Askofu Ikongo: Walioniteka, kunivalisha kitambaa cha sumu nawafahamu

Askofu Ikongo: Walioniteka, kunivalisha kitambaa cha sumu nawafahamu

UHUSIANO KATI YA SIASA ZA TANZANIA NA DINI-PART1

Kwa Muda mrefu Kumekuwepo na Wanasiasa Uchwara wasiojua Maana ya Siasa na dini na kudanganya Umma Kwa Kuwaita Viongozi wa dini wanaoongelea mambo ya Siasa kuwa wanachanganya Dini na siasa.Upepo Huo umeshakaa Akili Mwa watu wengi wasielema maana na Kuona Kana kwamba Haipaswi Viongozi wa dini au wanasiasa kuchanganya vitu hivi viwili.

Na Wanasiasa hawa hasa watawala Wamekeua wakunukuu Kabisa Maandiko ya Biblia MARKO 12:17 Kuwa YA KAISARI MPENI KAISARI NA YA MUNGU MPENI MUNGU.Wanasiasa hawa watawala wasiojua hata maandiko wanatafsiri Kuwa Hayo ya Kaisari ndio Mambo ya Siasa ambayo Mungu anataka ikiwa tunayafanya Hayo basi Tusichanganye na Mambo ya Mungu.Hivyo kwa Msingi huo wanaona Ni ajabu Viongozi wa Dini wanapokuwa wanazungumzia Mambo ya kisiasa.Na imeshakuwa Desturi Kushangaa kabisa wanapoona hata Mtu wa kawaida anapohusianisha Mambo ya kidini au ya Mungu na Siasa

Hii ni Dhana Potofu ambayo ndiyo nataka niiondoe Akili mwa Watanzania wanaorubuniwa na wanasiasa sio tu wasiojua Biblia bali Wanasiasa au watawala wasiopenda Kugushwa au Kukosolewa na Viongozi wa Dini.

KAZI YA VIONGOZI WA DINI KWENYE TAIFA/NCHI

Kwanza kabisa Ni makosa Kuhukumu Viongozi wa dini Kujihusisha na Siasa kama huelewi kazi za Viongozi wa Dini katika Mpango wa Mungu.Wengi kwa kutokuelewa Wanafikili Kazi ya Viongozi wa dini Ni kuhubiri tu habari za Neno na kuwakataza watu Kuacha matendo maovu Makanisani au Misikitini.Jambo ambalo si kweli kuwa kazi yao ni hiyo tu. Kazi Nyingneyo Ya Viongozi wa Dini ni
• Kuhakikisha jamii husika inakuwa na maisha bora na kuleta Ustawi katika Nchi

• Kuonya na Kukemea Watawala(Wanasiasa) pale wanapofanya matendo kinyume na haki za Raia

• Kutetea Wanyonge au Maskini pale wanaponyimwa Haki zao na Watawala wanasiasa

Viongozi wa Kidini wana sehemu kubwa sana ya katika mambo ya maendeleo ya Jamii yoyote na Pia Ndio wanaweza kuleta hatari kubwa ikiwa hatutajua umuhimu wao na Kuwapuuza kuwashirikisha katika mambo yanayohusu Maamuzi ya Umma kwa kudhani watakuwa wanachanganya dini na Siasa

Tangu zamani tawala Nyingi zilitambua Umuhimu na Mchango wa Viongozi wa Kidini katika Serikali zao(Tawala Zao) na hasa Sehemu Nyingi Viongozi wa kidini ndio walikuwa wanakuwa ndio washauri Wakubwa wa Wanasiasa(Watawala) au Sehemu Nyingine hasa Wao ndio walikuwa Watawala wa Nchi hizo.Sehemu Nyingi ambazo zimekubali Wanasiasa wamekubali kupokea Ushauri kutoka kwa Viongozi wa Dini tangu zamani nchi hizo zilikuwa na mafankia makubwa sana.Kwani hata Maandiko yanasema MWENYE HAKI ATAWALAPO WATU HUFURAI {MITHALI 29:2}

