#COVID19 Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

1. Mwinyi mzee wetu. Huchomi chanjo?

2. Kikwete huchomi chanjo?

Anyway.... Kachomeni chanjo. Na mchome waziwazi watu wasiseme mnaiigiza. Tumeona watu wakikosoa uchomaji wa Rais Samia..mi naamini alichoma ila walitumia sindano ambayo haiumizi au walimchoma ganzi kwanza.

Maana mpaka amemaliza kuchomwa alikuwa hajui ikabidi aambiwe tayari bila shaka. Jinsi alivyo ngangari.

Ni akina nani wapo nyuma ya Gwajima? Gwajima ana watu. Niamini mimi ana watu ambao wanajua anafanya nini.

Mimi huwa sikubaliani na Gwajima katika mambo yake mengi toka kipindi ameanza jihusisha na siasa zake za conflict n.k

Lakini ni nini anachokifahamu vizuri ila hakisemwi na watu wengine? Mi nashauri serikali iwateua mabalozi wa chanjo wawaelezee watanzania umuhimu wa chanjo.
 
Mi nadhani hao wote uliowataja akiwemo Samia mwenyewe walishachanjwa tangu zamani Kama wanaziamini chanjo hizi wasingesubiri hadi leo.

Alichokifanya Samia siku ile ilikuwa "demonstration" Kama wanavyozindua ujenzi wa majengo kwa kukata utepe.

Angesema ameshachanjwa asingeeleweka kirahisi Kama Rais. Walikosea kumuaandaa tu ndiomaana ikawa vile
 
Hao uliowataja unajuaje hawana chanjo..?????
Kikwete yuko Ulaya hana chanjo???? au mpaka ajitangaze
 
Uko sahihi kabisa
 
Hata mimi sijachoma, lakini nikiihitaji nitachoma sina shida. Ila huyo mhubiri anatumia vibaya sehemu yake kwa kulaghai wasikilizaji wake. Mimi ni Mkatoliki, lakini padri au askofu wangu akihubiri pumba siwezi kukaa na kuendelea kumsikiliza. Kila mahubiri lazima niyachuje na kuyapima kama yanaendana na masomo ya hiyo siku na kama ni mifano inayotolewa je inaendana? Lakini kuhubiri mambo ambayo ni unrelated na bila justification huwa naona ni wastage of time. Wahubiri wengi wanajificha kwenye Neno la Mungu, lakini wanachohubiri ni off-point na out of place.
 
Gwajima kasemea watu wengi Sana hata wataalamu wa afya,maana haijawahi patikana chanjo ndani ya mwaka mmoja.

Chanjo ambayo hata aliyechanjwa haiamini.Tangu rais achanjwe anaendelea kuvaa barakoa, Sasa chanjo ya Nini?
 
Kikwete yuko London kwenye mkutano wa Global education, na mama ndalichako haiwezekani ameruhusiwa kuingia UK bila kuwa na chanjo. Huyu mzee atakuwa aliifuata chanjo Marekani ya pfizer au moderna.
 

Labda. Lakini tunajua kitu kimoja, kwamba, imeandikwa "....hamkosi kuzitambua hila (mikakati yake - shetani kwa kutumia agents wake) mbaya..."
Unaumiza kichwa chako bure. Inasikitisha hata humjui wala kum - acknowledge aliyekuumba na anayeendelea kukufanya uishi mpaka leo na kuandika. Naye huyo aliyekuumba anasema hivi; "....watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa..." HOSEA 4:6a

Aliye nyuma ya Gwajima ni mmoja tu. Mungu Muumba wa mbingu na nchi na vyote vilivyomo katika Yesu Kristo. Huyu ndiye anayempa jeuri Gwajima kumpinga shetani na kazi zake zote...!!

Mwisho utakubaliana naye tu. Yuko huko for a special mission. Na mission hiyo ndiyo taratibu inaanza kuwa wazi. Wengi hatukumwelewa lakini sasa tunaelewa kwanini aliamua kuingia kwenye active politics kwa namna ile...
Ni uwezo aliopewa na Mungu Yehova ktk Yesu Kristo ma kuona mambo beyond normal human being capability.. Hii ndiyo tofauti yake na wewe na wengine. Mimi naelewa na sishangai wala ku doubt kila asemacho..
 
