Askofu Kilaini achemsha kwa ushauri huu!

Loo!! mtu akitaja tu Kanisa Katoliki unaguswa kweli na kuja juu ile mbaya. Badilisha jina basi..

Vyovyote utakavyoona ndio ivoivo..Mimi naona nachangia hoja ila wewe unao uhuru wa kuchukulia kuwa nakuja juu au chini, the choice is yours..

Kuhusu jina langu kama linakukera sana saga vyupa mimi nitakusaidia kukunywesha na safari laga. Jina langu litabakia hivihivi na nikuhakikishia hilo solidly, so mazee we just tambaa.
 
Watu wengi sana wanaanzisha makanisa kwa manufaa binafsi ikiwa ni pamoja na misaada na hizo tax excepmtions hivyo namuunga mkono Baba Askofu kwa ushauri wake kwa Serikali.. Ila kama jinsi alivyouwasilisha ndiyo iliyoleta mushkeli tumsamehe kwa kuwa naye ni binadamu na ana haki ya kukosea na kusamehewa. Cha muhimu tuzingatie alichokusudia kumaanisha kwenye ushauri wake.
 

Mazee, taasisi yeyote ile kabla ya kuandikishwa kwenye vitabu vya serikali inabidi ikidhi vigezo minimum, na hii si kwa makanisa tu. Kila mahali ndivyo ilivyo. Unaposema Kilaini ame-suggest hii criterion ya idadi ya waumini, sina hakika unachosema ni exclusive maana nijuavyo hili si geni na hujathibitisha kuwa hii criterion haikuwepo kabla ya ushauri alotoa.

Suala la kusema kutokuandikisha kanisa ni kukandamiza uhuru wa kuabudu, nadhani hilo ni suala la kikatiba. Mimi sio mtaalamu wa sheria na wala sio policy maker wala decision maker kwenye hii ishu. Ila naamini kikundi chochote kinacho-operate popote lazima kijulikane na kiwe kwenye kumbukumbu za serikali, kwa maana serikali ni muangalizi wetu sote. Vinaandikishwaje, hilo ni suala la utaratibu uliowekwa tayari.Utaratibu una mapungufu au la, hilo ni beyond the scope of this thread.
 

Jibu lake ni; kwa kanisa katoliki limeanza kwa mitume. Ref, kanuni ya Imani "....nasadiki kwa kanisa Takatifu Katoliki la Mitume" Ila imani ya kikristo according to the bible imeanza kwa Ibrahimu; manabii, mitume na kisha kristo yaani mpakwa mafuta Yesu na "kanisa la Kristo" limeanza siku Yesu alivyo fufuka nae akawa mzaliwa wa kwanza na kichwa cha wale watakaofuata baada yake.Hiyo congragation ikawa initiated rasmi na roho matakatifu siku ya Pentekoste baada ya Yesu kupaa mbinguni. This is according to Felister's deduction through the Bible sasa mwenye facts zaidi ya hii wanisaidie na ndiyo maana naamini namba sahii ya "kanisa la Kristo" ni mtu mmoja alie anzisha yaani Yesu. Ila sisi tukaanzisha vikundi ili kuwe na utaratibu wa kueleweka katika kuhubiri injili ya Yesu na hapo ndo tatizo likaanza. Naamini leo Yesu akishuka aje kufanya vetting unaweza kukuta haya makundi yetu yote hatakubali kuwa ni kanisa lake ila huko sintopenda kuingia maana ni kazi yake yeye mimi ugomvi uko kwa wale wanaopenda kujifanyia vetting kwamba wao ndo reference point ya huyo Yesu wakitumia vigezo vya akili ambazo ni nywele na kila mtu ana zake.
 

Waliokuwa wakiliamini ndiyo hao waliowafukuza hao 12 huko Israel na wakahamia Ulaya.

Niambie hilo agano la kale ni wapi kuna neno KANISA.
 
Mazee, taasisi yeyote ile kabla ya kuandikishwa kwenye vitabu vya serikali inabidi ikidhi vigezo minimum, na hii si kwa makanisa tu. Kila mahali ndivyo ilivyo.