Unaporuhusu Wenye haki,Viongozi wa Dini kushiriki kushauri katika maswala yanayohusu utawala kwa Umma ,Maneno ya Mungu yanaeleza Ndipo watu hufurahi .Lakini pale tunapofika hatua hatutaki kabisa hata Ushauri au Kuona Mambo ya Utawala ya Kisiasa yakielezewa au kukemewa na Viongozi wa Dini kuwa ni Kuchanganya dini na siasa tunakuwa tunakosea sana na Tunashindwa hata Kuelewa kuwa Upo Uhusiano Mkubwa sana kati ya Siasa na Dini na hauwezi kuvitofautisha
Ili tusiendelee Kuchanganya haya mambo mawili kati Dini na siasa ni Vyema labda tukapata maana sahihi za maneno ndipo nitakuonyesha kwa Undani Uhusiano wa Dini na Siasa

MAANA YA SIASA

Neno Siasa(Politics) Katika CAMBRIDGE DICTIONARY Inatafsli kuwa

 Politcs-the activities of the government, members of law-making organizations, or people who try to influence the way a country is governed:

 the study of the ways in which a country is governed:

 someone's opinions about how a country should be governed

Hizi ndio maana halisi ya Siasa inazungumzia Mawazo ya Mtu,kuhusiana namna Nchi inavyotakiwa kutawaliwa au kuongozwa,Pia inaeleza ni Shughuli ambayo Mtu anajarbu kushawishi jinsi ambavyo nchi iinatakiwa kuongozwa au kutawaliwa.Kwa Ujumla Unapozungumza Siasa unazungumzia Mambo ya utawala .Siasa ni njia ya kufanya maamuzi ya umma katika mji, au nchi au duniani haijalishi kwa maslahi ya umma huo au kwa maslahi ya watu wachache.

Hivyo ni kukosa Ufahamu kusema kuwa Eti viongozi wa dini au Mtu ambaye ni Raia wa Tanzania kutoa mawazo yake Kuhusu namna bora ya nchi inavyopaswa kuongozwa au kutawaliwa eti anachanganya dini na Siasa.Kulingana na katiba ya Nchi yetu Kila Raia ana huru wa kutoa mawazo yake kuhusu maswala yanayohusu Utawala wan chi husika.Mafuta yakipanda Bei inawaathiri hata hao Vongozi wa dini!!Kwahiyo unataka wasizungumze!Jambo lolote liliyumba katika nchi lnamuathir kila raia akiwemo huyo kiongozi wa dini,Hakuna Bei za mafuta za Viongoz wa Dini.

Kwakuwa masuala mengi yanayohusu umma kama vile ya afya, ajira, elimu, na mengi ya kufananayo yanahitaji maamuzi ya umma, na kwakuwa siasa ndio njia ya kufanya hayo maamuzi ya umma, hivyo basi mambo yote yanahouhusu umma hutawaliwa na siasa. Kwa hivyo napata uhalali wa kusema kuwa siasa ndio kila kitu kwa mustakabali wa umma na katu mwanadamu hawezi kujitenga na siasa midhali yungali ni sehemu ya umma.Hivyo wanapotokea Vongozi wa Serikali na Kukataza siasa hadi 2020 Kwa kuzuia Vyama vya siasa kufanya Mikutano ya kisiasa,Napata shida na Viongozi wao ni wazi wanahitaji Shule hii ili wajue namna ya kuiongoza Nchi iweze kuwa na maendeleo.Ukiondoa Siasa katika jamii hakuna maendeleo popote duniani yaliyoletwa bila siasa.

Kutokana na kuwepo na aina mbovu ya Vongozi wabaya (Watawala waovu,wabaya) wasioelewa hata maana ya siasa na kujua ina umuhimu gani katika jamii ndio wefanikiwa kupotosha Umma na kuwafanya watu wengi Kusema “SIASA NI MCHEZO MCHAFU” na wengine Utawasikia “SIASA NI UONGO TU”.Siasa si mchezo mchafu wala si uongo bali hao ni watawala waovu au watawala wabaya Ndio wanapotosha Umma na kupelekea kutopokea Ushauri kwa Wenye Haki,Viongozi wa Dini katka mambo yanayohusu Taifa eti kwa kuhofia watakuwa wanachanganya dini na siasa(MITHALI29:2)