Gwajima ndio kabaki kuwa taa ya Tanzania kipindi hiki... Wengine ni mamluki na madalali wa chanjo
 
Kila mahubiri lazima niyachuje na kuyapima kama yanaendana na masomo ya hiyo siku na kama ni mifano inayotolewa je inaendana? Lakini kuhubiri mambo ambayo ni unrelated na bila justification huwa naona ni wastage of time.
Msubiri kesho analeta dose nyingine
 
Gwajima ndio kabaki kuwa taa ya Tanzania kipindi hiki... Wengine ni mamluki na madalali wa chanjo
Naam anaangaza njia ya kwenda kuzimu. Hivi Huyo Gwajima ndiye huyu au mwingine?
Kama ndiye huyu, ingawa nakiri sina hakika, anaangaza kweli kweli!
 
Hata mimi sijachoma, lakini nikiihitaji nitachoma sina shida.
Vizuri kwa kuwa utatumia hiari yako kuchagua kati ya nzuri na mbaya. Ni hiari yako
Ila huyo mhubiri anatumia vibaya sehemu yake kwa kulaghai wasikilizaji wake.
Tangu lini giza likapatana na nuru? Nuru huangaza na giza huitii nuru. Wewe bado uko gizani, huwezi kuona kitu. Utakachoona kwa mtumishi huyu wa Mungu ni kile ambacho uono wako unakiona - ulaghai...!
Mimi ni Mkatoliki, lakini padri au askofu wangu akihubiri pumba siwezi kukaa na kuendelea kumsikiliza.
Bahati mbaya yeye sio mkatoliki kama ulivyo wewe. Yeye haabudu dini, anamwabudu Mungu aliye hai..!
1. Utayachuja mahubiri hayo kwa chujio gani? Unalo hilo chujio? Kumbuka, chujio la mahubiri yoyote ni Neno la Mungu (Biblia). Lakini kwa jinsi unavyo - argue tu hapa ni ushahidi tosha kuwa una upungufu wa Neno la Mungu ndani yako..!

2. Kama Rev. Bishop Josephat Gwajima anapotosha watu (anahubiri mambo "unrelated", yasiyo na justification ki - Biblia) kama ulivyosema mwenyewe hapo juu, hebu prove kuwa yuko wrong kwa wewe kuleta justification ya ki - Biblia - Neno la Mungu..!!
 
Ana watu wapi , tatizo la Gwajima kujifanya ni spy aliechangamka, leo utamuona Gwajima ana watu ,ila ogopa watu Kama Mzee wa upako, yule ni simba na mitandao wake upo intact, na mzee yupo kimia na kupiga injili , ila yule nawambieni na amini connection yake nje ya utumishi wa mungu ipo juu Sana,

Jiulize why Maghufuli alienda sali kakika kanisa lake tena kipindi Cha KWANZA mwanzoni ya utawala wake, ? Why 2015 wakati wa Lowasa alitamka wazi pale mlimani city kwamba Kuna kushindwa uchaguzi, lakini pia ni mwalim mzuri wa kareti aliwai dhibitisha mwenyewe


Mzee wa upako ni mtumishi wa Mungu , ila mengine mungu ndo anajua juu ya maisha yake, WENDA ni Mara 100 ya Gwajima nasema, Taifa Hili Lina mfumo mgum SANA,KATIBA NI SASA,
 
Mkuu umegusa kitu kwa Mzee wa upako, hebu funguka hata kwa codes basi?
 
Kama wewe unayaamini, mimi siyaamini na wote - mimi na wewe - tuna uhuru wa kuamini kwa namna tunavyoguswa. Mimi sijawahi kuguswa na hizi 'blanket statements' au 'hoja zoazoa'.
 
Mkuu umegusa kitu kwa Mzee wa upako, hebu funguka hata kwa codes basi?
Code, ???? , Mfateni akawapeni code ,mnayoita code mie simo, najua Gwajima Cha mtoto KWa mzee wa upako, japo hajiona anajua kila kitu ,asema bwana,2015 WAKATI mzee wa upako anatoa au kuidi mchango wake KWa Lowasa si chin mil MOJA pale mlimani city, Gwajima yupo busy mjibu SLAA NA MKE WAKE pale hotel maeneo ya River side ,jina limenitoka ila nilikuepo , msafara wa Gwajima ulikuja yeye akiwa kwenye Gari yake ya Hammer,

Kweli kipindi hicho alikua kweli amesimama Kama Askofu, na ni kweli watz walimpenda, nikiwapo mie KWa kusimamia haki,ila Gwajima wa 2015, akisima na Gwajima wa 2021 watatoana makamasi nasema,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…