Nakubaliana na wewe sana mkuu. Huu ugonjwa unatuonyesha picha halisi ya jamii zetu, viongozi wetu na mifumo yetu ya kupambana na majanga ilivyo.
Hivi kweli katika kipindi kama hiki cha corona mtu anaweza kuongea upuuzi kama huo? Kwamba dunia nzima wataalamu waliosema watu wajikinge ni wajinga? Viongozi wetu including rais ni wajinga? Na mijitu imekaa inampigia makofi! Huyu mchungaji kwanza alitakiwa saa izi awe rumande kwa kuhatarisha maisha..!!
Kuna watu wanadhani kwamba virusi vinawafahamu au vitawaogopa kwavile wao ni manabii, au wachungaji, au wanasali kwa fulani, au wana nafasi fulani katika jamii. Virusi havijui hilo!! Na virusi ukishavipata, ni wewe na familia yako mtakaoteseka usifikiri saa hiyo upo mloganzila mchungaji atathubutu kukusogelea..