Askofu Josephat Mwingira awataka waumini kuvua barakoa

Askofu Josephat Mwingira awataka waumini kuvua barakoa

Huyu ngonja impate ndo atajua umuhimu wa barakoa.

Halafu hivi Mungu anapatikana kwenye buildings zao tu? Eti utasemaje na Mungu. Mungu nasema nae kiroho tena popote pale including nyumbani kwangu.
 
Kwani binadamu tunaongea na Mungu kwa mdomo?

Halafu na huyu ana watu nyuma yake. Yesu mwenyewe alisema waabuduo wataabudu katika Roho na kweli na si kwa mdomo.

Jamani lazima tulijue neno la Mungu na tuwe na kawaida ya kumsikiliza Roho mtakatifu anasemaje na wewe lakini sio mwanadamu. Naamini kama ulikuja na barakoa na ulijisikia una amani tu kuingia nayo kanisani ni Mungu ameruhusu hilo.

Ndio maana hakuna mtu anakaa mlangoni mwa kanisa na kuzuia watu kuingia na kofia au wakivuta sigara ni kwa sababu kuna kuhukumiwa kuwa sio sawa kuingia na kofia kichwani kanisani. Inakuwaje unamruhusu huyu amzuie Roho aliyekuruhusu uingie na barakoa?

Hakika tutakufa kwa uzembe na ujinga kwani Corona haiangalii kama wewe ni wa Kiroho sana au mpagani - wamekufa makasisi, maaskofu na watu tuliojua kuwa no watakatifu. Kikwete alisema za kuambiwa changanya na zako.
 
Back
Top Bottom