masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,207
- 13,839
Askofu Mengele -katikati na Askofu Mwikali aliyesimama walipoita waandishi wa habari wakijieleza.
Askofu Mengele amefunga safari kwenda Mbeya kumpa tafu Askofu mwenziwe Askofu Mwaikali ambaye ana tuhuma zinazo muweka katika sintofahamu na kondoo wake.
Kitendo cha kupeana tafu kati ya hawa maaskofu hakina afya wala baraka za waumini wa sehemu hii, haswa wale wa kutoka Tukuyu, sehemu ambay Askofu Mwaikali ameinyanyapaa kwa kuhama.
Ikumbukwe kuwa Askofu Mwaikali amekosa heshima kutoka kwa waumini wake kwa vile amehamisha Makao Makuu ya Dayosisi ya Konde kwa ujanja ujanja, kitu ambacho wachungaji na waumini wa kutoka makao makuu yaliyohamwa wamepinga vikali.
Inasemekana kitendo cha Askofu Mwaikali kina hisia ya ubadhirifu, hila na matakwa binafsi.
Wachungaji zaidi ya 25 wametimuliwa kazi na huyu Askofu Mwaikali ati kwa kupinga maamuzi yake ya kuhama Tukuyu.
Waumini katika majimbo mbalimbali huko Rungwe wamepinga hatua za Askofu Mwaikali, na wachungaji aliowafukuza wanaendelea na huduma za kulisha kondoo katika makanisa yao.
Hivi karibuni Askofu Mwaikali alisusiwa ibada na waumini pale Tukuyu, na katika msiba wa mchungaji mmoja aliyefariki karibuni huko huko Tukuyu, wachungaji wote hata wale waliofukuzwa walihudhuria misa ya kumwombea mchungaji huyo. Na tamko lililotolewa ni kwamba Askofu Mwaikali hatakiwi kwenda huko.
Huu sasa ni mparaganyiko na kutengana kwa Dayosisi ya Konde rasmi.