Askofu Gwajima: Tanzania inashindwa kuendelea mbele kutokana na kutokuwa na muendelezo wa utawala mmoja kwenda mwingine

Watukome!
 
Ila huwa tunaambiwa wanatekeleza ilani sikuwai jua kua nchi huwa inaongozwa Kwa matakwa ya raisi anataka nn ,kumbe ilani ni useless
 
Na ndiyo maana tumepiga kelele saana kuwa hii nchi inayohitaji katiba mpya itakayojenga mfumo dhabiti tukiwa tunamaanisha tuwe na sheria zinazomuongoza rais anayeingia kufuata vipaumbele vya taifa na sio vipaumbele vya 'one man show' mwisho wa siku mtu mmoja anasimamisha mradi wa gesi anarukia mradi wa maji.
 
Chidi bwayi hajaridhika namna raia walivyoteswa na dikteta uchwara, uchaguzi ukifanyika kwa haki watu kama rashidi hawatanusa hata harufu ya bunge...
Si ndio maana anataka muendelezo, maana anajua bila huo hatarudi
 
Wote hao hakuna kabisa cha maana,,
Kinachotakiwa ni katiba bora na uwazi+uwajibakaji tu
 
Mi nafikiri maendeleo ya kitu au jambo lolote, linaanza na wewe mwenyewe

Alichozungumza jamaa Ni jambo la muhimu Sana na pengine kwa siku za usoni linaweza kutokea

Lakini, muhimu zaidi wakati tunasubiri unatakiwa kuanzia ngazi ya chini, hapa nazungumzia familia

Lengo ni kuwa na maisha bora, hivyo kama mzazi au mlezi hakikisha unaweka malengo ya juu ya familia yako iweje alafu unatekeleza

Hatimaye hata mwisho wako unapofikia unakuwa katika Hali ya jambo ulilotaka kufanya japo halijatimia kwa ukubwa wake lakini umeonesha uthubutu na sio 'kulalamika'

Mwisho, haya tunayoyakudia yatokee kwa % kubwa hatutayashudia
Tunatakiwa kuweka misingi.
 
Gwaji boy asibezwe ana point kubwa sana tuache mzaha
 
Sasa Gwajima hilo umeongea mbona lipo wazi na ni marais wanaotokana na chama chako wenye kufanya hivyo...

Hilo jambo wala hukupaswa kusubiri bunge kulitamka, ungeliwakilisha tu ndani ya chama chako kwenye vikao vyenu...
 
Haya yaliyo tufikisha ni udhaifu wa katiba yetu sisi wenyewe ya 1977, wa TZ Wenzangu mkae mkijua kupititia katiba ambayo ndio muongozo wetu wanamna gani tunataka kuongozwa ili hayo yasijirudie turudi kwenye rasimu ya katiba ya Mzee Warioba ambayo wananchi walishirikiswa otherwise tukaendelea kuimba ngonjera hizo hizo hadi kiama
 
Inashindwa kuendelea kutokana na kuwa na matapeli kama yeye kwenye uongozi wakati ni mwizi na tapeli wa kawaida anayepaswa kunyea debe.
 
