Askofu Gwajima: Tanzania inashindwa kuendelea mbele kutokana na kutokuwa na muendelezo wa utawala mmoja kwenda mwingine

Askofu Gwajima: Tanzania inashindwa kuendelea mbele kutokana na kutokuwa na muendelezo wa utawala mmoja kwenda mwingine

Tatizo mmelundikwa huko na jiwe, mnataka anaefuata awe kama jiwe, ukatili na kuonea wengine, acha kila mtu alete maendeleo kivyake!
 
Walimsulubu CAG Asad kwa kauli hii!
Tatizo ni bunge... Mpango wa taifa na Dira ya taifa ndio vipo haijalishi Rais gani kaingia.

Mawaziri wakidai bajeti wabunge wanapaswa kugoma yaliyomo kwenye mpango wa taifa, ilani, na dira ya taifa ndio yapitishwe.

Sasa ilani inasema katiba mpya afu Rais anaingia anadai sio ajenda yake..... Hapo ndio ilipaswa wabunge wakatae bajeti ya serikali yake mpaka aheshimu ilani yake. Sasa kma wabunge wanapiga makofi tu utamlaumu Rais?

Bunge ni dhaifu period
 
Tuwe na katiba itakayoruhusu wagombea binafsi wasiofungwa na chama chochote.
Hata Mkapa aliwahi kuliongelea hilo, hiyo ni dalili kuwa CCM hawana uwezo wa kuongoza taifa hili. Ila tutafanyaje sasa maana hata hao upinzani ndio hawako serious kabisaaaa.
 
😆😆😆..the state of politics right now inachekesha..,nimekaa nimejiuliza na kujijibu kua nikisapoti alichokisema nitaitwa MATAGA au muumini wa ufufuo na uzima,nikipinga nitaitwa Bavicha au kibaraka wa mabeberu..Dah!
 
Majibu yote yako kwenye rasimu ya katiba ya Warioba, wasipindishe maneno waongelee katiba mpya.
 
Mbona yeye ameshindwa kuendeleza alipoishia Yesu kumfufua Lazaro akamfufua mwendazake?
Hamna kitu hapo, ujumbe aliodhamiria kuutoa ni kumlazimisha Mama Samia kuendeleza yale ya mtangulizi wake. Kazunguka weeee, lakini spirit ni ile ile ya sukuma gang! Akae kimya, tushawachoka kutulamisha kumpenda hayati kwa lazima. Tusilazimishane.
 
K
Mbunge wa Jimbo la Kawe Josephat Gwajima akitoa mchango kuhusu hotuba iliyotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema nchi nyingi za Kiafrika zimekuwa haziendelea kwa kasi ya maendeleo kutokana na kushindwa kutumia rasimali kwani inaendana na 'manpower'.

Pia ameeleza kuwa Tanzania inashindwa kuendelea mbele kwa kasi kwasababu hakuna muendelezo wa Regime moja kwenda nyingine ambapo kila Rais anaingia madarakani na mipango yake hivyo huathiri maendeleo ya ukuaji wa mipango iliyoanzishwa.

Gwajima amtolea mfano Nyerere alietawala miaka 20 na kuacha viwanda 411, alipokuja Mwinyi aliboresha baadhi ya mambo lakini hakuendelea na wazo la viwanda na alipoingia Mkapa akauza vyote kwa kuvibinafsisha hivyo kukosa muunganiko kati ya 'regime' ya kwanza na regime ya tatu.

Gwajima amesema watakesha kama hamna huo muunganiko kwani hata Rais wa awamu ya nne hakushughulika na viwanda, bali mambo mengine lakini awamu ya tano akaamua kushughulika na viwanda, vilevile ambavyo awamu ya tatu ilivibinafsisha na kuviuza.

Gwajima amesema ni hatari kwasababu katiba inampa nafasi kila Rais anayeingia madarakani kwa namna yake, hekima yake na kwa namna anavyotafasiri yeye maendeleo.

Amesema siku moja atakapopatikana Rais ambaye hayuko sawasawa watu wataishia kulia na kutoa ombi la kuwa na vision ya kuwa na miaka 50 ya Taifa na anapoingia Rais lazima ilani ya chama chake izungumze mambo ambayo Taifa imejiwekea kama maono.

Gwajima amehoji endapo akatokea Rais ambae anafanya mambo yake yasiyo kwenye ilani kama kuna mtu wa kumuuliza mwenyekiti wa chama cha mapinduzi na Amiri Jeshi mkuu!


hayo ni madai ya katiba mpya ,​
 
Ushabiki wa kijinga ndio shimo la maendeleo yetu

Tufanye Gwajima hatumpendi, Ila tuchukue alichokisema tukifanyie kazi haraka Sana

Kilichosemwa na Askofu Gwajima, ndilo haswaa hitaji la lazima la nchi yetu, haiwezekani mtu anakuja na dhima ya viwanda mwingine akija aseme, hivi viwanda ni vizuri Kwa kufugia kuku wa mayai tutapata faida Sana, huku ni kuzunguka mlima msijue kama mpo kwenye safari

Naunga mkono hotuba ya Askofu
Gwajima hajasema kitu kipya. Hili limeshasemwa sana sana sana na sana. Ni marudio tu amefanya. Tanzania hakuna kitu ambacho hakisemwa. Tatizo liko kwenye utekelezaji. Huyo huyo Gwajima anayesema hivi ukimwambia aunga mkono katina mpya yenye kuanisha mambo kama haya hatakubali. Anajua bila katiba mbovu na uchaguzi wa mabavu hawezi kushinda.
 
