LGE2024 Askofu Juda Ruwa'ichi atoa tamko kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa

LGE2024 Askofu Juda Ruwa'ichi atoa tamko kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Mwisho wa uhuni umefika boss, kama huamini tunza huu uzi hutaamini macho yako.
Hamna kitu , bado mbadala haupo........zaidi zitakuja kelele tu labda wakitunisha msuli wakodi vibaka waje kuvunja amani ila kwa humu ndani bado hamna wa kubadili uelekeo,,.....tena kama mnafikiria hizo njia za uongozi zilizoletwa na wazungu zitafua dafu basi mnajidanganya,,...........demokrasia ya huku ni ya kula na vipofu, mzungu karidhishwa tu ili pesa imiminike ila utawala wa huku unaeleweka
 
Gentleman,
I am always truthfully man,
nikiona neno la Mungu linawekwa kando, halafu Askofu au kasisi anaanza kumwaga sera za chama Fulani cha kisiasa, namuona ameshindwa kazi ya kupeleka waamini mbinguni...

Askofu unawachochea waamini wajichukulie sheria mkononi?

kasisi unasubiri unyumbu wa chama Fulani cha siasa kanisani?

sasa kuna haja gani ya kwenda kanisani wakati anachohubiri kiongozi wa kisiasa ndicho hicho hicho anahubiri kasisi?🐒
Yile mpuuzi msenzio alipo sema watao msema vibaya rais wapotezwe hukuona anawachochea wananchi sio!? Kweli wewe sufuri kichwan
 
Kwa mara kwanza naungana na kanisa katoliki kupinga huu udhalimu wa CCM.

Tufikirie kiuhalisia tu! Mtu anayekamata madaraka kwa njia ya kudhulumu haki ya mwingine atawezea wapi kuisimamia haki ya mwingine atakaposhika madaraka?

Ndo mana hii nchi saivi kila mtu ni mwizi na mdhulumati. Sababu ni haya maujinga ya kukumbatia Viongozi wanaoingia madarakani wa njia ya udanganyifu na dhuluma!
 
Halafu sijui ana mapengo, ila ni mchaga, wanachadema wengi wanatokea huko. Kitima yeye anamuunga mkono msingida mwenzake. Wakatoliki wakiona Rais muislamu wanakuwaga na midomo mirefu
Kwa hiyo maaskofu wote wa TEC ni Wasingida na Wachaga? Au ndo kujitoa tu ufahamu?

Mimi mwenyewe nimejitenga na CCM saivi kwa sababu siwezi ishi kwa dhuluma alafu kila siku naenda kanisani kusali.

Nchi hii kansa inayoitafuna ni CCM na yanayosemwa na hawa viongozi wa dini ni sahihi
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kuwaambia viongozi wa dini ya kwamba nchi hii haina dini, bali wananchi wake ndio wana dini. Literally meaning alikuwa anawaambia kuwa wasifikiri kuwa wao ni sehemu ya utawala wa nchi hii. Dini yeyote sio LAZIMA iwepo Tanzania, Tanzania inaweza kuwepo bila dini yoyote.

..THUBUTU!!
 
Kufanya mkutano ratiba ikiwa sio yake kuna kosa gani kama amekubaliwa na aliyekuwa na nafasi? Mbona tunaona magari ya serekali yakitumiwa na ccm na hatuoni polisi wakitumia nguvu kubwa kuwakamata makada wa ccm?
Wewe utakuwa mjinga,ratiba imewekwa ya nini? Ndio maana mumekatwa Kwa kutifuata kanuni zilizopo harafu mnakuja kuongea upuuzi huku mitandaoni na hao wanaowafariji na wasio na Msaada .

Kwanza hata Wafuasi wenu hawapigi kura eti wanajisemesha ooh kura zitaibiwa,Sasa hapo ndipo ccm wanafurahi na Huwa unaona wanahamasishanazkuoigiana simu na kuwasafieisha watu wao kuanzia kujiandikisha Hadi kupiga kura.

Nyie endeleeni na ujinga wenu wa mitandaoni mtakoma.Mnaleta siasa za Ulaya Africa?
 
Kama kuna taasisi ilikemea uovu wa magu ni hiyo RC. Usidhani hatukuona matamko yao wakati wa yule kiongozi muovu. Hilo tamko la maaskofu ni baadhi tu ya viashiria vya mwisho wa ccm. Kwasababu ccm wanafaidika na huu udhaifu wa katiba, ni lazima wamchukie kila anayeweka uhalifu wao hadharani. Maaakofu wameweka msimamo wao hadharani, wakati wa mahesabu mikono yao itakuwa safi.
Tena walipingana nae waziwazi kwenye Corona. Walimpa makavu kweli kuwa aache sayansi ifanye kazi
 
Wewe utakuwa mjinga,ratiba imewekwa ya nini? Ndio maana mumekatwa Kwa kutifuata kanuni zilizopo harafu mnakuja kuongea upuuzi huku mitandaoni na hao wanaowafariji na wasio na Msaada .

