Askofu Josephat Mwingira awataka waumini kuvua barakoa

Askofu Josephat Mwingira awataka waumini kuvua barakoa

Corona imeleta siyo shida ya kimwili tu kwa binaadam lakini pia imetuonyesha udhaifu mkubwa kwa hawa watu wa Mungu, yaani hata common sense tu hawana na hii ndo inatupa picha kama jamii nzima kwanini tupo kama tulivyo kuanzia ujinga na umasikini wetu, poor us


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Da Mange anachanganyikiwa huko alipo, inamuuma sana, don know y?? Hahaha
 
Kibwetere ana afadhali.
Na hakuna atakachofanywa ..hili ndo la kusikitisha
Corona imeleta siyo shida ya kimwili tu kwa binaadam lakini pia imetuonyesha udhaifu mkubwa kwa hawa watu wa Mungu, yaani hata common sense tu hawana na hii ndo inatupa picha kama jamii nzima kwanini tupo kama tulivyo kuanzia ujinga na umasikini wetu, poor us


Sent from my iPhone using JamiiForums
Mpaka wasomi wetu
Unakuta mtu ana PhD Yuko kanisani Kwa mwingira
 
Hawa jamaa bana..
Wamesahau Mungu alimwambia Yosefu akimbilie Misri ili Yesu asiuawe na Herode? Kwani Mungu alishindwa kumficha huko Bethlehemu?
Wamesahau Mungu alimwambia Nuhu ajenge safina... Kwani hangeweza kufanya muujiza maji yasimdhuru Nuhu?

Hawa ndo wanafanya kazi za kutawanya kondoo. Kesho corona ikiingia pale kanisani hatabakia mtu.
 
Kwani binadamu tunaongea na Mungu kwa mdomo?

Halafu na huyu ana watu nyuma yake. Yesu mwenyewe alisema waabuduo wataabudu katika Roho na kweli na si kwa mdomo.

Jamani lazima tulijue neno la Mungu na tuwe na kawaida ya kumsikiliza Roho mtakatifu anasemaje na wewe lakini sio mwanadamu. Naamini kama ulikuja na barakoa na ulijisikia una amani tu kuingia nayo kanisani ni Mungu ameruhusu hilo.

Ndio maana hakuna mtu anakaa mlangoni mwa kanisa na kuzuia watu kuingia na kofia au wakivuta sigara ni kwa sababu kuna kuhukumiwa kuwa sio sawa kuingia na kofia kichwani kanisani. Inakuwaje unamruhusu huyu amzuie Roho aliyekuruhusu uingie na barakoa?

Hakika tutakufa kwa uzembe na ujinga kwani Corona haiangalii kama wewe ni wa Kiroho sana au mpagani - wamekufa makasisi, maaskofu na watu tuliojua kuwa no watakatifu. Kikwete alisema za kuambiwa changanya na zako.
Kuna sehemu umepotoka yawezekana umefundishwa vibaya kuhusu Imani . Corona imekuja kuwaumbua wale wote wenye imani haba, wawe waumini au wachungaji. Imefika hatua watu wameamini Mungu anaweza kuponya magonjwa fulani na mengine hawezi kitu ambacho si kweli.Kupitia Corona mwenye akili amejua kuwa uponyaji mwingi tunaouona kwenye Tv ni uongo na usanii mtupu.

Mungu alieumba vinavyoonekana na visivyoonekana hawezi shindwa kumuepusha au kumponya mtu na korona. Corona ni ugonjwa ulioletwa na shetani. Lakn kupitia Corona kuna watu tayari wamesha shetani ushindi.

Toka ugonjwa huu uanze hatujaskia mtu hata mmoja aliepona Corona kwa kuombewa. Manabii wengi hawathubutu kufanya hivyo maana wanajua Corona ni ugonjwa wa kweli kweli! Corona itaponywa tu na wachungaji wenye Imani thabiti isiyo na usanii ndani yake. Bahati mbaya it's hard to find.

Kwenda kanisani umevaa barakoa ni dalili za uoga na kukosa imani kwa Mungu.Ni heri ubaki nyumbani na barakoa yako. Watu wanapaswa kujua mbingu ni kwa ajili ya wenye Imani kubwa km ya Meshaki,Abeid na Shedrack. Au Daniel alietupwa kwenye shimo la Simba asiliwe. Km mtu hana imani ya namna hiyo basi huyo mbingu haimuhusu. Maelfu ya watu,mamia ya makanisa unayoyaona meengi ni bure. Watu wanasali tu km desturi lakini Mungu hayupo.


Hata Yesu angekuepo kimwili leo angewashangaa watu wanaoingia hekaluni kwenye nyumba ya Baba ake na barakoa. Nae angesema" Mbona mnamashaka mioyoni mwenu"?Mbaya zaidi wapo viongozi wa dini waliofunga makanisa kabsa ili kuikimbia Corona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu kama hawa kina Mwingira si wauaji wa halaiki? Why wanaachwa?


Kuna shida
Ni nini lakini ninyi wachungaji hewa?
Mnatimiza maagano yenu na mizimu yenu kuwaangamiza WaTz
Mungu analipiza kisasi mjue
Mungu ni wa hasira
Msiseme hatukuwaambia!
 
Huyu ngonja impate ndo atajua umuhimu wa barakoa.

Halafu hivi Mungu anapatikana kwenye buildings zao tu? Eti utasemaje na Mungu. Mungu nasema nae kiroho tena popote pale including nyumbani kwangu.
Kwani Barakoa ndio ina zuia Corona au maji tililika!!!..Kama Barakoa ingekua inazuia Corona nadhani wachina wasingepata huu ugonjwa kwasababu wachina wengi maisha Yao huvaa barakoa!!!...Barakoa ni Kinga ya hewa chafu lakini siyo kirusi hiki Cha Corona ndio maana tunaambiwa tuoshe mikono Mara kwa mara,tukae mbali kidogo,hebu tuwe na akili kidogo
 
Tip Tip------Maji maji
Tip Tip------Maji maji
Tip Tip------Maji maji
Kutahamaki, wameisha.
 
Ngoja wavue, uzuri korona inapenda wazee kama yeye atakua wa kwanza kuondoka, one less kilaza duniani
 
Back
Top Bottom