Sababu kuwepo kwa dini katika jamii ni kuhakikisha hiyo jamii inakuwa na maisha bora. Kwa vyovyote vile suala la maisha bora kwa jamii linahitaji maamuzi ya umma juu ya mambo kadhaa ambayo kwayo umma utaona kuwa yataleta maisha bora endapo yakifanywa. Kwakuwa dini inataka jamii iwe na maisha bora, na kwakuwa suala la maisha bora linahitaji maamuzi ya umma, hivyo basi dini hulazimika kuikiingia kwenye siasa aidha ikiwa nzima au kidogo

UHUSIANO WA DINI NA SIASA ZA TANZANIA

Pamoja na Kuwa Taifa letu linajinasibu kuwa si Taifa la Kidini wala halina dini na sina maana kuwa Nataka Taifa liongoze kwa Udini bali watu wake ni watu wenye Dini.Na dini Kubwa hapa Nchini ni UKRISTO na UISLAM. Kwakuwa siasa za taifa lolote huathiriwa na utamaduni wake, na kwakuwa dini kimaumbile ina tabia ya kujiingiza kwenye siasa, hivyo basi hata hapa nchini siasa zake huathiriwa na dini zenye idadi kubwa ya watu katika namna ya kuyakumbatia yale yanayoziunganisha hizo dini na kuheshimu yale yanayozitofautisha hizo dini. Kwakuwa asilimia kubwa ya watu katika umma wana dini, hivyo ni lazima maamuzi ya umma yaathiriwe na dini hata kiukweli hizo dini zinatafautiana.

Mfano sikukuu ya IDDI ni ya waislamu, iweje serikali isiyokuwa na dini ikaweka siku ya sikuu hii iwe mapumziko? Pia sikukuu ya CHRISTMASS ni ya kikristo, pia iweje siku hii serikali ikaifanya ni ya mpumziko? Maamuzi ya serikali kufanya siku hizi kuwa za mapumziko yameshinikizwa na dini hizo. Kwakuwa kwa mujibu wa ukristo sikukuu ya iddi si halali, kwakuwa kwa mujibu wa uislamu sikuu ya CHRISTMASS si halali, na kwakuwa siasa imezifanya siku za kusheherekea sikukuu hizi ni mapumziko, hivyo basi naweza kusema kuwa dini zimeingilia siasa za Tanzania katika namna ya kuvumiliana.

Niseme jambo moja kuwa dini ya kikristo na kiislamu hapa Tanzania zimejiingiza kidogo katika siasa, kama nilivyosema hapo awali kuwa, pamoja na mambo mengine, lengo la kuanzishwa dini ni kuleta maisha bora kwa jamii, na kwakuwa maisha bora ya jamii huhitaji maamuzi ya umma juu ya mambo kadhaa ambayo kwayo umma unaona pindi yakifanywa maisha yatakuwa bora, hivyo basi dini zetu nazo hujiingiza katika siasa kwa minajili ya kuharakisha harakati za kuleta maisha bora.
Matamko ya maaskofu, mashekhe, wachungaji, maimamu na viongozi wa kidini juu ya ufisadi , mauaji yanayofanywa na watu wasiojulikana na uvunjaji wa sheria unaofanywa na serikali ni kishiria cha dini hizi kutaka kuathiri njia ya maamuzi ya umma[Siasa]. Hivyo tunaweza kusema kuwa dini inaingilia siasa kwa kiasi fulani kwa lengo kutaka umma upate maisha bora. Si vibaya hata kidogo kwa dini kuathiri siasa za nchi katika muktadha huu.

Katika nchi iso dini kama yetu ni heri na ni vema kwa kiwango kikubwa kwa dini kujiingiza katika siasa kwa lengo na dhumuni la kuleta maisha bora kwa umma, lakini ni hatari kwa siasa kuacha kutazama maslahi ya umma badala yake ikajikita katika kutii na kutimiza matakwa ya dini moja tu katika namna ya kubagua dini nyingine. Kama tulivyoona katika nchi za kiislamu au kikristo ni sawa kwa siasa kutii matakwa ya dini moja ambayo kimsingi asilimia kubwa ya watu katika nchi hiyo ni waumini wa dini hiyo.


@Mamdenyi uko sahihi kabisa. Huwa nawashangaa wanaokimbilia Agano la Kale kuhalalisha kanisa kujihusisha na siasa za dunia. Wanachukua mfumo wa taifa la Israeli ya kale wanajaribu kuuoanisha na serikali za sasa.

