Askofu Gwajima, umekosea kujifanya mwamba na mwanaume, uwe mfano kwa jamii na heshimu familia yako. Uliyofanya na unayoyatetea si sahihi

Na mbona hamtaki kujibu hoja zake badala take mnataka akamatwe anyamazishwe tu kwa nguvu yaani. Why? Je ni yupi anayepotosha hapo? Kama mnajiamini mbona kuziba midomo wenzenu?
 
Kosa lake kwa sasa ni kushawishi wananchi wasichange huku hakuna mbadala . Pili ni personal attacks kwa waziri (shemeji) .

Ni kweli kuwa ndani ya muda mfupi serikali imekuwa na kauli zinazokinzana. Mwanzo wakiikataa Corona na chanjo zake. Lakini pili wakiikubali na chanjo zake. Hii imewachanganya wananchi . Na ndiyo maana wameifanya kuwa hiyari. Sasa Gwajima anatumia jukwaa lake la kanisa kuwarubuni wananchi si sawa. Lucas philipo
 
Tunajua Chadema mna hasira na askofu kwa sababu aliwashughulikia sana toka muonyeshe msimamo wenu wa corona. Mnataka tu akomolewe kwa hoja za kuuunga unga.
 
Askofu yuko sahihi na hata ukimsikiliza hoja zake kwa kina hajakataa chanjo ila anataka clarification ya kila anachoona hakiko sawa ukizingatia kipindi kifupi nyuma tuliambiwa corona hakuna tukashauriwa tule kachumbali za tangawizi na kupiga nyungu.
Mi nadhani suala la Askofu Ngwajima ni wake up call kwa viongozi na wataalamu wetu waache unafiki na kujipendekeza inapokuja masuala yenye maslahi mapana ya nchi bila kujali utaonekanaje mbele ya kiongozi mkubwa. Tukirudi nyuma wakati wa mwendazake Hawa viongozi na wataalamu hakuna aliyesimama akamwambia ukweli mwendazake wao wakawa wanasifu na kuabudu Sasa hivi ndio haohao wamegeuka Sasa wanapata wapi moral authority ya kutueleza tutumie njia za kitaalamu
 
Tunajua Chadema mna hasira na askofu kwa sababu aliwashughulikia sana toka muonyeshe msimamo wenu wa corona. Mnataka tu akomolewe kwa hoja za kuuunga unga.
Cdm imetoka wapi katika hoja hii ?!. Kwa kweli elimu yetu ni mbovu. Hapo kama ni mtihani si umepata zero !!.

Iliyo na dhamana na afya na majanga ya wananchi ni serikali si Gwajima na kanisa lake. So waziri kufuatia msimamo wa serikali ya awamu ya sita . Anayo haki ya kuhimiza watu wachanje . Sasa anapotokea mhuni kama Gwajima kushawishi watu wasichanje yeye ana mbadala gani huku Corona ikiendelea kuua watu ?!
 
Amekosa sifa za kuitwa Askofu.

Asome. 1 Timotheo 3:2 na Tito 1.7

Askofu anatakiwa awe mume wa mke mmoja, asisemwe kwa mambo mabaya, asiwe mtu wa hasira, asipende ugomvi, awe mwenye busara na kiasi.
Anayejiita Askofu Gwajima anakosea sana kugeuza nyumba ya ibada kuwa ukumbi wa mipasho. Huyu ajikite tu kwenye biashara ya kutengeneza zile video pendwa.
 
Hawawezi kumjibu
Hata wewe hapa hawawezi kukujibu.

Unapohoji unaonekana unapigana na mamlaka

Leo mtu anachanjwa bila kipima ufatiliaji wa mgonjwa hakuna.

Yote nikujipendekeza badala ya kuwajibika.
 
Sasa ndiyo ujue katiba ya Tanzania ni mbaya. Inamuumba mungumutu (Rais) . Ambaye kila mtu anataka ajipendekeze kwake.

Walijipendekeza kwa Jiwe huo na sasa wanajipendekeza kwa Mama
 
Kawaida ya askofu anapiga kimoja jumapili ila watu watahangaika wiki nzima kuchomoa ila hawawezi, jpili tena anapiga kingine! Hamumuwezi kabisa. Huu ni wakati wake.
Kakumwagia cha nguruwe eh!
 
Tunajua Chadema mna hasira na askofu kwa sababu aliwashughulikia sana toka muonyeshe msimamo wenu wa corona. Mnataka tu akomolewe kwa hoja za kuuunga unga.
Una maana Dorothy Gwajima na Job Ndungai ni wana Chadema?
 
Sasa ndiyo ujue katiba ya Tanzania ni mbaya. Inamuumba mungumutu (Rais) . Ambaye kila mtu anataka ajipendekeze kwake.

Walijipendekeza kwa Jiwe huo na sasa wanajipendekeza kwa Mama
Ndio tatizo hapo haijengi taasisi bora na imara zinazotoa majibu ya changamoto na hoja kuelekea maendeleo endelevu nakumbuka kuna dada daktari alitumbuliwa kwa kuonyesha msimamo wake wa kitaalamu watu walishangilia Sana kumbe yeye ndio alikua sahihi kuliko mwendazake. Katiba mpya ni muhimu katika kujenga taasisi imara, bora na zinazojitegemea bila kuadhiriwa na mawazo na mitazamo binafsi isiyo ya kitaalamu
 
Askofu uchwara huyu...anapiga miti wake za watu ( Flora Mbasha), anatapeli ( aliwahi mrubuni mama mmoja akampa kiwanja kinondoni, mume wake akampeleka mahakamani), anapiga miti waumini na warembo, anadanganya watu kuwa anafufua watu ( Amina Chifupa)..Ni mwingi.. alidanganyaga kuwa ameishaagiza treni..Tapeli mkubwa!
 

Mada kuu hapa ni kumhusu Gwajima; si chanjo.

Kwa kifupi kabisa, awe sahihi au la, HE IS NOT SMART.

Amejiweka kwenye kundi la watumishi wa Kristo. Iwe kwa ukweli au ubabaishaji. Genuine or fake. Basi na aenende kwa mwenendo wa Watumishi. Sio kwa jazba na kauli za ovyo ovyo ili kutafuta ushindi mitaani.

He should communiate his ideas and views in a manner befitting his (purported) status.
 
Ukifuatilia maisha binafsi ya askofu utapata tabu sana, na unaweza kukuta kuna maaskofu ambao wewe unawaamini sana kwa utakatifu ukifunuliwa mambo yao ya sirini unaweza kuzimia, fuata wanachofundisha siyo wanachotenda. Hata Yesu alisema " Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa, fuatisheni yale wanayoyanena lakini msifuatishe mienendo yao au matendo yao" yaani hapa mafarisayo walikuwa wanafundisha watu kuhusu torati ya Musa, lakini wao wenyewe maisha waliyokuwa wanaishi yalikuwa hayaakisi kile wanachofundisha....
 
Ninaowashangaa zaidi ni hao wanaokubali kuhubiriwa na Gwajima. Kwa vigezo vyote, na kwa namna yoyote ile, haiwezekani kabisa kuwa Gwajima anafanya kazi ya Mungu. Ni tapeli kwa kutumia neno la Mungu.

Lakini Mungu hadhihakiwi. Gwajima anaweza kuona amefanikiwa kwa kuwahadaa watu lakini inakuja siku, kwa wakati ufaao, Mungu atamwonesha kuwa japo anatuhurumia sote kwa dhambi zetu, lakini siyo katika kulitumia jina lake katika kufanikisha uovu wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…