Tangu Baba wa Taifa atatungazie kuwa kilimo ndiyo uti wa mgongo wa Taifa letu. Hakutaka kabisa kugusa madini. Kama kilimo kingewekewa mikakati ya kueleweka na kwa ardhi tuliyonayo tungekuwa tunalisha Afrika nzima kwa mazao mbalimbali.

Vyuo vya kilimo vingekua na short prommes za mafunzo kwa wakulima wanaofadhiliwa na vyama vyao vya ushirika.

Kila kijiji kingekua na nyumba na shamba la mfano ambalo wanafunzi wa vyuo vya kilimo wanakwenda field kwa miezi mitatu kufanya kazi na wananchi.

Maduka ya zana za kilimo kuleta za a za kisasa na wananchi kununua hata kwa mikopo.

Vyama vya ushirika kuendeshwa na wenye elimu kuanzia ya masoko, Fedha na public relations. Vijitafutie masomo nje ya nchi.
Mkuu una mawazo mazuri sana. Tungekuwa tumechagua kitu kimoja especially kilimo ambacho tuna uwezo nacho tungelisha dunia. Na ukishaendelea kwenye kilimo mengine yatafuata kwani tutakuwa tumeshapata uzoefu wa kusimamia kitu. Haya mambo hayahitaji kelele nyingi bali ni vitendo. Tanzania tungesema kilimo ni mkombozi wetu na nguvu zote tuzielekeze huko tungefika mbali. Tuna kila nyenzo inayohitajika kwenye kilimo. Gwajima karudia jambo lilikwishasemwa kitambo mno.
 
ccm kama vyura wa masika kila chura anaimba kivyake. nape anasema mama aachwe aandike kitabu chake cha awamu ya 6, gwajiboy anataka mama aendelee alipoishia Dr. John Pombe Joseph Magufuli, rest in peace.
 
Nimesikiliza, jamaa kaongea point kubwa tangu Bunge lianze, kila Rais anakuja na mishe zake, anaharibu mfumo uliopo anaanza upya, mfano jiwe kaja kafumua fumua kila kitu , mfumo wa Elimu kafumua , mfumo wa biashara kaufmua ,mfumo wa utumishi kaharibu haribu huko na kabla hata hajaseti mambo akafa ....yaan mnarudi nyuma maili buku.

Kwa kweli tunatakiwa tuwe na maono ya kimkakati aisee, kuwe na long run plan na short run plan, wakat wa uchaguz kila chama mbali na agenda zao lazima waonyeshe jinsi watakavyokamilisha agenda za kimkakati , na hapa ndo umhimu wa katiba mpya!

Hatuwezi kuendelea Kwa kutegemea mawazo ya mtu mmoja kuwaza anayotaka yeye yawe..... Anaharibu lililopo na hata kuvunja katiba ili atimize anayotaka yeye , aaah.

Mfano mradi wa Bandari wa Bagamoyo Kwa namna yyte Ile ni wa muhimu, Bandari ya DSM tayari ipo congested na overwhelmed na pia inaelekea kuwa beyond rehabilitation. Ni heri tujadili kwamba tutafte wapi hela ya kujenga tuachane na wahisani wenye masharti magumu , na sio kuupiga chini moja Kwa moja!
Gwajima anagundua sasa yale ambayo wenzake walisoma kwenye Dev Study 101. Hata hivyo nashangaa kuwa hajui kuna Vision 2025, kuna mpango wa maendeleo wa miaka mitano mitano, na kwa vile hatujabadili chama tawala, tunaongozwa na ilani za CCM muda wote. Swala la kuvipa viwanda kipaumbele tena si la Magufuli. Magufuli alipenda kuonyesha kuwa ni lake, lakini limejaa tele kwenye ilani ya CCM 2015-2020 na hakuitengeneza yeye bali Msoga na watu wake. Hata bwawa la umeme la Nyerere si lake tena; pamoja na vyanzo vingine vya umeme, bwawa limetanda mule, na Rais wa 6 atalitekeleza tu. Kwa hiyo kuna muendelezo. Tunaweza kupingana na sera zinazoendelezwa, lakini mwendelezo upo. Gwajima arudi asome vizuri.
 
Hivi kwanini mnakaririshwa vibaya hivi unafikiri Gwajima ni iliterate kama wanaokutuma jaribuni kuchukua mawazo yanayojenga sio Gwajima amemshinda Mdee ndo imekuwa nongwa
Rashid ni dumb pastor and well known con man
 
Hapo hapo anasema Nape alidukua hotuba yake!
ccm kama vyura wa masika kila chura anaimba kivyake. nape anasema mama aachwe aandike kitabu chake cha awamu ya 6, gwajiboy anataka mama aendelee alipoishia Dr. John Pombe Joseph Magufuli, rest in peace.
 
Ameongea jambo la maana.

Japo simpendi lakini siwezi kumuattack personal. Nazijudge hoja zake.
 
Chidi bwayi hajaridhika namna raia walivyoteswa na dikteta uchwara, uchaguzi ukifanyika kwa haki watu kama rashidi hawatanusa hata harufu ya bunge...
 
Akwende zake!
Asitupangie!
Church kwake nani anaendeleza!?
 
Back
Top Bottom