Askofu Gwajima: Tanzania inashindwa kuendelea mbele kutokana na kutokuwa na muendelezo wa utawala mmoja kwenda mwingine

Point ni njema ila kwa vile mama hatokei kanda fulani haruhusiwa kuasisi yale anayoyaona yanafaa katika uongozi wake,tuliwaambia mkatuona sisi yo wazalendo,mnaona sasa!
Hivi kwanini mnakaririshwa vibaya hivi unafikiri Gwajima ni iliterate kama wanaokutuma jaribuni kuchukua mawazo yanayojenga sio Gwajima amemshinda Mdee ndo imekuwa nongwa
 
Mimi huwa simkubali huyu jamaa lakini katika hili kaongea ukweli kabisa na hilo ndio tatizo letu. Tuchukulie mfano Dubai wao waliweka malengo wanataka kuwa number one kwa kila kitu hawataki number 2 kwa kila wanalofanya, kama ndege, airport, utalii na sijui bandari na mengi tu lakini sio kwamba ndio wamekuwa number one kwa kila kitu lakini hayo ndio malengo yao na kila mtu apiganie hayo. Sasa sisi kama Tanzania ni lazima tujiwekee vision je lipi tutakaloweza kututoa hapa na kutupeleka pale. Kama tunataka tuwe number one kwa kilimo Africa, tunataka tuwe nchi yenye elimu bora, afya bora na hii mifano tu basi iwe ni ilani ya kila chama iwe sharti mengine ya nyongeza kuboresha sawa tu lakini washindane sera za kutufikisha katika vision yetu. Naunga mkono hoja
Tangu Baba wa Taifa atatungazie kuwa kilimo ndiyo uti wa mgongo wa Taifa letu. Hakutaka kabisa kugusa madini. Kama kilimo kingewekewa mikakati ya kueleweka na kwa ardhi tuliyonayo tungekuwa tunalisha Afrika nzima kwa mazao mbalimbali.

Vyuo vya kilimo vingekua na short prommes za mafunzo kwa wakulima wanaofadhiliwa na vyama vyao vya ushirika.

Kila kijiji kingekua na nyumba na shamba la mfano ambalo wanafunzi wa vyuo vya kilimo wanakwenda field kwa miezi mitatu kufanya kazi na wananchi.

Maduka ya zana za kilimo kuleta za a za kisasa na wananchi kununua hata kwa mikopo.

Vyama vya ushirika kuendeshwa na wenye elimu kuanzia ya masoko, Fedha na public relations. Vijitafutie masomo nje ya nchi.
 
Gwajima kadata anahisi yupo madhabahuni ambapo ni ruksa kupitisha propaganda

Eti "tuwe na tafsiri yetu ya maendeleo" Kwanza sisi si tuliambiwa tupo uchumi wa kati?

Huo uchumi wa kati ulikuwa unakadiriwa kwa kuangalia itifaki zipi?

Tukiruhusu wanasiasa kama hawa 10 wawe wawakilishi wa wananchi huko bungeni basi nchi itakuwa iko mahala pabaya sana.

Anataka tuungane tukatae tafsiri ya maendeleo inayotambulika ulimwenguni kote halafu tutafute neno letu ambalo litakuwa linatufariji.

Hapo ni sawa na mwalimu anayeshindwa kufundisha wanafunzi wakafaulu akasema ili kuwa na idadi ya wafaulu wengi inatakiwa tuwe na tafsiri yetu ya ufaulu tusitumie tafsiri hii, hivyo kuanzia saizi kila atakayepata alama moja atahesabika kafaulu haijalishi hata kama yaliyobaki kakosa yote
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Hivi kwanini mnakaririshwa vibaya hivi unafikiri Gwajima ni iliterate kama wanaokutuma jaribuni kuchukua mawazo yanayojenga sio Gwajima amemshinda Mdee ndo imekuwa nongwa
Unaweza kuwa Literate kama Professor Lipumba,Palamagamba Kabudi,Gwajima na Ally Bashir wengineo lakini ujinga wa mawazo na upumbavu ukawa navyo kichwani
 
9we
Nimesikiliza , jamaa kaongea point kubwa tangu Bunge lianze, kila Raisi anakuja na mishe zake , anaharibu mfumo uliopo anaanza upya , mfano jiwe kaja kafumua fumua kila kitu , mfumo wa Elimu kafumua , mfumo wa biashara kaufmua ,mfumo wa utumishi kaharibu haribu huko na kabla hata hajaseti mambo akafa ....yaan mnarudi nyuma maili buku
Well said my friend!!!