Yesu Kristo hakuwahi kuwa na ugonvi na "serikali" badala yake maadui zake namba moja walikuwa watu wa "dini." Pilato alijaribu kumfungua awe huru, watu wa dini walisema nini?

Sio sawa kuhubiri siasa badala ya habari za ufalme wa Mungu. Yohana Mbatizaji hakufungwa kwa sababu za kisiasa bali baki za binadamu. Sababu za haki za binadamu kwa kumkemea Herode kupora mke wa ndugu yake, hilo nalo ni siasa? Tafakari
 
Waambieni hao viongozi wa kanisa waachane na siasa.

Biblia gani hizo wanasoma?

Mi nimesoma Bible ya king James, nimesoma lost books from the bible, ninasoma wisdom of Solomon (apocrapha) sijaona vikimchanganya Mungu na politics.
Kusoma na kuelewa ulichokisoma ni vitu viwili tofauti, huwezi kutenganisha dini na siasa. Vyote vinahusu mwanadamu yuleyule
 
Yawezekana huwa unasoma biblia ukiwa period ndiyo maana huoni siasa kwenye dini.

Mbona matukio ya kitaifa mnawaalika kuja kupiga sala kwanini mchanganye siasa na dini.

Watumishi wa Mungu wasio kemea udhalimu kwa kisingizio kuwa dini haitakiwi kuchanganya na siasa ni sawa na mtumishi wa shetani

Unataka watumishi wafumbie macho udhalimu wa awamu ya tano ???
Hapo umedhalilisha utu wa mwanamke, huna mama wala dada wewe? Huwezi kuchangia mada kwa hoja bila matusi? Hiyo period ndio heshima ya mwanamke acha matusi kwa mama na dada zetu &*¥₩# wewe [emoji35][emoji35]
 
Hiyo Biblia uliyosoma haikuwa na habari za Eliya Mtishibi? Hivyo vi Lost books vyako havijamgusia Yohana Mbatizaji hadi alipokatwa kichwa na Mfalme Herode?
Kifupi Eliya unajua kilichomkuta mpaka aliamua kuacha kazi ya unabii kwa jinsi alivyowindwa na mke wa mfalme jezeebel kuuawa,Akasema Mungu basi sitaki JEZEEBELI ANAWINDA KUNIUA SITAKI TENA HII KAZI

Yohana mbatizaji sawa alimkemea herode lakini kwa gharama ya kichwa chake alikatwa shingo!!!!!

Kifupi kiongozi wa dini toka zamani ruksa kuchanganya dini na siasa NA KUKEMEA viongozi wa kisiasa lakini kwa gharama ya kichwa chake

Kiongozi wa dini kuacha madhabahu na kwenda kukemea wanasiasa walioko madarakani ni ya kwake ili mradi awe tayari kichwa chake kukiweka machinjioni

Tumeona hadi uganda tu hapo ASKOFU WA ANGLICAN Janan LUWUM aliacha madhabahu akaenda kukemea mwanasiasa IDD AMIN hakuchukua round akauawa

Ushauri wangu dini na siasa ni vizuri viwe mbali kila mtu ahangaikie eneo lake lakini sikuzuii ili mradi uwe tayari kwa lolote kama wewe ni kiongozi wa dini
 
Waambieni hao viongozi wa kanisa waachane na siasa.

Biblia gani hizo wanasoma?

Mi nimesoma Bible ya king James, nimesoma lost books from the bible, ninasoma wisdom of Solomon (apocrapha) sijaona vikimchanganya Mungu na politics.
Biblia yote inazungumzia ufalme. Biblia na Korani ni vitabu vya kuimarisha haki duniani.
Hivyo watawala wote wanapaswa kumtii Mungu kuliko vitu vyote. Tukiwa na watawala waliopo juu ya ufalme wa Mungu ni hatari sana.

Soma kitabu cha Samweli,Waamuzi, Amosi n.k. vinaongelea siasa tupu.
Dini inakua mbaya kwenye siasa ikiwa inahamasisha kubagua dini nyingine au kabila lakini dini kupinga Sera za vyama na utendaji mbaya wa watawala ni halali kabisa na ndio kusudi halisi la dini.

