Mpaka uwe unaijua biblia vizuri ndio utaelewa vizuri haya mambo.
Agano jipya Mungu amenunua wanadamu wa kila lugha,jamaa ili wawe makuhani na wafalme kwa kila amwaminiye kristo
Ufunuo 5:9-10
9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.
12 wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.