Kwanza hata Wafuasi wenu hawapigi kura eti wanajisemesha ooh kura zitaibiwa,Sasa hapo ndipo ccm wanafurahi na Huwa unaona wanahamasishanazkuoigiana simu na kuwasafieisha watu wao kuanzia kujiandikisha Hadi kupiga kura.

Nyie endeleeni na ujinga wenu wa mitandaoni mtakoma.Mnaleta siasa za Ulaya Africa?
Haya maneno ya kebehi ndugu yangu kuna siku utakuja kuyajutia. Ukweli usemwe, CCM imefikia mwisho maana kwa haya wanayoyafanya kwenye uchaguzi ni uchafu sio tena demokrasia
 
Kushinda kwa kishindo kwa uchaguzi wa kihuni ndio kishindo gani? Unashinda kwa kishindo kwa uchaguzi wa kupika idadi ya wapiga kura, na dosari za wazi?!
Ahahahahaha! Hao wanaolalamika CCM imepika matokeo wako wapi? Msumbiji watu wanaolalamika waziwazi. Hapa Tanzania wanaolalamika kupokea matokeo we umewaona? Ahahahahaha!! Ushindi wa kishindo unasubiriwa tena 2025!!! Ahahahahaha!!!
 
Gentleman,
dawa ya mchochezi ni kumpuuza tu kwa dharau inatosha.

Hata hivyo,
Nyumbu pamoja na ukurupukaji wake wote huishia mdomoni mwa simba au mamba na matokeo yake hasara anapata yeye mwenyewe, dah 🐒
Ogopa sana wingi wa hao unaowaita numbu. Yaani wewe unayejiona una akili ukiwa mmoja na unazungukwa na wapumbavu 1000, huna utakalofanikiwa.
 
Wakuu,

Askofu Mkuu Jimbo la Dar na Mwenyekiti wa Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Tanzania, Juda Thadeus Ruwa'ichi anatoa tamko sasa hivi kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa, Katika mkutano na Wanahabari unafanyika kwenye viunga vya 'Parokia ya Bikira Maria Mama wa Huruma Mji mpya Relini.


Askofu Ruwa'ichi ametaja baadhi ya mauaji ya wanasiasa na raia yaliyotokea hivi karibuni kuwa ni pamoja na yale yaliyotokea Novemba 26, 2024 huko Tunduma mkoani Songwe na Manyoni mkoani Singida sambamba na mauaji yaliyotokea jijini Dar es Salaam Novemba 27 mwaka huu, ambayo Kanisa hilo limetaja mauaji hayo yote kuwa ni ya kukusudia

"Mwanzoni mwa mwezi huu (Novemba 2024) kule Iringa na Bukoba waliuawa pia wanasiasa wawili (2), Tanzania tunaelekea wapi kwa kujenga tabia hii?, kitendo cha mauaji ya wanasiasa kinapaswa kulaaniwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria, hakuna mwenye mamlaka ya kumuuwa mwenzake, kutekeleza ama kudai haki za kisiasa wakati wa uchaguzi wakati wa uchaguzi sio vita ni ushindani"

Aidha, Kanisa Katoliki limesema tabia ya kuchukulia mauaji ya wanasiasa na raia kama vifo vya kawaida na vinavyopaswa kuzoeleka ni tendo baya sana linaloweza kupelekea kujengeka tabia ya kupoteza na kukosa ulinzi wa haki ya uhai kama ilivyo kwenye Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

"Wapo waliokabidhiwa jukumu la kulinda Ibara hii, tunapoona mauaji haya yakiongezeka tunajiuliza maswali mengi juu ya uwajibikaji wa serikali kwa wananchi"

Kuhusu mweendo wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa liofanyika Novemba 27

"Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana maeneo mbalimbali ya nchi yetu inaonekana kwamba uchaguzi wa Serikali za Mitaa umegubikwa na mapungufu mengi, ambayo wengi ninyi kama wanahabari mnayajua. Shughuli zito kama hii ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa inapoenda kiholela hatuipendi nchi yetu, hatuwatendei raia haki na hatushughulikii raia wote".

"Viongozi mbalimbali wa dini walitoa matamko kuhusu mwenendo wa maandalizi kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, matamko yale yalikuwa ni tahadhali tufanye hilo zoezi kwa hali inayokidhi. Ni zoezi (niliite takatifu) katika nchi yoyote, Uchaguzi halali na haki ni zoezi takatifu la kiraia, kwahiyo ni lazima lifanywe kwa uzito, uangalifu na uadilifu unaotakiwa"