Kama dini inakaa kimya wanasiasa wanaokesha kwenye Bar na uzinzi huku wakiiba rasilimali za umma na kujilimbikizia Mali huku wananchi wakiishi maisha ya umaskini mkubwa na maendeleo duni basi dini hiyo haina umuhimu wowote na dini hiyo ni tawi la utawala wa Shetani na sio utawala wa Mungu.

Kasome Tena Bibilia na Quran ukiwa umejinyenyekesha mbele za Mungu na sio ukiwa umekaa bar.
 
Basi unasoma halafu huelewi. Ungekuwa unaelewa ungeelewa kwa nini Yeremia alifungwa, nani alihusika kumchagua Saul na kumtengua, nani alimteua Daud... Ungefahamu Ugomvi wa Yesu na Utawala wa Kirumi, kwa nini Yohana mbatizaji alikatwa kichwa. Yapo mengi unafahamu Yohana Mbatizaji alikemea nini?

Siasa ipo sana katika Biblia labda kama huelewi. unamfaham Esther alifanya nini pale Mordekai alipotaka kuwatowesha watu wake?

Wewe hufahamu Siasa ndo maana unaona kama hakuna Siasa. Biblia ina Siasa sana na ina watumishi wengu ambao wamehusika na siasa.

Ukweli mtupu mkuu, naomba kukusahihisha kidogo ni Hamani aliyetaka kuwatowesha Mordekai na watu wake.
 
Nakuheshimu lakini usipotoshe wasiosoma Biblia wakadhani ni kitabu kinachofumbia mamcho uovu wa viongozi.
Kasome kitabu cha Daniel, Kasome mambo ya Nyakati, Kasome Matendo ya Mitume.
Mnakaririshwa hapo Lumumba mnakuja kuharisha huku JF mkijifanya mnajua Biblia?
Kwa taarifa yako Biblia nzima imejaa simulizi za watu wa Mungu wakikemea maovu ya viongozi hadi wengine wakauawa. Hiyo Biblia uliyosoma haikuwa na habari za Eliya Mtishibi? Hivyo vi Lost books vyako havijamgusia Yohana Mbatizaji hadi alipokatwa kichwa na Mfalme Herode? Katika soma yako hujawahi kusikia habari ya mashahidi wa Uganda na Mfalme Kabaka? Au neno Mfalme linakudanganya unadhani siyo wanasiasa? Mbona walikuwa na Baraza la Mawaziri hadi Mariwali? Kama unaamini kitabu tofauti na Biblia kaa kimya, Biblia huijui.
Wewe liongo kabisa. Hizo serikali / falme zilitawala kwa misingi ya dini na si kweli walikua kama sisi.
 
Waambieni hao viongozi wa kanisa waachane na siasa.

Biblia gani hizo wanasoma?

Mi nimesoma Bible ya king James, nimesoma lost books from the bible, ninasoma wisdom of Solomon (apocrapha) sijaona vikimchanganya Mungu na politics.
Hivi unajua kuwa hukumu ya Yesu ilikuwa ni ya Ki Siasa na unajua kuwa Yesu alikuwa Mpinzani, Literally ?
Unajua Pilato alikuwa nani ?
Hujaelewa Biblia wewe umesoisoma kama Novel tu.
Halafu Viongozi wa Dini kusifia inakuwa poa,wakikosoa mnasema wanachanganya dini na Siasa
Ila Jiwe kupenda kwenda kwenye nyumba za Ibada kupanda Mimbarini na kuongea ,kufanya Siasa kwenu sawa.
Jaribuni kutumia akili alizowapa Mungu na sio kutumia Matumbo na Makalio
 
Basi unasoma halafu huelewi. Ungekuwa unaelewa ungeelewa kwa nini Yeremia alifungwa, nani alihusika kumchagua Saul na kumtengua, nani alimteua Daud... Ungefahamu Ugomvi wa Yesu na Utawala wa Kirumi, kwa nini Yohana mbatizaji alikatwa kichwa. Yapo mengi unafahamu Yohana Mbatizaji alikemea nini?

Siasa ipo sana katika Biblia labda kama huelewi. unamfaham Esther alifanya nini pale Harmani alipotaka kuwatowesha watu wake?

Wewe hufahamu Siasa ndo maana unaona kama hakuna Siasa. Biblia ina Siasa sana na ina watumishi wengi ambao wamehusika na siasa.