Mpaka hapa tupo pamoja. Sina problem na taasisi kuandikishwa. Tatizo langu ni "mchujo" na vigezo vitakavyotumika.

Unaposema Kilaini ame-suggest hii criterion ya idadi ya waumini, sina hakika unachosema ni exclusive maana nijuavyo hili si geni na hujathibitisha kuwa hii criterion haikuwepo kabla ya ushauri alotoa.

Kuthibitisha kama alichosema Kilaini kilikuwepo au la is besides the point. Msimamo wangu ni kwamba mapendekezo ya Kilaini ni kinyume cha katiba. Period.


This is defeatist thinking. Kama raia wa kutosha wakijitokeza waka weka wazi maoni yao kwamba katiba inakiukwa, basi serikali itabadili msimamo wake. Serikali isiyosikiliza matakwa ya wengi inakua ya kidikteta. Serikali yetu haiko hivyo.
 
 
Loo!! mtu akitaja tu Kanisa Katoliki unaguswa kweli na kuja juu ile mbaya. Badilisha jina basi..

Mbona ikitajwa Quaran....na nyie huwa mnakuja juu.....mkuki kwa nguruwe nini?
 
Mpaka hapa tupo pamoja. Sina problem na taasisi kuandikishwa. Tatizo langu ni "mchujo" na vigezo vitakavyotumika.

Nashukuru kuwa tatizo lako liko kwenye mchujo.

Kuthibitisha kama alichosema Kilaini kilikuwepo au la is besides the point. Msimamo wangu ni kwamba mapendekezo ya Kilaini ni kinyume cha katiba. Period.

Naona tunarudi back to square one. Hivi kutoa maoni imekuwa kinyume cha katiba tangu lini?

This is defeatist thinking. Kama raia wa kutosha wakijitokeza waka weka wazi maoni yao kwamba katiba inakiukwa, basi serikali itabadili msimamo wake. Serikali isiyosikiliza matakwa ya wengi inakua ya kidikteta. Serikali yetu haiko hivyo.

Naamini kuwa katiba sio absolute and exclusive, na ndio maana hurekebishwa, kuboreshwa n.k .. na sipingani na nguvu ya umma kuishape nchi yao through katiba. Tukirejea kwenye mada ni kuwa Kilaini au Gamanywa , sio anayeandika katiba na wala hayupo kwenye mlolongo huo wa kisheria ..so its logical we can leave him out this issue , at least.
 
Makanisa kama yale yaliyojiingiza kwenye DECI wazee ni makanisa kweli au ujanja wa kupata fedha tu kutoka kwa wananchi masikini.
 
Makanisa kama yale yaliyojiingiza kwenye DECI wazee ni makanisa kweli au ujanja wa kupata fedha tu kutoka kwa wananchi masikini.

Labda useme weye pengine utaonekana huiingilii katiba au hutetei maslahi yako binafsi!
 
 
Naona tunarudi back to square one. Hivi kutoa maoni imekuwa kinyume cha katiba tangu lini?

No. Ni wewe mwenyewe ulibaki square one. Mimi nipo square two. Nasema kwamba matamshi ya Askofu Kilaini kwamba taasisi za kidinii zichujwe wakati wa kuandikishwa yanakinzana na uhuru wa kuabudu unaotolewa na katiba.


Kama ikipigwa kura ya maoni na Watanzania walio wengi wakaamua hawataki uhuru wa kuabudu, mimi sina tatizo na hilo.
 
Kwangu mimi huu ni Ushauri wa hatari kwa nchi iliyojiwekea misingi ya uhuru wa kuabudu kwenye katiba yake. Yaani watz 200 wakitaka kuabudu wasihalalishwe kuabudu! Idadi gani ni halali?

Ushauri wa Kilaini ni mbovu haukuzingatia ukomavu wa kiuongozi kwa kiongozi mkuu kama yeye kwa sababu zifuatazo:

1.Kwa kiongozi aliyekomaa kiungozi ukidai kitu ukapata inabidi unyamaze usiendelee na kidomodomo.Aliomba kodi iondolewe imeondolewa na serikali ilibidi baada ya kutimiziwa alichotaka anyamaze asiendelee na kidomodomo kwa mtu mkomavu kiuongozi.

