Askofu Gwajima: Tanzania inashindwa kuendelea mbele kutokana na kutokuwa na muendelezo wa utawala mmoja kwenda mwingine

Askofu Gwajima: Tanzania inashindwa kuendelea mbele kutokana na kutokuwa na muendelezo wa utawala mmoja kwenda mwingine

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Mbunge wa Jimbo la Kawe Josephat Gwajima akitoa mchango kuhusu hotuba iliyotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema nchi nyingi za Kiafrika zimekuwa haziendelei kwa kasi ya maendeleo kutokana na kushindwa kutumia rasimali kwani inaendana na 'manpower'.

Pia ameeleza kuwa Tanzania inashindwa kuendelea mbele kwa kasi kwasababu hakuna muendelezo wa Regime moja kwenda nyingine ambapo kila Rais anaingia madarakani na mipango yake hivyo huathiri maendeleo ya ukuaji wa mipango iliyoanzishwa.

Gwajima amemtolea mfano Nyerere alietawala miaka 20 na kuacha viwanda 411, alipokuja Mwinyi aliboresha baadhi ya mambo lakini hakuendelea na wazo la viwanda na alipoingia Mkapa akauza vyote kwa kuvibinafsisha hivyo kukosa muunganiko kati ya 'regime' ya kwanza na regime ya tatu.

Gwajima amesema watakesha kama hamna huo muunganiko kwani hata Rais wa awamu ya nne hakushughulika na viwanda, bali mambo mengine lakini awamu ya tano akaamua kushughulika na viwanda, vilevile ambavyo awamu ya tatu ilivibinafsisha na kuviuza.

Gwajima amesema ni hatari kwasababu katiba inampa nafasi kila Rais anayeingia madarakani kwa namna yake, hekima yake na kwa namna anavyotafasiri yeye maendeleo.

Amesema siku moja atakapopatikana Rais ambaye hayuko sawasawa watu wataishia kulia na kutoa ombi la kuwa na vision ya kuwa na miaka 50 ya Taifa na anapoingia Rais lazima ilani ya chama chake izungumze mambo ambayo Taifa imejiwekea kama maono.

Gwajima amehoji endapo akatokea Rais ambae anafanya mambo yake yasiyo kwenye ilani kama kuna mtu wa kumuuliza mwenyekiti wa chama cha mapinduzi na Amiri Jeshi mkuu!


 
Nimesikiliza, jamaa kaongea point kubwa tangu Bunge lianze, kila Rais anakuja na mishe zake, anaharibu mfumo uliopo anaanza upya, mfano jiwe kaja kafumua fumua kila kitu , mfumo wa Elimu kafumua , mfumo wa biashara kaufmua ,mfumo wa utumishi kaharibu haribu huko na kabla hata hajaseti mambo akafa ....yaan mnarudi nyuma maili buku.

Kwa kweli tunatakiwa tuwe na maono ya kimkakati aisee, kuwe na long run plan na short run plan, wakat wa uchaguz kila chama mbali na agenda zao lazima waonyeshe jinsi watakavyokamilisha agenda za kimkakati , na hapa ndo umhimu wa katiba mpya!

Hatuwezi kuendelea Kwa kutegemea mawazo ya mtu mmoja kuwaza anayotaka yeye yawe..... Anaharibu lililopo na hata kuvunja katiba ili atimize anayotaka yeye , aaah.

Mfano mradi wa Bandari wa Bagamoyo Kwa namna yyte Ile ni wa muhimu, Bandari ya DSM tayari ipo congested na overwhelmed na pia inaelekea kuwa beyond rehabilitation. Ni heri tujadili kwamba tutafte wapi hela ya kujenga tuachane na wahisani wenye masharti magumu , na sio kuupiga chini moja Kwa moja!
 
