Askofu Lusekelo (Mzee wa Upako): Kesi ya Mbowe inakera sana na inaniumiza moyo

Askofu Lusekelo (Mzee wa Upako): Kesi ya Mbowe inakera sana na inaniumiza moyo

Ni siku ya tatu sasa akihutubia ktk moja ya safu ya mafundisho yake katika jamii. Askofu wa Kanisa la TAG hapa Ubungo Kibangu Maarufu kama Mzee wa Upako ametoa maoni yake juu ya kesi anayohisi huenda ni ya kuzingizia ya Ugaidi dhidi ya Mbowe.

Askofu huyo licha ya kudai kuwa wafuasi wa chama cha demokrasia na Maendeleo Chadema wamekuwa wakimtukana mitandao kwa kumhisi yeye na CCM ni maswahiba ametanabaisha kuwe yeye ni rafiki wa watanzania wote na vyama vyote na hata waio na vyama.

Ktk safu hiyo ambapo aligusia maswala ya Amani, Upendo na Haki ktk nchi amelalamikia kitendo cha mamlaka kumtubumu Mh Freeman Mbowe kwa makosa makubwa ya Ugaidi baada ya kuanza harakati za Kudai Katiba Mpya.

" Naamini Mbowe ni Mtu Muungwana, wangeweza kumuita na kumweleza kuwa Mzee Hii kasi yako ni kubwa punguza kidogo na angeweza kuelewa kuliko kumwita Gaidi" sehemu ya kauli zake.

Mzee wa Upako anapata taabu sana kutambua kama kweli Mh Mbowe ni Gaidi au Sio Gaidi. Huku akitanabaisha kuwa kesi hii itakuwa na Impact kubwa ndani na nje ya Taifa letu la Tanzania.

Amewashauri wenye mamalaka kuwa badala ya kumtweza Mbowe wamemfanya kuwa maarufu zaidi na kwamba Mambo kama haya yanawapa maadui zetu sababu za kuingilia Mambo Yetu kama Taifa.

View attachment 2123456
sasa nimeamini maneno ya huyu mzee
 
AMANI ya NCHI ni ya MUHIMU zaidi kuliko Mbowe au mwanasiasa yeyote yule.

Funzo kwa wanasiasa kwa hiki anacho pitia Mbowe kwa sasa ni;

Mtu yeyote yule au mwanasiasa yeyote atakaye jaribu kuchezea/kucheza na Amani ya Nchi atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria bila kujali wadhifa wake, awe CCM, NCCR, CDM, CUF, n.k atashughulikiwa kikamilifu.

Amani yetu ni kitu muhimu zaidi kuliko mtu yeyote au chama chochote kile.
team roho mbaya leo mnalala na viatu tena.
 
Atueleze ni kwanini anapata taabu kuamini ? Nadhani hakupata taabu UAMSHO walipoitwa magaidi ?. I see a pattern here.

Siamini kama Mbowe ni gaidi by the way, profile yake tuu haifit na izo tuhuma. Nadhani viongozi wengi wa CCM wana tatizo la kujiamini, personally si mwanachama wa chama chochote cha siasa. Na sijawahi kuomba uanachama hadi sasa, nasimama na haki tuu na jamii ilipo. Samia anaweza shinda uchaguzi bila ya hila wa ghilba yoyote katika uchaguzi, hamna haja ya kuwa na pressure yoyote jikiteni zaidi katika kuleta maendeleo na kuchapa kazi.

Wekeni maslahi ya taifa mbele kuliko ushindani usio na tija kwa jamii. Si lazima kushinda kwa kishindo kila uchaguzi, sheria zibadilishwe zinadumana hatua za maendeleo katika taifa.

Maasalaam.
Vipi nini maoni yako?
 
Back
Top Bottom