"Nchi yetu ni ya Siasa ya vyama vingi, hata kama tunaweza kuelekea kuwa na ulemavu wakujihisi kwamba ni nchi ya chama kimoja lakini Tanzania ni nchi ya Vyama vingini na raia Mtanzania kuwa mshiriki wa chama chochote hiyo ni haki yake kiraia hakuna raia yoyote ambaye amezaliwa nakufungamanishwa na CCM, CHADEMA au CUF na vingine, hivyo vyama vyote ni machaguo au maamuzi ya raia mwenyewe na raia anapoamua kwamba anataka kujihusisha anapaswa kuheshimiwa. Watanzania tuendelee kujenga utayari wakuithamini nchi yetu, kuipigania nchi yetu na kupendana, kushikamana na kutendeana haki"

Tumetamka mara kadhaa kwamba inabidi tujipange, tujipange kutazama nyanja mbalimbali zinazohitaji maboresho au marekebisho katika mwenendo wa siasa za nchi yetu, hilo sio haki ya Wanasiasa ni haki ya raia wote kuwa na mpangilio na mwelekeo wa kisiasa ambao unatendea haki na unalinda usitawi na unapania maendeleo ya nchi yetu. Mtu yeyote mwenye nia njema na nchi yetu hawezi acha kulipigia kelele hili na yeyote anayeona tamko kama hili linawameng'enya ni vizuri wakajitadhimini.

CCM wao wamejizatiti kwa mapambano ya Aina yoyote ambayo yatawafanya waendelee kubaki Madarakani, swala la uchaguzi wao hilo kwa sasa hawana habari nalo kabisa wao kwa sasa ni mikakati tu ya jinsi ya kuwatawala watu kwa njia yoyote,Wapinzani pamoja na wananchi kwa ujumla hawana mikakati yoyote yakujinasua katika kongwa hilo kwani Wao wako makini sana na kila chipukizi linalo chipua kuhatalisha madaraka yao, wanahakikisha hakuna mtu yoyote anaye jaribu kuwaaamsha wenzake wanahakikisha wana anza naye kupambana naye Aidha kumpiga kiuchumi, kumbambikia kesi na ikiwenzekana kumpoteza. Hali hiyo imesababisha Hofu kwa kila mtu, siyo raia wakawaida, siyo hakimu, siyo wanasiasa, siyo POLISI wenyewe, siyo usalama wa Taifa, siyo wanaharakati, siyoViongozi wa Dini hofu inamkumba mpaka Rais mwenyewe, unadhani ni nani anayesababisha hofu, siyo mtu yoyote ila ni mifumo mibovu ya Taasisi zetu za kutoa uamuzi, Leo hii kwa mfano Spika anaweza akafanya kitendo kizuri tu kwa maslai ya nchi kesho akawa hayupo kazini, Jaji anaweza akaamua shauri liloletwa mezani kwake kwa haki kabisa kesho akawa hayupo kazini, chombo cha habari kinaweza kikahabarisha habari nzuri tu kwa manufaa ya Taifa kesho yake kikafungiwa, kwa kuwa nchi imejengwa katica Circle ya hofu kila mtu sasa anatazama utashi wa haliye juu yake, akiona jambo hili litamfurahisha bosi wangu ndiyo hicho anachofanya ilimradi alinde maslai yake, hapa tulipofikia siyo pazuri na kunasiku moja mtu mwenye madaraka ataamua kuvunja hii Circle ndiyo hapo patashika nguo chanika itakapotokea. Kwa sasa kila mmoja anamuogapa mwenzake kwakuwa hatuna taasisi imara za kulinda haki za watu. Mifumo yote imechezewa kiasi kupata haki yako mpaka kwa hisani ya Bosi fulani na hii ni kwa taasisi zote za uma. Tunaipeleka nchi kubaya sana. Kwa mfano ukienda magerezani kuna watu wapo huko wana miaka zaidi ya kumi kisi zao wala hazisikilizwi na wengine rufaa zao zimekwama sehemu wasizo ua wala hawajui watumie njia gani kuzikwamua, Hii yote ni kwa mifumo ya taasisi yetu inategemea utashi wa watu siyo utashi wa kitaasisi. Ila nitoe rai zangu watu wale wale, wanaokwenda kwa mifumo ileile kwa njia zilezile hawataweza kutatua haya matatizo, kwa sababu wao wanafaidika na hii hali, sasa ni nini cha kufanya, Hata mimi sijui. Kwakuwa hawa watu huwa wanawai kula kichwa cha mchungaji na kondoo wanatawanyika. Kama vile wapalestina wanavyo pambana miaka na miaka na israeli na maelfu wanauwawa, sidhani kama hizo njia ni sahihi. Bado tunanafasi kama wanachi kuboresha mifumo yetu ingawa itachukuwa mda mrefu lakini naamini ipo siku kila kitu kitakwenda vizuri ila si kwa urahisi. Mungu ibariki Tanzania.
 
Mwaka 2019 na 2020 baadhi ya vyama vilisusia uchaguzi. Kwanini mwaka huu wamekomaa kushiriki? Nijibu hili ili nijibu swali lako la msingi.
We utajuaje kama mi nilikua nchini? Jibu swali kwanza. Unaona sasa hata wewe nafsi inavyo kusuta?
 
Back
Top Bottom