  • Nimemuelewa Ask. Gwajima, nafikiri maelezo yake yanasema “TUNATAKA KATIBA MPYA”, ameongeo kimsimbo zaidi ila maelezo yake yanasimbua kila kitu. Kama kila kila Rais akiingiia aliongoza kwa namna yake... hekima zake na utashi vinaamua vipaumbele maana yake... Kwa akili ya kawaida ‘maono ya miaka 50 au 30’ yatatekelezwa vipi katika utawala wa katiba ambayo inaacha mwanya wa kila Rais kuongoza kwa namna yake? Askofu hapa ‘anatutonya’ kwamba katiba tuliyonayo haifai. Inashindwa kulazimisha mwendelezo wa tawala moja na nyingine. Bila utuo tutabaki kuwa na mipango mingi kwenye makaratasi, linaanzishwa hili linaachwa. Katiba hii inaruhusu kila ‘steringi kuja na mapigo’ yake , kama tunataka mapigo saresare katiba mpya inahitajika.
  • Kwani hatujawahi kuwa na maono? Tumewahi na tunayo yaliwekwa miaka 20+ iliyopita : THE TANZANIA VISION 2025, mpango ambao uliandikwa miaka ya tisini na kitu. Maono yanazungumza vitu vingi vitamu, mpaka najiuliza ni sisi wabongo ‘tumetunga’ ama vipi, ni zama za Ndg. Rais Mkapa, ni maono hayo. Ndani humo kuna mambo ya utawala bora, Maendeleo ya TEHAMA, Elimu, Sayansi na Teknolojia, Viwanda, Kilimo: kama vitu vilivyotiliwa mkazo.
  • Hakuna mwendelezo wa dhati katika matendo. Tumekuwa watamu katika kuunda na kutunga mipango kwenye makaratasi. Kuna sera tamu-tamu zilizotungwa ili kuirejelea hayo maono ya 2025, tatizo ni utekelezaji na huku ‘kuongoza kwa namna yake’ .Kuna sheria zingine zinatungwa na zinajichanganya na maono, kwa sababu zinatungwa kwa ajili ya watu fulani– tunashida, shida ya mfumo.
  • Maono ya 2025, ambayo babu zetu walitunga (kama wewe ni kizazi cha ‘dotikom‘ — umezaliwa 1990s) yanazunguzia maendeleo ya TEHAMA, kuwa na mtanzania mwenye elimu na weledi wa kutosha kiasi cha kuwa na umahiri na ushindani katika soko la hapa ndani na duniani kwa ujumla. Sheria zikitungwa ilikukomesha watu fulani inaharibu mtiririko na muunganiko wa maono yetu. Kwa mfano, kumiliki chaneli ya You Tube kuwa gharama kubwa kwa Tanzania na vifurushi vya data, na sheria zingine zingine zinasimbua nini... Zinatoa maana ya kwamba wakati watunga maono waliona mbali, na walikuwa na uwezo huo wote— kuona mbali na karibu; waendeleza maono wana miopia, haoni mbali wanaona karibu tu! Wapi “WAPI KILIMO KWANZA” ? Wapi “BIG RESULT NOW, BRN”?
  • Maono yashikamanishwe na falsafa, katiba, sera, sheria na elimu ya nchi. Maono yasijulikane na viongozi na watumishi wa serikalini pekee, hata mtoto wa chekechea anatakiwa aungamanishwe na “jambo letu la kitaifa”. Tatizo mipango mingi inafeli kwa sababu ya maono ya Taifa kushikiliwa na watu wachache na kuwa na mzigo nayo ilihali ‘wananzengo’ hatuelewi kinachoendelea, siasa chafu zinasababisha kutunga sheria zinazokomoa hawa ili kuneemesha wale. Mbaya zaidi, siasa chafu, hazioani kabisa na maono.
  • Tanzania Nchi yangu! Tunahitaji katiba mpya, kama hili hatulioni tutarajie zaidi kuwa na maendeleo ya nasibu, kuendelea kutokana na namna ya ‘kuongoza kwa aina yake’!
 
Gwajima si askofu bali askopo
 
Lakini umeelewa alichoongea mkuu

Kaongea point hakuna haja ya kupinga kila kitu
Siipendi ccm Ila jamaa kaongea point kubwa Sana

I have learned to look things in a bigger perspective ways
 
Lakini umeelewa alichoongea mkuu

Kaongea point hakuna haja ya kupinga kila kitu
Siipendi ccm Ila jamaa kaongea point kubwa Sana

I have learned to look things in a bigger perspective ways
Sipingani naye bali sitaki mambo ya nyani kutoona kundule akaona ya wenzake. Aanzie kwake kwa kuacha utapeli na wizi.
 
Halafu cha kushangaza wote ni wa kutoka maccm lakini bado anaharibu kila kitu badala ya kuendeleza alipoishia mwenzie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…