Nabii Isaya alienda kumwambia Sauli mwanasiasa kuwa Mungu amemkataa.. hiyo haikuwa Siasa?

Hao wanasiasa kwa nini wanaapishwa na viongozi wa Dini au wanatumia Biblia na Quran kuapa? Hiyo siyo kuchanganya Dini na Siasa?
Barikiwa sana Mtumishi
 
Mene mene tekeri na peresi ni Ujumbe uliotolewa na Mungu kwa Askofu au nani? Daniel ni kwanini alitupwa kwenye Tundu la Simba?

Eliya alijuwa anapambana na Akina nani? Mpaka kufikia hatua kutafutwa na majeshi? Akina Paulo na Sira nini kiliwafanya watupwe Gerezani?

Kwa nini mnataka kumwacha Shetani awawekee wigo ili aendelee kuwakandamiza? Mfalme Hezekiah aliambiwa nini na Mungu naye akafanya maombi kuomba Mungu abatilishe alichomwambia?

Mtakuwa vipofu mpaka lini? Je ufahamu wenu utashikiliwa na shetani haya Mauti? Naaama mauti ya mwili na upotofu wa roho. Je mmemkabidhi shetani aendeshe maisha yenu na shughuli zenu mkitegemea kuneemeka kiroho na kimwili?

@Mamdenyi uko sahihi kabisa. Huwa nawashangaa wanaokimbilia Agano la Kale kuhalalisha kanisa kujihusisha na siasa za dunia. Wanachukua mfumo wa taifa la Israeli ya kale wanajaribu kuuoanisha na serikali za sasa.

Yesu Kristo hakuwahi kuwa na ugonvi na "serikali" badala yake maadui zake namba moja walikuwa watu wa "dini." Pilato alijaribu kumfungua awe huru, watu wa dini walisema nini?

Sio sawa kuhubiri siasa badala ya habari za ufalme wa Mungu. Yohana Mbatizaji hakufungwa kwa sababu za kisiasa bali baki za binadamu. Sababu za haki za binadamu kwa kumkemea Herode kupora mke wa ndugu yake, hilo nalo ni siasa? Tafakari
 
Kwani waliomtesa yesu nakumtundika msalabani nakisha kumuua walikuwa kinanani? Sio walikuwa watawala, farao alipambana na mussa alikuwa Nani? Lakini kubwa hapa nikuwa viongozi wa dini wanaongoza watu wakihubiri amani,upendo je, wanasiasa hawayapendi haya? Na siasa ni Nini? Sio mfumo wa maisha yawatu he, Mungu alipomaliza kazi yake kuiandaa dunia hakugawa mamlaka? Ninani aliambiwa aitawale dunia navitu vyote? Au nyinyi niwale wafuasi wamalaika mkuu aliyemuasi Mungu kwakupinga maelekezo yake? siasa ipo tangu ilipoumbwa dunia tu,,
 
Waambieni hao viongozi wa kanisa waachane na siasa.

Biblia gani hizo wanasoma?

Mi nimesoma Bible ya king James, nimesoma lost books from the bible, ninasoma wisdom of Solomon (apocrapha) sijaona vikimchanganya Mungu na politics.

Ulichosoma labda ni biblia iliyotungwa mtaa wa lumumba. Lakini Biblia sahihi ina reference nyingi tu ambapo watumishi wa Mungu Jehovah waliwaonya na wakati mwingine kuwakaripia watawala walipofanya uovu. Bwana Yesu mwenyewe alimkemea Herode mtawala wa Kirumi (of course biblia yako ya lumumba haiwezi kuwa na mstari huu)

Soma Luka 13:31
"Saa ile ile Mafarisayo kadha wa kadha walimwendea, wakamwambia, Toka hapa, uende mahali pengine, kwa sababu Herode anataka kukuua. 32Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilika."
 
Hapo umedhalilisha utu wa mwanamke, huna mama wala dada wewe? Huwezi kuchangia mada kwa hoja bila matusi? Hiyo period ndio heshima ya mwanamke acha matusi kwa mama na dada zetu &*¥₩# wewe [emoji35][emoji35]
Sasa kama Period ni Heshima kwa Mwanamke kuna tatizo gani pale juu kwa Jamaa kutoa heshima kwa Kumwambia huyo Mwanamke amechangia Akiwa Period ?
 
Back
Top Bottom