kibirizi wa kibirizi
Member
- Aug 11, 2018
- 11
- 9
Watu kama hawa kina Mwingira si wauaji wa halaiki? Why wanaachwa?
ndugu watanzania na watumishi wa Mung una waumini,chondechonde tuvisome vitabu vitakatifu tuvielewe na tufundishane njia sahihi yenye utukufu mbele za Mungu bila kuhitaji kuwa tofauti na wengine au kutafuta umaarufu.
Jana kuna sheikh mmoja tanga kawakataza waumini wake kwenda msikitini wakiwa wamepaka sanitizer kisa eti ni pombe wasiingize msikitini.
Katika quran kuna aya nyingi zinazoonyesha wakati wa hatari hata halamu huwa halali ili mradi uponye Maisha yako…ndugu zangu waisilam mnajua vyema aya hizi sitapenda kujikita huko maana kitabu hicho sikitumiii…
Nije kwa huyu mtumishi Mwingira anayetumia biblia kama mimi, kweli kuvaa barakoa ni kosa? Ni ukosefu wa Imani? Unashindwa kuongea na Mungu ukiwa umevaa barakoa? Mbona tunaongea na kusikilizana huku tumevaa barakoa? Mungu ana masikio yasiosikia mpaka sauti kubwa?
Mungu anasikia kwa kuangalia moyoni kwa kuangalia moyo wa mwombaji, je hili Mtumishi hulijui/halijui,….imeandikwa waabuduo halisi watamwabudu Mungu katika roho na kweli
Kuhusu kumjaribu Mungu, malaika alivyomtokea Joseph na kumwamuru akimbilie misri wakati Jesus bado kichanga ina maana Mungu alishindwa kumlinda na mkono wa Helode usimzuru? Ina maana Joseph angekaidi si angavuruga mpango wa Mungu? Mimi na wewe hatujui nini kingetokea maana waliuwawa Watoto wote……imeandikwa
Watumishi/waumini tuvitumie vitabu na roho sio akili zetu wenyewe tutapotea na Mungu atatuuliza kuwa tulikuwa na sababu ya kupotea sijui tutajibuje,.
Kama ni kauli ya Rais, sizani kama alimaanisha hivyo labda alieleweka tofauti…kuomba tuombe lakini vilevile tahadhali zichukuliwe tena kwa nguvu zote.
TUTUMIE AKILI MAANA NAZO ZIMEUMBWA KWA KAZI HIYO KWA NYAKATI HIZI.