#COVID19 Askofu Gwajima: Wapo waliochanjwa chanjo feki ili kuwashawishi watu wachanjwe. Sijachanjwa na haitatokea

Siku hizi Gwajima hasemi tena kua corona imeletwa na Network ya 5G?

🤣🤣🤣🤣
 
Kwa hiyo huyu anasema waziwazi kuwa viongozi wa serikali WAFEEE halafu yupo tu anadunda mtaani dakika hii.

Huu mchezo wao nitauelezea kesho vizuri.
 
Je hizo CHANJO unazozitaja unasaini CONSENT form? Kwamba ukichoma kitachokutokea serikali haiwajibiki ni juu yako au huoni hata hao serikali wana mashaka nayo?
 
Kumfukuza haitasaidia. Aidha kuwe na mdahalo wa wazi ambapo wataalam wa afya wajibu hoja zake hadharani na alete uthibitisho wa madai yake.
Itasaidia ndani ya chama chetu.....

Atabaki nje aendeleze misimamo yake.....

Tumeshafukuza wengi tu huko nyuma ilitusaidia.,. ..

#CCMImfukuzeGwajima
#KaziIendelee
 
Je hizo CHANJO unazozitaja unasaini CONSENT form? Kwamba ukichoma kitachokutokea serikali haiwajibiki ni juu yako au huoni hata hao serikali wana mashaka nayo? View attachment 1874757
Hujawahi kuwa na mgonjwa wa kufanyiwa upasuaji eeee?!!!!

Nako Kuna CONSENT FORM ya kujaza.....mbona ile huulizi?!!!!

#ChanjoNiBoraKulikoTiba
 
Ooops, mbona ume hoji kitu cha ajabu Mkuu?.
 
17th March,2021
Character ya true prophet ni pamoja na kusimamia unachoamini ni sahihi hata kwa gharama ya maisha yako... Wale wengine wanacheza mziki kadiri ya mdundo wa bi mkubwa.
 
Ndiyo maana nazipenda mno 'Systems' za Israel, China,Urusi, Korea Kaskazini, Ufaransa, Rwanda na Uganda kwani Wapuuzi kama huyu hivi sasa wangeshakuwa 'Historia' nchini Kwao.
 
Lazima tutambue tuna maanisha nini pale inapotokea suala kuwa ni hiyari, yaani mtu hafungwi na masharti yoyote yale katika kutekeleza. Neno hili hutumika likiwa ni kinyume cha suala kutendeka kuwa ni lazima, yaani mtu huwajibika kutenda kwa kufungwa na masharti yanayoelekeza.

Suala hili la chanjo ya UVIKO 19, kwa hali ilivyokuwa sasa, ni jambo la hiyari kwa hiyo ni lazima itokee mijadala inayokinzana kuhusu matumizi yake. Wale wenye kuzikubali pasipo kuwa na shaka yoyote juu yake wapo sawa, vilevile wale wenye kutilia mashaka chanjo hizo nao wapo pia sawa kihoja na kimantiki.

Natambua pande hizi mbili kinzani juu ya chanjo, hazina ugomvi wowote juu ya tafadhari nyingine za kiafya zinazopaswa kuchukuliwa ili kukabiliana na gonjwa hili, bali mgogoro mkubwa wa kimtazamo upo katika uharaka wa matumizi ya chanjo husika.

Ni jambo la kufikirisha sana pale viongozi wa kiroho wanapo himiza ama kuonya kwa nguvu sana kuhusu kitu fulani. Tunatambua viongozi wa serikali na wataalamu wa afya maamuzi yao hujikita katika mambo ambayo yapo yumkini na yanathibishwa kwa kanuni za kisayansi na njia za kimaabara.

Binafsi natambua viongozi wa kiroho huishi kwa kicho mbele ya Mungu kwa sababu wanatambua nyakati tulizopo sasa zinatupeleka katika utimilifu wa unabii wa siku za mwisho. Ni jambo la kuogofya sana kiroho endapo mtu utajikuta upo katika anguko kuu endapo utajikuta unakiuka tahadhari inayotolewa na malaika wa tatu kama vile ambavyo tunapata nukuu ifuatayo;

Ufunuo 14:9-11

Na malaika wa tatu aliwafuata hao wawili akisema kwa sauti kubwa, “Yeyote anayemwabudu yule mnyama na sanamu yake na kukubali kutiwa alama yake juu ya paji la uso wake au juu ya mkono wake, yeye mwenyewe atakunywa divai ya ghadhabu ya Mungu ambayo imemiminwa katika kikombe cha ghadhabu yake bila kuchanganywa na maji. Mtu huyo atateseka ndani ya moto wa madini ya kiberiti mbele ya malaika watakatifu na mbele ya Mwanakondoo. Moshi wa moto unaowatesa hupanda juu milele na milele. Watu hao waliomwabudu huyo mnyama na sanamu yake na kutiwa alama ya jina lake, hawatakuwa na nafuu yoyote usiku na mchana.”

Wakati mikakati motomoto ikifanyika kuelekea NWO, ni vyema tukawasikiliza pia viongozi wa kiroho. Maandiko matakatifu yanapotuambia kuhusu sauti ya malaika, hutaweza kumuona malaika yoyote yule akipaza sauti yake, bali huo ni ujumbe wa injili kwa wakati husika. Kaa chonjo na simama imara pale usikiapo ujumbe wa injili ukikuonya juu ya jambo fulani.
 
Character ya true prophet ni pamoja na kusimamia unachoamini ni sahihi hata kwa gharama ya maisha yako... Wale wengine wanacheza mziki kadiri ya mdundo wa bi mkubwa.
Subiri uone.
Hii kitu itamla.
 
Co
Comedian! Kama hao anaotaka wafariki si wakifariki wanaenda kwa Mungu? Shida iko wapi na nani atakayeishi milele?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…