Askofu Kassala atoa ‘Dikrii’ ya kufungwa kwa Kanisa Kuu la Kiaskofu Jimbo la Geita

Askofu Kassala atoa ‘Dikrii’ ya kufungwa kwa Kanisa Kuu la Kiaskofu Jimbo la Geita

Katika hili la kufunga Kanisa, mimi mawazo yangu yanatofautiana kidogo na uamuzi aliouchukua Baba Askofu.

Assuming zilikuwa ni hujuma ambazo zililenga kudhoofisha Ibada Kanisani, na kwamba zinaweza kujirudia tena, je tutaendelea kufunga MaKanisa kwa muda hadi lini, kisa wezi? Kwa nini isiwe kwamba baada ya mwizi kuvamia, ndiyo iwe kichocheo cha Ibada kuongezeka zaidi kukemea uovu huo ili usije ukajirudia tena? Mara zote Kanisa la Mungu liko vitani na adui huwa hata siku moja hatoi nafasi ya kulifanya lipumzike; kwa nini tuvamiwe na adui halafu ndiyo wakati huo tusitishe mapigano?

Kwa vile ni mara ya kwanza, ni sawa Baba Askofu aendelee na uamuzi wake ila kama itakuja kutokea kwa mara nyingine, japo hatuombei hilo, ninamuomba sana Baba Askofu azidishe Ibada badala ya kufunga Kanisa
Jengo lililofungwa ni cathedral kama saint Joseph kwa Dar. Hapo hapo ilipo cathedral kuna makanisa (majengo mengine) au parokia jirani, kwa hiyo misa na ibada zote za kila siku zinafanyika kama kawaida. Ila lile jengo ndio (tuseme) linasafishwa au linatakaswa kwa muda huu.
 
Sakramenti ya Ekaristi Takatifu ni moyo wa Kanisa, Kwani ndiyo Mwili na Damu ya Yesu Kristu
Sijui wa RC mtakuwa na akili ya kumwabudu Mungu lini?
Ndio maana hamjui hata kufungua biblia zaidi ya mapokeo ya Kirumi na sheria za kanisa tu.

Haya endelea kutukana
 
Kwa masikitiko makubwa na tumaini kubwa kwa Mungu, napenda kuwataarifu kwamba, huduma zote za ki-ibada na ki-Sakramenti katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Jimbo Katoliki la Geita zamesitishwa kuanzia leo tarehe 27 ya Mwezi Februari ya Mwaka wa Bwana 2023.

Uamuzi huu unafuatia tukio la KUFURU NA UNAJISI lililofanyika ndani ya Kanisa hili, ikiwa imafanyika pia Kufuru kubwa kwa Sakramenti ya Ekaristi Takatifu, na unajisi kwa utakatifu wa jengo hili la Kanisa na vifaa mbalimbali vya Ibada Takatifu.

Kwa Dikrii hii, Mimi Flavian Matindi Kassala, ambaye kwa Neema ya Mungu na Mamlaka ya Kiti cha Kitume ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita, na ambaye Sahihi yangu nimeiweka hapo chini, na kwa mamlaka ninayopewa na Sheria Kanuni ya Kanisa (Rejea Na 1211-1213), na kwa maelekezo ya Mamlaka ya Kiaskofu, (Rejea Ceremonial of Bishop namba 1070-1072) napenda kutamka kwamba:

  1. Uharifu uliotokea katika Kanisa Kuu la Jimbo la Geita usiku wa kuamkia tarehe 26 Februari 2023 NI KUFURU KUBWA kwa Sakramenti ya Ekaristi Takatifu na umeivunjia Sakramenti ya Ekaristi Takatifu Heshima yake kwa kiasi kikubwa sana na hivyo umeathiri.
  2. Uharifu uliotokea katika Kanisa Kuu la Jimbo la Geita usiku wa kuamkia tarehe 26 Februari 2023 UMELINAJISI Kanisa hili katika utakatifu wake uliowekwa wakati wa Kutabarukiwa kwake.
  3. Uharifu uliotokea katika Kanisa Kuu la Jimbo la Geita usiku wa kuamkia tarehe 26 Februari 2023 ni UHARIFU MKUBWA SANA ambao umeiathiri kwa kiasi kikubwa sana hadhi na Muumini Mkatoliki na Jamii yetu kwa ujumla.
Kutokana na matukio hayo, Kanisa hili limepoteza kwa kiasi kikubwa Baraka yake na jamii ya Waamini imeumizwa sana kutokana na Kashfa, Kufuru, na Unajisi uliofanyika kwa Imani yetu. Na hivyo ninaagiza kwamba:

