Basi unasoma halafu huelewi. Ungekuwa unaelewa ungeelewa kwa nini Yeremia alifungwa, nani alihusika kumchagua Saul na kumtengua, nani alimteua Daud... Ungefahamu Ugomvi wa Yesu na Utawala wa Kirumi, kwa nini Yohana mbatizaji alikatwa kichwa. Yapo mengi unafahamu Yohana Mbatizaji alikemea nini?
Siasa ipo sana katika Biblia labda kama huelewi. unamfaham Esther alifanya nini pale Harmani alipotaka kuwatowesha watu wake?
Wewe hufahamu Siasa ndo maana unaona kama hakuna Siasa. Biblia ina Siasa sana na ina watumishi wengi ambao wamehusika na siasa.
Nabii Isaya alienda kumwambia Sauli mwanasiasa kuwa Mungu amemkataa.. hiyo haikuwa Siasa?
Hao wanasiasa kwa nini wanaapishwa na viongozi wa Dini au wanatumia Biblia na Quran kuapa? Hiyo siyo kuchanganya Dini na Siasa?