Nijibu swali hili: Daniel alifungwa kwa kumkosoa mfalme kuhusu mambo ya kisiasa? Weka sababu yake kuwekwa jela na hata kwenye tundu la simba. Usiwe muumini wa kulishwa maneno wakati maandiko yako mbele yako. Nasubiri.
Onyesha kwamba Eliya alikuwa mjumbe wa kisiasa wa mfalme Ahab. Pia jiulize kulikuwa na imani ngapi katika Israeli nyakati za Agano la Kale. Je, kulikuwa na wanahai, waislamu, wahindu n.k? Au labda Eliya alitafutwa kwa sababu za kisiasa?
Kwani Paulo na Sila waliwalifungwa kwa sababu zipi hasa? Mifano yako yote ni mfu. Washtaki wao walikuwa ni mafarisayo, watu wa dini. Sasa tueleze hapa, siasa waliyokemea iko wapi kwenye maandiko. Nasisitiza usitaje majina Tu, fafanua visa halisi.
Tofautisha nyakati. Wakati wa Hezekiah taifa la Israeli kulikuwa likimtumikia Mungu mmoja Tu. Naye alikuwa mfalme wao kama taifa. Taifa lilikuwa la KIFALME wala sio la kidemokrasia kama mlivyo sasa. Mfalme alipaswa kuchukua maongozi moja kwa moja toka kwa Mungu, lakini leo hata asiye amini Mwenyezi Mungu aweza kuwa rais. Ndio maana kuna nanna nyingi ya kuapa, sio lazima kutumia biblia. Kumbe leo hii tuna mfumo tofauti kabisa.
We ndiye kipofu wa kiroho, hujui hata kama Kristo alisema utawala wake si wa dunia hii. Sasa walio wake wanaijua sauti yake. Wasio wake wanakwenda tu wakijihesabu ni wa dunia hii, wasijue kwamba ufalme wake si wa dunia hii. Ni vipofu wasiojua kusudi la kuitea kwao, hivyo kusombwa naupepo wa dunia.