  1. Kanisa Kuu la Kiaskofu la Jimbo Katoliki la Geita halistahili kwa maadhimisho ya Sakramenti ya Ekaristi, wala ya Sakramenti yoyote, wala kwa ibada yoyote.
  2. Kufuatia hali hii, Kanisa Kuu la Kiaskofu la Geita litabaki limefungwa kwa huduma zote za Ki-Ibada kuanzia tarehe 27 Februari 2023 hadi tarehe 18 Machi 2023, ili kusubiri Utakaso wake.
  3. Kwa kipindi hicho cha kufungwa kwa Kanisa, Familia nzima ya Mungu Jimboni Geita inaingia katika kipindi cha siku 20 za kuelekea adhimisho la TOBA YA MALIPIZI (Penitential Reparation) kuanzia tarehe 27 Februari 2023 hadi tarehe 18 Machi 2023.
  4. Kwa kipindi chote cha kuelekea Toba ya Malipizi Mapadre waandae na kuwaandaa Waamini katika Jimbo zika kwa Ibada za Upatanisho, mahubiri ya Toba, na Mafundisho juu ya Utakatifu wa Kanisa na kuyatoa daima kwa waamini wao ndani ya maadhimisho mbali mbali.
  5. Kwa kipindi chote cha kuelekea Toba ya Malipizi waamini wote Wakatoliki wanaalikwa kusali, kufunga, kutubu, kupokea Sakramenti ya Upatanisho na kuomba huruma ya Mungu. Katika Matendo yote haya tuombe Mungu atujalie wongofu wa ndani.
  6. Kanisa Kuu la Jimbo litafunguliwa tarehe 18 Machi 2023 kwa adhimisho ibada ya MISA TAKATIFU itakayoanza saa Nne asubuhi, na itakayohusisha pia maadhimisho ya: TOBA YA MALIPIZI; BARAKA KUTAKATIFUZA KANISA KUU; NA KURUDISHA EKARISTI TAKATIFU NDANI YA KANISA KUU.
  7. Adhimisho la tarehe 18 Machi 2023, litakuwa ni la Kijimbo, na hivyo Mapadre, Watawa, na Waamini wanawajibu wa kuhudhuria. Watu wote wenye mapenzi mema wanakaribishwa pia kushiriki katika maadhimisho yote haya.
Hali tukiyaweka haya yote mikononi kwa Huruma ya Mungu,
SERVUS MISERICORDIAE VULTUS

FLAVIAN MATINDI KASSALA
ASKOFU WA JIMBO KATOLIKI GEITA



Kuvamiwa kwa Kanisa, Soma: Kanisa Kuu la Kiaskofu Jimbo Katoliki la Geita limevamiwa usiku wa kuamkia February, 26 2023
Uharibifu uliofanyila ni mkubwa sana
Hatujui mtekelezaji alitumwa au ni utashi wake.

Unamajisi vitu ambavyo vimewekwa wakfu ni kujitafutia balaa. Kama hutaki kuamini wanachokiamini watu wengine dawa ni kuachana nao wafanye yao na wewe fanya yako ilimuradi jauvunji sheria na amani baina yenu.

Ahojiwe mtuhumiwa nani yupo nyuma yake.

Mimi sinaga imani na Katoliki lakini tutaelezana kwenye hoja na si kutumia matendo kulazimisha hoja
 
Kwa wasiofahamu

Ekaristi ni mojawapo kati ya sakramenti saba za Kanisa ambazo ni alama wazi zilizowekwa na Yesu Kristo mwenyewe ili kutuletea neema ya wokovu. Tofauti na sakramenti zingine Ekaristi ni Kristo mwenyewe katika maumbo ya mkate na divai.

