Mpendwa kipimo kipi kitatumiwa na serikali kujua hili kweli kanisa na lipi si kanisa? Je idadi ya watu ndo calibration ya hiyo meter itakayopima hayo makanisa? Nadhani hayo yatakuwa si makanisa kwa maana ya kanisa bali NGOs, CBOs, or any other organizations. Jaribu kukubali ukweli bila kuweka hisia. Huoni kuwa Askofu Kilaini na Gamanywa hapo anatetea uhai wa Kanisa lake kwani serikali kutoa democracy ya kuamini chochote inawapa freedom wakatoliki na wapentekoste kuhama ukatoliki au upentekoste kwenda kwingine? Ndo maana siamini katika dini kabisa maana binadamu wachache wana monopolise dini kwa faida binafsi na kuacha agenda ya Mungu nje yaani Imani. Kama kweli Kilaini anaamini katika roho mtakatifu yeye anashida gani? maana Yesu alisema hataliacha kanisa mpaka ukamilifu wa dahari meaning anauwezo wakulilinda lisifutike sasa hilo lake mbona anataka kulilinda kwa nguvu ya kidunia badala ya kimungu? Kama Mungu yupo pamoja nae nani atakua kinyume nae? Na kama issue ni kodi kwani hata kanisa likiwa na watu milioni thelathini matapeli je hawata kwepa kulipa kodi? Je hata kama hao milioni thelathini ni waaminifu Askofu wao akawa tapeli je hilo kanisa halitakwepa kulipa kodi?