Ushabiki wa kijinga ndio shimo la maendeleo yetu

Tufanye Gwajima hatumpendi, Ila tuchukue alichokisema tukifanyie kazi haraka Sana

Kilichosemwa na Askofu Gwajima, ndilo haswaa hitaji la lazima la nchi yetu, haiwezekani mtu anakuja na dhima ya viwanda mwingine akija aseme, hivi viwanda ni vizuri Kwa kufugia kuku wa mayai tutapata faida Sana, huku ni kuzunguka mlima msijue kama mpo kwenye safari

Naunga mkono hotuba ya Askofu
 
Ushabiki wa kijinga ndio shimo la maendeleo yetu

Tufanye Gwajima hatumpendi, Ila tuchukue alichokisema tukifanyie kazi haraka Sana...
Point ni njema ila kwa vile mama hatokei kanda fulani haruhusiwi kuasisi yale anayoyaona yanafaa katika uongozi wake, tuliwaambia mkatuona sisi yo wazalendo, mnaona sasa!
 
Gwajima asituchose hapa.

Kashindwa kutununulia nyavu za kuvulia samaki deep sea wana Kawe akama alivyoahidi. Kashindwa kutupeleka wana Kawe Birmingham kula bata kama alivyoahidi. Mafuriko kwenye barabara za kule Boko hata hatusemi.

Yote tisa, kumi kashindwa hata ku perform core activity yake ya kufufua watu - kamuacha rafiki yake mpendwa Magufuli azikwe tu hivi hivi wakati ana kipawa cha kufufua kweli!!
 
Mimi huwa simkubali huyu jamaa lakini katika hili kaongea ukweli kabisa na hilo ndio tatizo letu. Tuchukulie mfano Dubai wao waliweka malengo wanataka kuwa number one kwa kila kitu hawataki number 2 kwa kila wanalofanya, kama ndege, airport, utalii na sijui bandari na mengi tu lakini sio kwamba ndio wamekuwa number one kwa kila kitu lakini hayo ndio malengo yao na kila mtu apiganie hayo.

Sasa sisi kama Tanzania ni lazima tujiwekee vision je lipi tutakaloweza kututoa hapa na kutupeleka pale. Kama tunataka tuwe number one kwa kilimo Africa, tunataka tuwe nchi yenye elimu bora, afya bora na hii mifano tu basi iwe ni ilani ya kila chama iwe sharti mengine ya nyongeza kuboresha sawa tu lakini washindane sera za kutufikisha katika vision yetu. Naunga mkono hoja
 
Hii nchi swala la maendeleo tusahau kabisa

Huu ndio ukweli au nasema nasema uongo ndugu zangu

Hii nchi inaongozwa kwa muda mrefu na watu wasio na uelewa kabisa wa Dunia ya kisasa,hebu fikiria channel za YouTube zote ni free kasoro zinazomilikiwa na watanzania walioko Tanzania
 
Mbunge wa Jimbo la Kawe Josephat Gwajima akitoa mchango kuhusu hotuba iliyotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema nchi nyingi za Kiafrika zimekuwa haziendelei kwa kasi ya maendeleo kutokana na kushindwa kutumia rasimali kwani inaendana na 'manpower'....
Hata huyo anayemtetea alikiuka muendelezo wa mazuri ya mtangulizi wake tena boss wake kwa miaka kumi alimuamini kumbe amekaa unafiki na usaliti mkubwa.

Pamoja na hayo, ni kweli tunahitaji mifumo endelevu kwenye taasisi ya urais ambayo itasimamia maendeleo sawia ya nchi yetu.

Hii ndio ilipaswa kuwa kazi kuu ya TISS lakini wenzetu wamegeuka idara ya CCM na umbea tupu plus kujipendekeza ili kupewa uDC au RC. TISS ndio wangesimamia hii misingi ili muendelezo uwepo Ila tumepoteza dira ya taasisi nyeti kabisa.
 
Yeye ameshaweka agenda za kanisa lake wazi pindi nae akiaga dunia? eg;
Namna bora ya kupiga hela kwa maujanja 'makusanyo'
Nani wa kuendeleza zoezi la 'kufufua watu'
 
Du Wanapata shida sana na kifo cha mtukufu wanataka vyote alivyotaka mtukufu viendelezwe hata kama havina tija. Yeye mtukufu alivunja vunja vyote vya watangulizi wake na kuanza vyake ambavyo vilikuwa wala havufuati mpango wa taifa wa maendeleo wala CCM wala alichotaka kupeleka nchi nako hakujulikani. Rais wa sasa atafuataje kwenda kulingamiza Taifa la hasha nchi hii ni ya wote.
 
Back
Top Bottom