2.Utafiti nilioufanya kwa makanisa madogo nchi mbalimbali duniani hukataa kusajiliwa na serikali kwa sababu huamini kuwa Mungu na kaisari (Mtawala) ni vitu viwili tofauti.Na kwa misingi Hiyo ya utofauti wao hulipa kodi zote serikalini kama Yesu alivyowaagiza kuwa mpeni kaisari kilicho chake kaisari (kodi} na mpeni Mungu kilicho chake Mungu (sadaka).Wao hawaigusi serikali na serikali haiwagusi kila mmoja huheshimu mipaka yake.

Sasa serikali ilikuwa inalia ipewe chake wakatoliki hawataki kulipa cha kaisari (kodi) na wanaona fahari kutomlipa kaisari chake (kodi). Makanisa mengi madogo kwa taarifa yake Kilaini hayo anayosema yana watu wachache mengi hayana mpango wa kukwepa VAT. hujenga majengo yao bila kuomba misamaha ya kodi kwenye vifaa vya ujenzi na wala hawana mpango wa kuomba VAT iondolewe.Iwe simenti,nondo,baisikeli,magari,vinanda,magitaa n.k huvinunua na VAT zake hivyo hivyo na hawataki kuomba msamaha wa kodi kutokana na imani yao ya kidini kuwa lazima kodi ilipwe kama Yesu ALIVYOAGIZA.

Labda yeye Kilaini na usomi wake atueleze ni kwa mamlaka gani aliyonayo aweza kataa kulipa kodi wakati Yesu mwanzilishi wa kanisa alilipa kodi.Huo unafuu wa kusamehewa kodi kautoa kitabu gani cha biblia au kaupata wapi? Kama Yesu Alilipa kodi na mitume wake walilipa kodi hadi akafanya muujiza wa samaki ili ipatikane pesa ya kulipa kodi yeye kilaini na papa benedicto ni akina nani wasilipe kodi? Kanisa linalokiuka hata maagizo ya Bwana wao la kutaka walipe kodi na halitaki ni hatari.Napendekeza kanisa katoliki lifutiwe usajili au likubali kulipa kodi kama Yesu alivyoagiza ili liendelee kutambuliwa kama kanisa na si genge la maharamia wakwepa kodi ya VAT waliojificha nyuma chini ya altare ya kanisa ya kugawia sakramenti.

Kushambulia makanisa madogo kayaonea na mimi kama mpiganaji wa porini AMBAYE NI SAUTI KWA WASIO NA SAUTI nasema hapana.Hongereni makanisa madogo ambao huwa mnalipa VAT kwenye bidhaa mnazonunua na ambao hamjawahi kukanyaga serikalini hata kwa mjumbe wa nyumba kumi kujikomba msamehewe kodi ya VAT.Hongereni.Nyie mtaenda huko mnakoita mbinguni na Kilaini na wenzie wataenda gizani jehanamu kwenye kona yenye moto mkali siku ya kiyama kwa kukataa kumpa kilicho chake kaisari(VAT) kama Yesu alivyoagiza.

Kilaini alipaswa ajue kuwa Kutolipa VAT siyo kitu cha kuchekelea kwa makanisa yote kama ilivyo kwa Lutheran,Angilikana,katoliki na hicho kinachoitwa Baraza la makanisa ya wapentekoste cha akina Askofu Mwasota.Kwa makanisa mengi madogo kukataa kukataa kulipa kodi kama VAT ni upotofu wa kiimani.Na ndio maana waliamua KUJITENGA NA kuanzisha yao yenye waumini wachache lakini wenye nidhamu ya hali ya juu ya kulipa kodi zikiwemo za VAT wakipinga mfumo wa kishetani ndani ya makanisa makubwa yaendayo kinyume na Yesu alivyoagiza.

