Askofu Kassala atoa ‘Dikrii’ ya kufungwa kwa Kanisa Kuu la Kiaskofu Jimbo la Geita

Ujinga sana huu, yule Padri aliyebaka mtoto aliyekuja kuungama mbona halikufungwa? Ile kufuru ni kubwa zaidi sana ya hii
Ingekuwa ni mtihani, wewe ulistahili kupata 0! Maana hakuna uhusiano wa hiki ulichokiandika, na hilo tukio la kufungwa Kanisa.
 
Tena nyinyi mlionyimwa elimu ya duniani ndiyo kabisaaa! Hamtakiwi kuongea chochote. Maana mmekaa kishari shari tu.

Hilo tukio lingefanyika kwenye nyumba yenu ya ibada, muda huu mngekuwa mnalialia tu na kujilipua kwa mabomu.
Zoom hii picha utaona kilichofanya kanisa lifungwe
JamiiForums-1459547918.jpg
 
Kwa masikitiko makubwa na tumaini kubwa kwa Mungu, napenda kuwataarifu kwamba, huduma zote za ki-ibada na ki-Sakramenti katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Jimbo Katoliki la Geita zamesitishwa kuanzia leo tarehe 27 ya Mwezi Februari ya Mwaka wa Bwana 2023.

Uamuzi huu unafuatia tukio la KUFURU NA UNAJISI lililofanyika ndani ya Kanisa hili, ikiwa imafanyika pia Kufuru kubwa kwa Sakramenti ya Ekaristi Takatifu, na unajisi kwa utakatifu wa jengo hili la Kanisa na vifaa mbalimbali vya Ibada Takatifu.

Kwa Dikrii hii, Mimi Flavian Matindi Kassala, ambaye kwa Neema ya Mungu na Mamlaka ya Kiti cha Kitume ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita, na ambaye Sahihi yangu nimeiweka hapo chini, na kwa mamlaka ninayopewa na Sheria Kanuni ya Kanisa (Rejea Na 1211-1213), na kwa maelekezo ya Mamlaka ya Kiaskofu, (Rejea Ceremonial of Bishop namba 1070-1072) napenda kutamka kwamba:

  1. Uharifu uliotokea katika Kanisa Kuu la Jimbo la Geita usiku wa kuamkia tarehe 26 Februari 2023 NI KUFURU KUBWA kwa Sakramenti ya Ekaristi Takatifu na umeivunjia Sakramenti ya Ekaristi Takatifu Heshima yake kwa kiasi kikubwa sana na hivyo umeathiri.
  2. Uharifu uliotokea katika Kanisa Kuu la Jimbo la Geita usiku wa kuamkia tarehe 26 Februari 2023 UMELINAJISI Kanisa hili katika utakatifu wake uliowekwa wakati wa Kutabarukiwa kwake.
  3. Uharifu uliotokea katika Kanisa Kuu la Jimbo la Geita usiku wa kuamkia tarehe 26 Februari 2023 ni UHARIFU MKUBWA SANA ambao umeiathiri kwa kiasi kikubwa sana hadhi na Muumini Mkatoliki na Jamii yetu kwa ujumla.
Kutokana na matukio hayo, Kanisa hili limepoteza kwa kiasi kikubwa Baraka yake na jamii ya Waamini imeumizwa sana kutokana na Kashfa, Kufuru, na Unajisi uliofanyika kwa Imani yetu. Na hivyo ninaagiza kwamba:

  1. Kanisa Kuu la Kiaskofu la Jimbo Katoliki la Geita halistahili kwa maadhimisho ya Sakramenti ya Ekaristi, wala ya Sakramenti yoyote, wala kwa ibada yoyote.
  2. Kufuatia hali hii, Kanisa Kuu la Kiaskofu la Geita litabaki limefungwa kwa huduma zote za Ki-Ibada kuanzia tarehe 27 Februari 2023 hadi tarehe 18 Machi 2023, ili kusubiri Utakaso wake.
  3. Kwa kipindi hicho cha kufungwa kwa Kanisa, Familia nzima ya Mungu Jimboni Geita inaingia katika kipindi cha siku 20 za kuelekea adhimisho la TOBA YA MALIPIZI (Penitential Reparation) kuanzia tarehe 27 Februari 2023 hadi tarehe 18 Machi 2023.
  4. Kwa kipindi chote cha kuelekea Toba ya Malipizi Mapadre waandae na kuwaandaa Waamini katika Jimbo zika kwa Ibada za Upatanisho, mahubiri ya Toba, na Mafundisho juu ya Utakatifu wa Kanisa na kuyatoa daima kwa waamini wao ndani ya maadhimisho mbali mbali.
  5. Kwa kipindi chote cha kuelekea Toba ya Malipizi waamini wote Wakatoliki wanaalikwa kusali, kufunga, kutubu, kupokea Sakramenti ya Upatanisho na kuomba huruma ya Mungu. Katika Matendo yote haya tuombe Mungu atujalie wongofu wa ndani.
  6. Kanisa Kuu la Jimbo litafunguliwa tarehe 18 Machi 2023 kwa adhimisho ibada ya MISA TAKATIFU itakayoanza saa Nne asubuhi, na itakayohusisha pia maadhimisho ya: TOBA YA MALIPIZI; BARAKA KUTAKATIFUZA KANISA KUU; NA KURUDISHA EKARISTI TAKATIFU NDANI YA KANISA KUU.
  7. Adhimisho la tarehe 18 Machi 2023, litakuwa ni la Kijimbo, na hivyo Mapadre, Watawa, na Waamini wanawajibu wa kuhudhuria. Watu wote wenye mapenzi mema wanakaribishwa pia kushiriki katika maadhimisho yote haya.
Hali tukiyaweka haya yote mikononi kwa Huruma ya Mungu,
SERVUS MISERICORDIAE VULTUS

FLAVIAN MATINDI KASSALA
ASKOFU WA JIMBO KATOLIKI GEITA

Kuvamiwa kwa Kanisa, Soma: Kanisa Kuu la Kiaskofu Jimbo Katoliki la Geita limevamiwa usiku wa kuamkia February, 26 2023
Amen na Mungu asimame nanyi Waumini wote wa Kanisa Katoliki Geita na hasa wanaosali hapo Cathedral[emoji120][emoji120]
 
Wananchi wanachanga michango mingi kujenga:
1. shule ila watoto wao lazima walipe ada kubwa kusoma katika hiyo shule, mtoto wa masikini kama ana ada hawezi soma katika hiyo shule
2. waumini wanajenga hospitali ila muumini hawezi kwenda pale kwenye hospital kutibiwa bure na gharama za matibabu ni kubwa hatari.

Hawa jamaa wanafanya biashara ya kuuza matumaini kwa watu wakijinadi kwamba wanafanya kazi ya mungu. Imani zao hazina tofauti na imani zetu za kale ambazo watu waliomba mvua wakapata na kuomba neema wakabalikiwa.

Uzuri ni kwamba sisi waumini tunachangia na hatulalamiki.Na watoto wetu tunawapeleka kwenye hizo shule na School fees tunalipa kama kawaida.

Hospital tunakwenda nantunapatiwa huduma safi kabisa kwa malipo stahiki.

Tumsifu Yesu Kristu [emoji120][emoji4]
 
Tena nyinyi mlionyimwa elimu ya duniani ndiyo kabisaaa! Hamtakiwi kuongea chochote. Maana mmekaa kishari shari tu.