Ekaristi ni kitovu na kilele cha maisha ya Kanisa, kwa kuwa kwayo Kristo anachagamana na Kanisa lake na waamini wake wote na sadaka ya sifa na shukrani iliyotolewa mara moja Msalabani kwa Mungu Baba. Kwa sadaka hii anamimina neema za wokovu kwa mwili wake ambao ni Kanisa (KKK 1407). Ekaristi Takatifu ni roho ya Kanisa (Denz.3364). Ni Sakramenti ya umoja na upendo, kimsingi, Ekaristi ni kiini kamili katika Kanisa, na Kanisa haliwezi kitu pasipo hiyo. Kwasababu ni Kristo mwenyewe anayejitoa kweli kama sadaka kwa ajili ya Kanisa katika Ekaristi Takatifu na ni katika Ekaristi Kanisa hufikia uhalisia wake wa juu wa asili yake, yaani, kuwa linaonekana, la daima, na alama wazi ya neema ya wokovu ya Mungu iliyopo duniani kupitia Kristo.

Kumbe Ekaristi inaunda Kanisa na Kanisa linaitengeneza Ekaristi, na ndimo linamochota nguvu za kiroho.
.Hivyo hakuna jumuiya ya Kikristo inayoweza kujengwa na kusimama imara bila adhimisho la Sakramanti Kuu ya Ekaristi Takatifu (Presbyterorum Ordinis, n. 6). Katika Ekaristi Takatifu fumbo la Ukombozi wetu linawekwa hai na kufikia kilele katika sadaka ya Bwana, kama inavyotamkwa katika maneno ya konsekrasio: “huu ndio Mwili wangu utakaotolewa kwa ajili yenu na hii ndiyo Damu yangu itakayomwagika kwa ajili yenu”, “Fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi” (Luka 22:19-20).

Kwa haya machache nadhani mnapata picha ni jinsi gani unajisi na kufuru iliyofanyika ni mkubwa kiasi gani. Hivyo ili kuondoa najisi hiyo, Ni lazima toba zifanyike pasipo kutumia kanisa na vifaa hivyo vilivyotiwa najisi, Mpaka vitakapotakasika na kitabarukiwa tena.
 
Hivi hatuwezi kuwsomba Maaskofu wakafunga dikrii kwenye hazina yetu zinakoibiwa kodi zetu kuwanyoosha wahuni na wezi
 
shangaa sasa. jengo lipo watu wapo ,viongozi wapo ni kitu gani hicho kilichoharibiwa hadi ibada zisitishwe
kuna vi miungu huko vimejeruhiwa
ila jamaa ni mkatili, eti mlevi, mlevi akazima hadi cctv cameras
Vitu usivyovijua na havikuhusu visikupe headaches.Kazania yale unayoyapenda na kuyaamini.
 
Ni ibada tena kubwa mno; isipokuwa swali langu ni kwamba waumini wanakusanyikia wapi sasa?
Kwenye Parokia zao,wa Geita Ambao walikuwa wanasali Kanisa kuu wanaweza kutafutiwa alternative Nyingine,Mfano kutengenezewa ma-tent nje ya Kanisa lililofungwa au km Kuna ukumbi wanaweza kusalia humo.Siku 20 sio nyingi kihivyo.
 
Nashukuru sana ndugu mwerevu
Alichokueleza ndiyo sahihi.Kinachoelezwa ni mtu/watu kufanya uharibifu kanisani.Kunajisi vitu vya kanisa.Sasa huo ulawiti ulifanyikia kwenye mabenchi au altareni ndani ya kanisa?Jifunze kuelewa na kuoanisha mambo.
 
Hii ni sawa na itkafu tu malipizi sio mchezo dogo yule lazima afe au awe ndondocha na kupotea kusiko julikana

USSR
Hekima ya Mungu ituongoze tusifikie sisi kufanya conclusions ambazo Mungu hakusudii kuzifanya.

Hata akibadilika na kutubu kwa aliyoyafanya ni bora alimradi hilo lipate kibali kutoka kwa Mungu mwenyewe.
 
Mmmh Mambo yamekuwa yamoto,mashambulizi kila kona,kanisa limemuona kijana mwizi ila halijamuona Padri mlawiti. Wacha sisi tuendelee kuomba amani mashariki ya kati.
Haya matukio mawili umeyafuatilia kwa umakini na ukaribu?

Huyo padre mlawiti ulipata habari kwamba alishasimamishwa na Kanisa ikaachiwa serikali ku-deal nae kama ambavyo inge-deal na mimi au na wewe kama tungekuwa tumetenda jinai?
 
Back
Top Bottom