Gwajima Josephat kaongea vyema kabisaaa, lakini given kwamba hoja yake ina lengo fulani lililojificha chini ya carpet kwa muda/kipindi hiki hiyo hoja yake hebu ikae pembeni tumuache Mh. Rais Samia Suluhu Hassan afanye yale anayoyaona yeye yanafaa kulifanyia Taifa kama walivyofanya watangulizi wake. Namuomba sana Gwajima aache kum-pre empty Rais wetu Samia.

Rais mstaafu Ally Hassan Mwinyi kipindi kileee alivyokwenda kumpongeza Hayati JPM kwa kazi nzuri anayoifanya alisema tumpe support JPM kwa yale anayoyafanya kwasababu kila zama na kitabu chake. Kwahiyo tumuache nae Rais Samia aandike kitabu chake kama walivyofanya watangulizi wake, tusimuingilie tafadhalini sana!!!

Halafu naomba nimkumbushe Gwajima Josephat kwamba kuwa na moja kitaifa ni wazo zuri lakini inategemeana na nyakati na majira pia. Kwa mfano, Kabla ya Mwl. Nyerere kugatuka mamlakani tulikuwa na mfumo wa chama kimoja lakini hali ikaja kubadilika na kuingia kwenye vyama vingi kutokana na nyakati.

Pia wakati wa Mwl. Nyerere tulikuwa na Public Enterprises lakini hiyo sera ikaja kubadilika kutokana na nyakati, tulikuwa na sera ya vijiji vya ujamaa lakkni ikaja kubadilika kutokana na nyakati.

Mwisho, hebu tumwache mama yetu Samia Suluhu Hassana tuone anatupeleka wapi kama tulivyowaacha watangulizi wake ukizingatia kuwa yeye amesema kipindi chake hiki ni awamu ya SITA.

Asante!
 
Ndo maana alkua anataka jpm atawale milele?

Akamfufue Basi arudi aendeleze, so uwa anajinadi anafufua watu.
 
Kawakilisha hoja nzuri, kabisaaaaaa! Taifa lisilo na dira ni sawa na jumba la uchunguzi wa mambo ya anga (observatory) lisilo na "telescope" (kiona mbali).
 
Sina shaka na uwezo wa kujieleza na ata kupambanua mambo wa Askofu Gwajima na leo nafikiri kaongea logic sana. Ni kweli kama Taifa tunapitia wakati mgumu sana mana kila Rais anayeingia anaanza moja na wakati huo tunakuwa tayari tuko mbele ila tunarudishwa kuanza upya.

Ni vema kuwa ata na vision ya miaka 30 na kila chama waingize hiyo ktk Ilani yao ili yyte anayeshinda akute tayari kuna mambo ambayo lazima ayakamilishe na lazima aanze nayo ktk kuyaendeleza pale alipoishia mtangulizi wake.

Ili tuweze kufanikiwa haya yote ni wazi tunahitaji katiba mpya ambayo pia itamuelekeza Rais kuangalia zaidi vision ili tuweze kufikia lengo.

Kongole sana kwa Askofu Gwajima, naamini ataendelea kujiweka tofauti na genge na wanafiki.
 
Mbunge wa Jimbo la Kawe Josephat Gwajima akitoa mchango kuhusu hotuba iliyotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema nchi nyingi za Kiafrika zimekuwa haziendelei kwa kasi ya maendeleo kutokana na kushindwa kutumia rasimali kwani inaendana na 'manpower'

Pia ameeleza kuwa Tanzania inashindwa kuendelea mbele kwa kasi kwasababu hakuna muendelezo wa Regime moja kwenda nyingine ambapo kila Rais anaingia madarakani na mipango yake hivyo huathiri maendeleo ya ukuaji wa mipango iliyoanzishwa.

Gwajima amtolea mfano Nyerere alietawala miaka 20 na kuacha viwanda 411, alipokuja Mwinyi aliboresha baadhi ya mambo lakini hakuendelea na wazo la viwanda na alipoingia Mkapa akauza vyote kwa kuvibinafsisha hivyo kukosa muunganiko kati ya 'regime' ya kwanza na regime ya tatu.

Gwajima amesema watakesha kama hamna huo muunganiko kwani hata Rais wa awamu ya nne hakushughulika na viwanda, bali mambo mengine lakini awamu ya tano akaamua kushughulika na viwanda, vilevile ambavyo awamu ya tatu ilivibinafsisha na kuviuza.

Gwajima amesema ni hatari kwasababu katiba inampa nafasi kila Rais anayeingia madarakani kwa namna yake, hekima yake na kwa namna anavyotafasiri yeye maendeleo.