Hilo tukio lingefanyika kwenye nyumba yenu ya ibada, muda huu mngekuwa mnalialia tu na kujilipua kwa mabomu.
Niliwahi kushuhudia tukio walicharangana mapanga Msikitini kukageuka kuwa uwanja wa damu pale Mkolani Mwanza,watu watatu walikufa pale pale akiwemo Imamu wa msikiti.
 
ningewashauri hili swala lipo kiimani zaidi linagusa imani za watu na maumivu ya ndani ya watu hii si siasa au habari za kawaida bora mtuachie wakatoliki kwa kadri ya taratibu zetu.
Waache tu waendelee na upuuzi wao wa kukashfu,uzuri tumejaliwa sana na tumejengwa kwenye misingi ya kuvumilia mawimbi yote yenye kujaribu Imani yetu. Hapa kuna watu wengi maisha yamewavuruga na akili zao hazipo sawa.
 
Makanisa haya ni matatizo.
Kumbe makanisa yakivamiwa na sakramenti kuharibiwa ibada zinakufa?

Mmmh huyu Mungu anatuonaje?
Si imeandikwa tutamwabudu Mungu rohoni?
Hujui usemalo. Wapi aliposema ibada zisifanyike. Ibada zimezuiliwa kufanyika ndani ya Kanisa lililonajisiwa. Kuna makanisa mengine yanaendelea kutoa huduma. Soma vizuri alichokiandika usikurupuke.
 
Geita mji wa ajabu kuna shida huko matukio ya ajabu ajabu yanatokea huko.
 
Roma wako makini Sana na taratibu zao za kanisa wanazingatia Sana kanuni zao za imani.
 
Kwa masikitiko makubwa na tumaini kubwa kwa Mungu, napenda kuwataarifu kwamba, huduma zote za ki-ibada na ki-Sakramenti katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Jimbo Katoliki la Geita zamesitishwa kuanzia leo tarehe 27 ya Mwezi Februari ya Mwaka wa Bwana 2023.

Uamuzi huu unafuatia tukio la KUFURU NA UNAJISI lililofanyika ndani ya Kanisa hili, ikiwa imafanyika pia Kufuru kubwa kwa Sakramenti ya Ekaristi Takatifu, na unajisi kwa utakatifu wa jengo hili la Kanisa na vifaa mbalimbali vya Ibada Takatifu.

Kwa Dikrii hii, Mimi Flavian Matindi Kassala, ambaye kwa Neema ya Mungu na Mamlaka ya Kiti cha Kitume ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita, na ambaye Sahihi yangu nimeiweka hapo chini, na kwa mamlaka ninayopewa na Sheria Kanuni ya Kanisa (Rejea Na 1211-1213), na kwa maelekezo ya Mamlaka ya Kiaskofu, (Rejea Ceremonial of Bishop namba 1070-1072) napenda kutamka kwamba:

  1. Uharifu uliotokea katika Kanisa Kuu la Jimbo la Geita usiku wa kuamkia tarehe 26 Februari 2023 NI KUFURU KUBWA kwa Sakramenti ya Ekaristi Takatifu na umeivunjia Sakramenti ya Ekaristi Takatifu Heshima yake kwa kiasi kikubwa sana na hivyo umeathiri.
  2. Uharifu uliotokea katika Kanisa Kuu la Jimbo la Geita usiku wa kuamkia tarehe 26 Februari 2023 UMELINAJISI Kanisa hili katika utakatifu wake uliowekwa wakati wa Kutabarukiwa kwake.
  3. Uharifu uliotokea katika Kanisa Kuu la Jimbo la Geita usiku wa kuamkia tarehe 26 Februari 2023 ni UHARIFU MKUBWA SANA ambao umeiathiri kwa kiasi kikubwa sana hadhi na Muumini Mkatoliki na Jamii yetu kwa ujumla.
Kutokana na matukio hayo, Kanisa hili limepoteza kwa kiasi kikubwa Baraka yake na jamii ya Waamini imeumizwa sana kutokana na Kashfa, Kufuru, na Unajisi uliofanyika kwa Imani yetu. Na hivyo ninaagiza kwamba:

  1. Kanisa Kuu la Kiaskofu la Jimbo Katoliki la Geita halistahili kwa maadhimisho ya Sakramenti ya Ekaristi, wala ya Sakramenti yoyote, wala kwa ibada yoyote.
  2. Kufuatia hali hii, Kanisa Kuu la Kiaskofu la Geita litabaki limefungwa kwa huduma zote za Ki-Ibada kuanzia tarehe 27 Februari 2023 hadi tarehe 18 Machi 2023, ili kusubiri Utakaso wake.
  3. Kwa kipindi hicho cha kufungwa kwa Kanisa, Familia nzima ya Mungu Jimboni Geita inaingia katika kipindi cha siku 20 za kuelekea adhimisho la TOBA YA MALIPIZI (Penitential Reparation) kuanzia tarehe 27 Februari 2023 hadi tarehe 18 Machi 2023.
  4. Kwa kipindi chote cha kuelekea Toba ya Malipizi Mapadre waandae na kuwaandaa Waamini katika Jimbo zika kwa Ibada za Upatanisho, mahubiri ya Toba, na Mafundisho juu ya Utakatifu wa Kanisa na kuyatoa daima kwa waamini wao ndani ya maadhimisho mbali mbali.
  5. Kwa kipindi chote cha kuelekea Toba ya Malipizi waamini wote Wakatoliki wanaalikwa kusali, kufunga, kutubu, kupokea Sakramenti ya Upatanisho na kuomba huruma ya Mungu. Katika Matendo yote haya tuombe Mungu atujalie wongofu wa ndani.
  6. Kanisa Kuu la Jimbo litafunguliwa tarehe 18 Machi 2023 kwa adhimisho ibada ya MISA TAKATIFU itakayoanza saa Nne asubuhi, na itakayohusisha pia maadhimisho ya: TOBA YA MALIPIZI; BARAKA KUTAKATIFUZA KANISA KUU; NA KURUDISHA EKARISTI TAKATIFU NDANI YA KANISA KUU.
  7. Adhimisho la tarehe 18 Machi 2023, litakuwa ni la Kijimbo, na hivyo Mapadre, Watawa, na Waamini wanawajibu wa kuhudhuria. Watu wote wenye mapenzi mema wanakaribishwa pia kushiriki katika maadhimisho yote haya.
Hali tukiyaweka haya yote mikononi kwa Huruma ya Mungu,
SERVUS MISERICORDIAE VULTUS

FLAVIAN MATINDI KASSALA
ASKOFU WA JIMBO KATOLIKI GEITA

Kuvamiwa kwa Kanisa, Soma: Kanisa Kuu la Kiaskofu Jimbo Katoliki la Geita limevamiwa usiku wa kuamkia February, 26 2023
Katika hili la kufunga Kanisa, mimi mawazo yangu yanatofautiana kidogo na uamuzi aliouchukua Baba Askofu.

Assuming zilikuwa ni hujuma ambazo zililenga kudhoofisha Ibada Kanisani, na kwamba zinaweza kujirudia tena, je tutaendelea kufunga MaKanisa kwa muda hadi lini, kisa wezi? Kwa nini isiwe kwamba baada ya mwizi kuvamia, ndiyo iwe kichocheo cha Ibada kuongezeka zaidi kukemea uovu huo ili usije ukajirudia tena? Mara zote Kanisa la Mungu liko vitani na adui huwa hata siku moja hatoi nafasi ya kulifanya lipumzike; kwa nini tuvamiwe na adui halafu ndiyo wakati huo tusitishe mapigano?

Kwa vile ni mara ya kwanza, ni sawa Baba Askofu aendelee na uamuzi wake ila kama itakuja kutokea kwa mara nyingine, japo hatuombei hilo, ninamuomba sana Baba Askofu azidishe Ibada badala ya kufunga Kanisa
 
Hivi umesoma kwa umakini Kweli waraka huo?,Hivi Kufunga na Kufanya toba kwa siku 20 sio kusali?.
 
Mmmh Mambo yamekuwa yamoto,mashambulizi kila kona,kanisa limemuona kijana mwizi ila halijamuona Padri mlawiti. Wacha sisi tuendelee kuomba amani mashariki ya kati.
 
Back
Top Bottom