza kuhakikisha usalama wetu .... hivyo chanjo kuanza na wao inamake a lot of sense.