Amesema siku moja atakapopatikana Rais ambaye hayuko sawasawa watu wataishia kulia na kutoa ombi la kuwa na vision ya kuwa na miaka 50 ya Taifa na anapoingia Rais lazima ilani ya chama chake izungumze mambo ambayo Taifa imejiwekea kama maono.

Gwajima amehoji endapo akatokea Rais ambae anafanya mambo yake yasiyo kwenye ilani kama kuna mtu wa kumuuliza mwenyekiti wa chama cha mapinduzi na Amiri Jeshi mkuu!

Gwajima anashindwa kutambua kwamba vision namba moja ya taifa ni katiba halafu hayo mengine yanafuata.

Gwajima anashindwa kutambua tatizo mama la nchi hii ni ccm na viongozi wengi wanafiki kama yeye utaendelea vipi kama taifa wakati viongozi hawapatikani kwa kura za wananchi bali kwa masanduku ya kura zakutengeneza stationary ?

Gwajima anashindwa kutambua kuwa awamu ya tano ndiyo awamu pekee iliyoharibu nchi kiasi cha kuondoa hata ustaarabu wa kawaida wa nchi na nchi kutawaliwa kishetani.

Pengine jibu pekee tunaloweza kupata kutoka kwenye hoja ya Gwajima ni kwamba na yeye amepata AQCQUIRED STUPIDITY
 
Ushabiki wa kijinga ndio shimo la maendeleo yetu

Tufanye Gwajima hatumpendi, Ila tuchukue alichokisema tukifanyie kazi haraka Sana

Kilichosemwa na Askofu Gwajima, ndilo haswaa hitaji la lazima la nchi yetu, haiwezekani mtu anakuja na dhima ya viwanda mwingine akija aseme, hivi viwanda ni vizuri Kwa kufugia kuku wa mayai tutapata faida Sana, huku ni kuzunguka mlima msijue kama mpo kwenye safari

Naunga mkono hotuba ya Askofu
Kweli kabisa mkuu, tuna shida kubwa sana ya kushindwa kuchukua mawazo ya mtu kwasababu aliyetoa mawazo tunamchukia.
 
naam Askofu amegusa penyewe. yani tunavyoenda ni sawa na timu ya mpira isiyokuwa na falsafa yake ya uchezaji (kwa wale wapenzi wa soka wananielewa hapa)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gwajima anashindwa kutambua kwamba vision namba moja ya taifa ni katiba halafu hayo mengine yanafuata.

Gwajima anashindwa kutambua tatizo mama la nchi hii ni ccm na viongozi wengi wanafiki kama yeye utaendelea vipi kama taifa wakati viongozi hawapatikani kwa kura za wananchi bali kwa masanduku ya kura zakutengeneza stationary ?

Gwajima anashindwa kutambua kuwa awamu ya tano ndiyo awamu pekee iliyoharibu nchi kiasi cha kuondoa hata ustaarabu wa kawaida wa nchi na nchi kutawaliwa kishetani.

Pengine jibu pekee tunaloweza kupata kutoka kwenye hoja ya Gwajima ni kwamba na yeye amepata AQCQUIRED STUPIDITY
Kweli mtu wa Mungu watu wabaya husahau kusimamia sheria mama(katiba ya nchi) Gwajima alitafakari hilo.
 
Mbunge wa Jimbo la Kawe Josephat Gwajima akitoa mchango kuhusu hotuba iliyotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema nchi nyingi za Kiafrika zimekuwa haziendelei kwa kasi ya maendeleo kutokana na kushindwa kutumia rasimali kwani inaendana na 'manpower'

Pia ameeleza kuwa Tanzania inashindwa kuendelea mbele kwa kasi kwasababu hakuna muendelezo wa Regime moja kwenda nyingine ambapo kila Rais anaingia madarakani na mipango yake hivyo huathiri maendeleo ya ukuaji wa mipango iliyoanzishwa.

Gwajima amtolea mfano Nyerere alietawala miaka 20 na kuacha viwanda 411, alipokuja Mwinyi aliboresha baadhi ya mambo lakini hakuendelea na wazo la viwanda na alipoingia Mkapa akauza vyote kwa kuvibinafsisha hivyo kukosa muunganiko kati ya 'regime' ya kwanza na regime ya tatu.

Gwajima amesema watakesha kama hamna huo muunganiko kwani hata Rais wa awamu ya nne hakushughulika na viwanda, bali mambo mengine lakini awamu ya tano akaamua kushughulika na viwanda, vilevile ambavyo awamu ya tatu ilivibinafsisha na kuviuza.