Ni heri kuwa na makanisa madogo yenye watu chini hata ya mia mbili lakini walipa kodi kuliko kuwa na mikanisa mikubwa yenye mamilioni ya waumini lakini hayalipi kodi.kiuchumi ni biashara kichaa.
 
Kwangu mimi huu ni Ushauri wa hatari kwa nchi iliyojiwekea misingi ya uhuru wa kuabudu kwenye katiba yake. Yaani watz 200 wakitaka kuabudu wasihalalishwe kuabudu! Idadi gani ni halali?
.


kwa hiyo wakitokea "akinakibwetele" waachwe tu kwa sababu ya uhuru wa kuabudu,udhibiti muhimu.
 
Makanisa na dini zote zinastahili kulipa kodi bila ulalamishi wala nini. Suala la usajili limeletwa kutokana na serikali kulalamika kuwa baadhi ya makanisa ni makanisa uchwara na yanatumia misamaha isivyo.

Wengine ndo wakashauri serikali iwe makini katika kusajiri hayo makanisa. Hapa nia ni kuiepusha serikali mgogoro wa kusajiri makanisa yatakayotumiwa kukwepa kodi. Huu ni ushauri mzuri. Tatizo ni kutekelezeka kwake. Kuna uwezekano mkubwa wa kuzua lawama ya kuingilia uhuru wa kuabudu.

Wengine wanashauri serikali iwe makini katika kutoa hiyo misamaha, hata kama itasajiri kila kikundi cha kidini bila scrutiny yoyote kwani serikali haina uwezo wa ku-scrutinize uhalali wa taasisi za kidini. Serikali haina utaalam katika mambo hayo. Huu nao ni ushauri mzuri ingawa tatizo la kiutekelezaji vile vile linabaki vile vile.

Tatizo mi naona ni kuyachukulia maoni ya Kilaini kama yalikuwa na maana ya kuifanya serikali ndo iwe muamuzi wa mwisho nani awe dini na nani asiwe. Kama alivyochangia mwingine kuwa ziko taasisi za dini zisizotaka hata hiyo misamaha ya kodi kwa sababu za kiimani. Imani yao inawaambia kulipa kodi ni lazima, kwa nini waombe misamaha?

Tafsiri za maneno au maandishi ya kidini mara nyingi huwa hazifanani ndo maana tuna dini na madhehebu tofauti nyingi sana.

Kwa kuwa kiwango cha ukwepaji wa kodi kimeshafika juu, serikali ifute misamaha yoote ya kodi. Ipunguze viwango vya kodi ili vilipike bila ulalamishi. Ili kuepuka matatizo mengi ambayo tunakutana nayo leo na tutaendelea kukutana nayo ni kuondoa kabisa huu utaratibu wa misamaha ya kodi kwa mtu, kampuni au kikundi chochote.

Ikiwa serikali inampenda sana mtu furani au taasisi furani basi iwape ruzuku au itafute jinsi ya kuwafidia. Lakini kodi ilipwe bila kukwepa au msamaha. Hii itaondoa matatizo mengi sana. Itapunguza mianya mingi sana inayotumiwa na wakwepa kodi wengi. Hili ndo litakuwa suluhisho la kudumu.
 
Let us see what does the law in Tanzania says in respect of worship.

Article 19 (2) of the United Republic of Tanzania's Constitution (1977) clearly states that worship and propagation of a religion is an individual's private affair and therefore the state authority shall not involve itself in the affairs and management of religious bodies.

Have a good one.
 

hapo juu tuko ukurasa mmoja Mkuu...............

Ukiwa na system inayofanaya kazi yake inavyotakiwa.......haya maneno ya huyu Ndugu Kilaini wala yasingekuwa na maana........

....sidhani kama Kilaini kakurupuka tu........he has seen and experienced....who knows.......the ball is with the Government now.........let them take a note!
 
.


kwa hiyo wakitokea "akinakibwetele" waachwe tu kwa sababu ya uhuru wa kuabudu,udhibiti muhimu.

Mwanaluguma, hebu nipe link kati ya ''ukibwetere'' na ''idadi ya waumini + kusamehewa kodi". Sioni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…