Gwajima amesema ni hatari kwasababu katiba inampa nafasi kila Rais anayeingia madarakani kwa namna yake, hekima yake na kwa namna anavyotafasiri yeye maendeleo.

Amesema siku moja atakapopatikana Rais ambaye hayuko sawasawa watu wataishia kulia na kutoa ombi la kuwa na vision ya kuwa na miaka 50 ya Taifa na anapoingia Rais lazima ilani ya chama chake izungumze mambo ambayo Taifa imejiwekea kama maono.

Gwajima amehoji endapo akatokea Rais ambae anafanya mambo yake yasiyo kwenye ilani kama kuna mtu wa kumuuliza mwenyekiti wa chama cha mapinduzi na Amiri Jeshi mkuu!

Imeandikwa wapi vilee! Labda kweli lkn pia huwezi kuwatumikia mabwana 2. Nikifikisha miaka 50 nafungua huduma yangu ya soda ya upako
 
Askofu Rashid ana point kidogo ... hasa kwa Tanzania ambayo imeongozwa na Chama Kimoja miaka yote. Kama kweli wanatekeleza Ilani ya CCM inakuwaje kunakuwa na tofauti za kimtazamo kati ya awamu na awamu?

Eti anadai Waislamu wenzau .... Askofu Rashid bwana......!!
 
Mbunge wa Jimbo la Kawe Josephat Gwajima akitoa mchango kuhusu hotuba iliyotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema nchi nyingi za Kiafrika zimekuwa haziendelei kwa kasi ya maendeleo kutokana na kushindwa kutumia rasimali kwani inaendana na 'manpower'

Pia ameeleza kuwa Tanzania inashindwa kuendelea mbele kwa kasi kwasababu hakuna muendelezo wa Regime moja kwenda nyingine ambapo kila Rais anaingia madarakani na mipango yake hivyo huathiri maendeleo ya ukuaji wa mipango iliyoanzishwa.

Gwajima amtolea mfano Nyerere alietawala miaka 20 na kuacha viwanda 411, alipokuja Mwinyi aliboresha baadhi ya mambo lakini hakuendelea na wazo la viwanda na alipoingia Mkapa akauza vyote kwa kuvibinafsisha hivyo kukosa muunganiko kati ya 'regime' ya kwanza na regime ya tatu.

Gwajima amesema watakesha kama hamna huo muunganiko kwani hata Rais wa awamu ya nne hakushughulika na viwanda, bali mambo mengine lakini awamu ya tano akaamua kushughulika na viwanda, vilevile ambavyo awamu ya tatu ilivibinafsisha na kuviuza.

Gwajima amesema ni hatari kwasababu katiba inampa nafasi kila Rais anayeingia madarakani kwa namna yake, hekima yake na kwa namna anavyotafasiri yeye maendeleo.

Amesema siku moja atakapopatikana Rais ambaye hayuko sawasawa watu wataishia kulia na kutoa ombi la kuwa na vision ya kuwa na miaka 50 ya Taifa na anapoingia Rais lazima ilani ya chama chake izungumze mambo ambayo Taifa imejiwekea kama maono.

Gwajima amehoji endapo akatokea Rais ambae anafanya mambo yake yasiyo kwenye ilani kama kuna mtu wa kumuuliza mwenyekiti wa chama cha mapinduzi na Amiri Jeshi mkuu!

Haya mambo angetakiwa aongee wakati JPM yupo kwenye power
 
Ushabiki wa kijinga ndio shimo la maendeleo yetu

Tufanye Gwajima hatumpendi, Ila tuchukue alichokisema tukifanyie kazi haraka Sana

Kilichosemwa na Askofu Gwajima, ndilo haswaa hitaji la lazima la nchi yetu, haiwezekani mtu anakuja na dhima ya viwanda mwingine akija aseme, hivi viwanda ni vizuri Kwa kufugia kuku wa mayai tutapata faida Sana, huku ni kuzunguka mlima msijue kama mpo kwenye safari

Naunga mkono hotuba ya Askofu
Tatizo ni bunge... Mpango wa taifa na Dira ya taifa ndio vipo haijalishi Rais gani kaingia.

Mawaziri wakidai bajeti wabunge wanapaswa kugoma yaliyomo kwenye mpango wa taifa, ilani, na dira ya taifa ndio yapitishwe.

Sasa ilani inasema katiba mpya afu Rais anaingia anadai sio ajenda yake..... Hapo ndio ilipaswa wabunge wakatae bajeti ya serikali yake mpaka aheshimu ilani yake. Sasa kma wabunge wanapiga makofi tu utamlaumu Rais?

Bunge ni dhaifu period
 
Back
Top Bottom